Ushauri na Mbinu Mbalimbali Kuhusu Uendeshaji wa Biashara ya Kuosha Magari (Car Wash)

Lughe

Senior Member
Oct 26, 2010
116
19
1280-174942860-tire-wash.jpg


Hi to everyone, and hope you're doin fine.

Nimefikiria kuwa na mradi wa uoshaji magari sambamba na huduma ndogondogo nyingine kama pressure n.k badala ya kutojishughulisha kabisa.

Ni mradi mdogo ila nimeupenda kwani is a free risk and have low operating cost as generally nahjtaji kuwa na:

1. Compressor machine
2. Stand by generator in case of Tanesco power off
3. Water tank 250ltr kwa kuanzia
4. Site/rental

Kwa estimate naweza kusanya zaidi ya 30 thousands per day kwa capital kama ya 2.4millions.

Haya ni mawazo yangu katiki pasua kichwa yangu.

Kwahiyo basi, nawaombeni ushari wenu kuhusu hii idea ya huu mradi kama inamanufaa, vilevile nitafurahi sana kujua maeneo ambayo ni mazuri/location kwa hii shughuli Ubungo, Kimara, Dar es Salaam.

Natanguliza shukrani.

WADAU WENGINE WENYE NIA YA KUENDESHA BIASHARA HII
Nataka kuinvest Dar, naomba wadau msaada wa mahali naweza fungua car wash dar ambapo naweza kupata wateja vifaa vyote ninavyo hii biashara ipo ndani ya moyo kuliko fani ambayo nimesomea mpaka chuo. Kupenda kuosha magari imekuwa ndani ya damu kwani tangu utotoni nilikuwa napenda sana kuosha magari ya baba.wakati baba alifikiri ananipa adhabu kumbe mm nilikuwa napenda.

Hivyo nimeona nifanye kitu ambacho napenda na nakifahamu. Wadau naombeni msaada wenu. Hii itakuwa ya pili yakwanza stationery nimefungua songea pia ni msaada wenu wanaJF.

THANKS IN ADVANCE
Ebwana wasalam wana jukwaa,

Kama ada ya jukwaa hili uhai wake upo kwenye kureta vitu na majambo yenye tija kwa dhumuni la wote tuondokane na maisha haya ya kimaskini na kuweza kuishi maisha yenye tija.

Niende moja kwa moja kwenye mada kuna vitu vingi vyenye tija na vinavyolipa katika maisha lakini vitu vingi, biashara nyingi zinazolipa zinahiataji pesa za kutosha kuwekeza hivyo kwa sisi maskini inakuwa ni vigumu sana kuweza hata kukalibia biashara hizo.

Lakini pia kutokana na uwezo wetu mdogo wa kimaskini na sisi kuna biashara zenye tija ambazo kwa level zetu tukijibana na kujitutumua tunaweza kuzifanya na kutoka kwenye haya maisha kwa njia yoyote ile moja ya biashara hiyo ni car wash.

Hakuna mjuzi sana wa mambo humu pia hakuna anayejua kila kitu ila hii haisababishi wewe kutokujua vitu kwa uchunguzi wangu hii biashara inalipa sana kutoka kwenye sources mbalimbali ila hapa nataka kujua tu je jumla mzima ya mtaji wa project hii ya car wash ukijumuisha vitu vyote.

Hapa nazungumzia mfano zile kidogo modern kama za kwenye shell mbalimbali mijini, napenda nijue hicho ili nianze movement zangu hivi sasa za kuzisaka hizo pesa sasa hivi.

Kwa anayejua anieleze tu minimum shilingi ngapi na maximum shilingi ngapi bila kuanisha nini na nini kinaitajika.

OCTOBER MAN

NAWASILISHA
Habari wadau,

Nimefanikiwa kupata capital na ninataka kufungua car wash sites mbili ninahitaji kujua yafuatayo:
1. Vifaa vya kutumia (capital equipments)
2. Sehemu ya kuvipata kwa bei nafuu na ubora unaoridhisha.
3. Je biashara inalipa kwa hapa Dar es Salaam?
Habarini wadau, naomba mnipe ushauri/maelekezo etc. ni muda sasa nimekua nafikiria kuanza hii biashara, lakini sijui nianzie wapi. Sina experience wala mtu wa karibu anaefanya hii biashara na mara nyingi mtu hawezi kukupa ushauri kama anakujua personally sababu ya ubinafsi na wivu wa kibinadamu.

Naombeni mnipe maelekezo hii biashara inahitaji mtaji wa bei gani? Je natakiwa nianze na nini? Vitu gani vya muhimu kuzingatia wakati wa kuanzisha na hata kuendesha hii biashara.

Angalizo sina mtaji mkubwa, so itakua vizuri kama mki simplify mambo.

Ahsante.

USHAURI NA MWONGOZO TOKA KWA WADAU
CHUKUA UZOEFU HUU MDOGO
Kuna wakati nilishakua na idea ya kufanya hii biashara na nilizunguka kwa watu wanaoifanya hii kazi walinipa uzoefu wao na pia gharama ambazo utalizimika kuzitumia.

Kwa mfano kuna Tank la kuweka maji kuanzia Lita 5,000 inategea na ukubwa wa carwash yako, ni muhimu kuweka tank kwa kuwa endapo utatumia maji direct kutoka kwenye mabomba ya Dawasco wanadai bili itakuja kubwa kutokana na pump ile ya presha inavuta maji na hewa kwa wingi hii itafanya meter kuzunguka zaidi ya ilivyo kawaida.

Pia zile mashine za kuoshea uwe nazo at least 2 ambazo kwa bei ya wakati huo (2014) zilikua kuanzia 1.5mil inategemea na ukubwa na brand ya mashine zile za Japan zinauzwa bei juu kidogo na wanadai ni imara zaidi. Usisahau mashine ya kuflonza vumbi ndani ya gari, ndoo kama 5 hivi,mpira,sabuni,uniform za wafanyakazi wako, na mishahara.

Vitu hapo juu yakupasa ununue baada ya kuhakikisha yard yako imekamilika sio mbaya ukianza na inayoingiza gari 4 kwa wakati mmoja.
USHAURI WA VIFAA VINAVYOHITAJIKA

Vifaa vinavyohitajika kwa kuanzia ni Pressure Washer hii bei yake inategemeana na ukubwa wa mashine yenyewe lakini niliwahi kuona moja Jengo la NHC posta Bei ikiwa ni laki sita kama miaka mitatu nyuma.

Kifaa kingine ni Vacuum hiki ni kwaajili ya kuvuta uchafu ndani nayo bei yake inategemea. Tatu MAJI unafikiria kazi au biashara hii basi ufikirie maji ya uhakika kama hakuna maji ya Dawasco basi kwa Dar kuna wale wanaouza kwenye Makenta.

Eneo ambapo biashara hii utaifanya hapa bei inategemea na eneo na mwenye eneo. Lakini pia kingine ni Sabuni maalumu za kuoshea magari hizi sifahamu wapo zinapatikana na bei zake sifahamu.

Vijana wa kufanya nao kazi ambao watakuwa wanaosha malipo mtakubaliana
Vitambaa vya kuoshea na kufutia magari
Polish na Airfresh

Baada ya hapo bei nadhani zinajulikana japokuwa zinatofautiana sehemu na sehemu lakini bei nayofahamu mimi ni Shilingi Elfu 10 kwa gari ndogo hizi Sedan, SUV hatchback nk.

Mengi nadhani wapo wanaoweza kuongezea kila la heri katika kulifanikisha hili

UZOEFU WANGU: VIFAA NA RASILIMALI WATU

Namiliki Car Wash huku kunduchi karibia na Eneo la Jeshi.

--Kodi ya Eneo--150,000 tshs. Na hii ilishuka kutoka 500,000 tshs wakati nafungua. Kwasababu mzunguko wa biashara ulikuwa mdogo. Bei mara nyingi ni maelewano.

--Malipo ya wafanyakazi? Na walip kwa gari. Gari tunaosha tshs 10,000. Ya kwao asimilia 30. Hesabu inatoka baada ya siku kuisha

--Bei--tunatoa huduma ya kuosha gari ''FULL'' au ''KUOSHA BODI'' na tunafanya service ya magari pia. Gharama zake?
KUOSHA FULL--10,000/=
KUOSHA BODI--5,000/=
CAR SERVICE---10,000/=
KUOSHA CARPET--10,000 mpaka 30,000

--Faida inategemeana na:
---Huduma unazopanga kutoa
---Mauzo ya vifaa vya spea--Engine Oil, Oil filter, Oil Coolants, Brake fluid, Air Filter
---Mzunguko wa wateja
---''Marketing''
---Ufanisi wa kazi...Ukiosha gari vizuri wateja watarudi
---Usalama wa mali za wateja. Kuna wafanyakazi ni wadokozi. Wakiiba hela wateja wanazoacha kwenye gari wateja hawarudi tena

Ni mchanganyiko wa vitu hapo juu vinavyochangia hela utakayotengeneza.

Gharama utakazotumia?
--Unahitaji mashine ya ''compressor'' au ''presha''
--Unahitaji ''gun'' zile mashine zinatoa maji
--Unahitaji ''vacuum cleaner'' kwa ajili ya kutoa vumbi ndani ya gari
--Unahitaji mashine ya upepo
--Unahitaji ''polish'' kwa ajili ya kung'arisha dashboard na sehemu za ndani ya gari
--Unahitaji tenki la maji
--Bili za dawasco
--Kodi TRA
--Umeme
--Kodi ya Eneo
--Usafi--ufagio, na dustbin
--Usimamizi wa hali ya juu

KUANZISHA BIASHARA YA KUOSHA MAGARI
Biashara ya kuosha magari ni mradi wa faida. Iwe una pesa za kutosha kuanzisha biashara kubwa au unataka tu kuanza biashara ndogo na kuweka pesa mfukoni, biashara ya kuosha gari kamwe haikatishi tamaa. Katika chapisho hili, lengo ni kukuonyesha jinsi ya kuanzisha biashara yako ya kuosha gari iwe kama biashara ya wakati wote.

Kuna watu ambao hutumia wakati kuokoa pesa, na kuna watu ambao hutumia pesa kuokoa wakati. Unapoanza biashara ya kuosha magari, kimsingi unalenga watu ambao wanahitaji kutumia pesa kuokoa muda.

Kadiri maisha yanavyozidi kuwa ngumu na jamii zetu zina kasi, sio kila mtu ana wakati wa kuamka asubuhi na mapema na kuosha gari lake kabla ya kuanza majukumu ya kila siku. Hata ikiwa watafanya hivyo, ni kazi kubwa kusafisha eneo la ndani na kuosha matairi yawe safi, sivyo?

Jifunze utaalamu wa kuosha gari
Anza kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu. Tembelea huduma yoyote ya kitaalam ya kuosha magari unayojua na ujifunze chochote unachoweza kutoka kwao. Unaweza kujitolea kufanya kazi bure wakati unajifunza.

Pata eneo zuri la kibiashara
Eneo ni muhimu sana kwa biashara ya kuosha gari. Eneo zuri ni nini?

Kwa mwanzo, eneo lako linapaswa kuwa lenye shughuli nyingi na wanaopata mapato ya kutosha ambao wanaweza kumudu kulipia huduma yako. Unakumbuka wakati nilisema unawalenga watu wanaotumia pesa kuokoa muda?

Unatakiwa kuzingatia sana eneo la biashara yako. Watu wanaotembelea maduka ya magari (palipo na mafundi) kawaida wanataka kuosha uchafu kwenye magari yao kabla ya kuendelea na biashara yao. Kwa hivyo, ukipata nafasi karibu na duka la magari ama fundi makenika, unaweza kuwa katika eneo zuri sana kibiashara. Vivyo hivyo kwa maeneo yenye vumbi sana, machafu.

Hakikisha kuna maji ya kutosha
Kuosha gari inahitaji maji, maji mengi. Utahitaji chanzo cha kutosha cha maji, kwa hivyo zingatia kuzingatia kwako eneo. Nimeona watu wanaofungua biashara ya kuosha magari karibu na kijito. Wengine hununua tanki kubwa la kuhifadhi maji na kujaza kila siku.

Ikiwa eneo lako lina kisima cha maji karibu, hiyo inafanya kazi pia. Jinsi ya kupata maji ni juu yako. Jambo moja ninaweza kukuambia ni kwamba hupaswi kuwarudisha wateja wako kwa sababu ya kutokuwa na maji, watakuona kama mtu usiye wa kutegemeka.

Nunua vifaa na vifaa
Jambo moja ninalopenda kuhusu biashara ya kuosha gari ni kwamba unaweza kuianzisha kwa kiwango chochote. Unaweza kuwekeza kiasi kikubwa cha pesa, ikiwa unaweza kuimudu kuanza uoshaji wa kisasa wa magari. Unaweza pia kupata ndoo mbili, kitambaa kimoja na sabuni na kuosha magari ya watu. Njia yoyote unayochagua, utapata pesa ikiwa utatoa huduma nzuri.

Kwa kadiri iwezekanavyo, pata kila vifaa unavyoweza kumudu katika biashara yako. Itaonesha wateja wako unajua unachofanya kweli. Pia utaweza kulipisha ada nzuri kwa kazi yako.

Baadhi ya vifaa hivi ni:
  • Pressure car washer
  • Towels
  • Brushes
  • Chemicals
  • Compressors
  • Conveyor
  • Mobile wash systems, etc

Ikiwa unaweza kununua vifaa hivi tangu unapoanza, sawa. Lakini ikiwa unaanza kidogo, ninashauri uwekeze pesa unayopata kupata vifaa bora kwa biashara yako ya kuosha gari.

Ongeza huduma
Unaweza kuongeza huduma kwa biashara yako ya kuosha gari ili kuongeza mapato. Unaweza kuongeza baa ndogo ili watu wapate kiburudisho wakati wanangojea gari lao. Unaweza pia kuongeza kituo cha kutazama michezo, duka la kubashiri (betting shop), n.k.

Je, ni kazi ya muda tu ama ni ya muda wote?
Kweli, hii inategemea wewe. Ikiwa huna kazi yoyote au biashara kwa sasa, unaweza kuanza biashara ya kuosha gari wakati wote. Usijali, ikiwa unafanya kazi nzuri, hakika itaweka pesa kubwa kwenye mifuko yako.

Ukienda kufanya kazi kwa wakati wote, unaweza kumudu biashara yako jinsi inavyokufaa, unaweza kuanza na mtaji kidogo au usiwe na kama nilivyokwisha sema, na unaweza kufanya kazi peke yako au kuwasimamia wafanyikazi wako moja kwa moja kulingana na kiwango cha biashara.

Ikiwa unapoanza biashara kama kishindo cha upande, utakuwa unaongeza mkondo mkubwa wa mapato. Walakini, utategemea watu wengine kuendesha biashara hiyo, kwa hivyo unahitaji kubuni mfumo / mchakato ambao hufanya iwe ngumu kwao kukudanganya. Kudanganywa ni rahisi sana wakati hausimamii moja kwa moja wafanyikazi wako.

Mwisho
Fanya kazi nzuri. Chukua tahadhari zaidi kulinda magari ya watu na kile kilichomo. Wizi mmoja, kashfa au utovu wa nidhamu utapelekea wateja wako kukukimbia.
 
Sawa. Unaweza kuwa mtaji mdogo ila naomba unipe makadirio yako na ukinipa na mfano nitafurahi sana.
 
Mkuu nilipata wazo hilo mapema last month. Nikaenda maeneo ya posta kufuatilia bei ya hizo compressor. Bei ya chini kabisa ni 3,500,000/=. Kwa hiyo jaribu kurekebisha hiyo bajeti.
 
Kama biashara unataka kuifanyia mjini lazima uongeze mtaji ili kuweka huduma ya kisasa zaidi na yenye ushindani.
 
Kwa kuanzia kabla hujafikiria kitu. Piga hesabu ya kuchimba kisima maji..weka kama Million 5 na Generator la umeme Million nyingine 5 na Lease ya eneo at minimum. Kama laki 3 kila mwezi. Baada ya hapo jazia bajeti za lazima na angalia utachukua muda gani ku-break even.

Kutokana na matatizo ya Maji na Umeme. Utavutia wateja kama kama watapata uhakika kwa kusafishiwa magari muda wote. Sio wanachoma mafuta kuja kwako halafu wanakuta vijana wako wanasoma magazeti hakuna maji wala umeme.
 
Kwa kuanzia kabla hujafikiria kitu. Piga hesabu ya kuchimba kisima maji..weka kama Million 5 na Generator la umeme Million nyingine 5 na Lease ya eneo at minimum. Kama laki 3 kila mwezi. Baada ya hapo jazia bajeti za lazima na angalia utachukua muda gani ku-break even.

Kutokana na matatizo ya Maji na Umeme. Utavutia wateja kama kama watapata uhakika kwa kusafishiwa magari muda wote. Sio wanachoma mafuta kuja kwako halafu wanakuta vijana wako wanasoma magazeti hakuna maji wala umeme.

Mkuu asante kwa mawazo mazuri ya kuwa na sustainable and independent source ya maji lakini kama mradi huu utafanyika DSM maji ya kuchimba kisima yana chumi hivyo hufanya body za magari kuoza (corrosion) yaani kupata kutu (iron+salt=rust)

Hiyo basi lazima utegemee maji ya ruvu toka DAWASCO kwa kujenga underground reservoir tanks au kuweka suspended poly tanks.

Hili ni la kuzingatia sana, pia biashara hii inaweza kuenda samabamba na refreshments au beverages.
 
Ndugu nimefanya utafiti target yako ni kiwango kidgo amapo weye tutakulipa 2500 mpaka 3000 kwa gari na kwa namana mandalizi yako yalivyo , kwako tutaleta gari upukute vumbi wakati tukisubiria siku ya kuosha tukaoshe kikweli kwa wenye viosheo. Unauweka wapi huu mradi wako pale Wami darajani ama? Maana hela yako hii yote itaishia kweneye kunua ma tanki ya maji madogo labda ma2!

Unamiliki gari? Basi nakushauri tembelea car washers hapa Dar uone how serious they are and how this is a serious business amabko kuna shemu ukiambiwa ulipe 50,000/= wala hubishi. Unapeleka gari wanafungua mpaka viti wanavitoa nje wamnalisafisha gari sehemu zote kwa mashine za kisasa ambazo hii 2.4 yako hapa labda itanunua mpira wake wa kurushia maji.

Ina one word nasema JIPANGE. Usilete utani kwenye kazi!
 
Nataka kuinvest Dar, naomba wadau msaada wa mahali naweza fungua car wash Dar ambapo naweza kupata wateja vifaa vyote ninavyo hii biashara ipo ndani ya moyo kuliko fani ambayo nimesomea mpaka chuo.

Kupenda kuosha magari imekuwa ndani ya damu kwani tangu utotoni nilikuwa napenda sana kuosha magari ya baba. Wakati baba alifikiri ananipa adhabu kumbe mm nilikuwa napenda.

Hivyo nimeona nifanye kitu ambacho napenda na nakifahamu. Wadau naombeni msaada wenu. Hii itakuwa ya pili yakwanza stationery nimefungua songea pia ni msaada wenu wanaJF.

THANKS IN ADVANCE
 
Tafuta eneo kuanzia salenda brdge (Ali hassan Mwinyi Road) hadi Mbezi Beach, maeneo ya tangi bovu kuelekea mbele kidogo.

Au maeneo ya msasani na Oysterbay.

Maeneo hayo ndio maeneo yenye watu wanaohitaji zaidi kuoshewa magari na hawajali bei wanajali huduma bora.
 
Mkuu, KIGAMBONI. Hamna Carwash ya maana na kuna watu wengi wanahamia wenye magari ya kifahari na wanauwezo. Fanya survey between Monday-Friday. Jioni wakati wanarudi home kutoka Town. Ukienda weekend utakutana na magari ya watu wanaoenda shamba/Site na beach places haitakupa picha nzuri, ila katikati ya week utapacha picha halisia. Mungu bariki mimi nahamia huko mwakani so I will be u customer too :)
 
Duh!

Nasemaga huu u capital sijui nani aliluleta duniani. Niko naosha gari sehemu nimekaa kama masaa mawili.

Nakula supu pemben hapa Sinza nimeona mama mmoja wa kichaga hapa pembeni ya hongera ameshaosha gari zaidi ya 20 hii ni masaa machache niliopo na akila gari ni buku kumi yaani 10,000.

Nimewiwa kukujulisha mwenzangu kama una sehemu nzuri ya biashara na una kile kitu ka kepital ndugu yangu haka kabiashara kanalipa na sidhan kama kanaitaji TRA, yaani tumepaki pembeni tumezagaa kama tunazika msibani kinondoni kumbe unasubiri mwenzio atoke.

Wajasiriamali wa JF pambaneni jamani wakati weni huu baycort iko kwa ajili yenu.

Naihisi bado wanakopesha awa jamaa
 
Unamjua RIZ moja? Anzisha kaaa woshi jijini, kama humjui ndo utamjua.
 
Hivi waziri wa biashara ni nani, au wa Mazingira, au Tawala za mikoa. Naomba namba ya simu ya mmoja wao nimshauri apige marufuku biashara za kuosha magari kwenye curbs. Ukiingia restaurant kidogo tu ukirudi unakuta huwezi kukanyaga ardhi kufika kwenye gari, mimaji imetanda kila mahali. Wanafanya biashara bila leseni, bila kodi wala usajili, wanaharibu mazingira, wanavuruga mipango miji ya jiji, wanaiba vitu, esp ukikataa kuoshewa. Serikali iko wapi?
 
Hivi waziri wa biashara ni nani, au wa mazingira, au tawala za mikoa. Naomba namba ya simu ya mmoja wao nimshauri apige marufuku biashara za kuosha magari kwenye curbs. Ukiingia restaurant kidogo tu ukirudi unakuta huwezi kukanyaga ardhi kufika kwenye gari, mimaji imetanda kila mahali. Wanafanya biashara bila leseni, bila kodi wala usajili, wanaharibu mazingira, wanavuruga mipango miji ya jiji, wanaiba vitu, esp ukikataa kuoshewa. Serikali iko wapi?

Kodi yako imekusaidia nini wewe?
 
kodi yako imekusaidia nini wewe?
Ahsante.

Mimi kulipishwa kodi halafu mwingine halipishwi inaniumiza kwa sababu mzigo wa kodi unakuwa mkubwa zaidi.

Tax base ya Tanzania (yani asilimia ya wananchi wanaolipa kodi) ni ndogo mno kwa hiyo kodi na tariffs mbali mbali zinakuwa kubwa. Tunaolipishwa kodi ni wale tulio kwenye uchumi rasmi tu, tunabeba mzigo wa wengine.

Waosha magari ovyo ovyo ambao hawasajili, hawalipi kodi, hawana leseni, wanatuumiza tunaowalipia. Wanachafua mazingira, mimaji kila mahali, wanaharibu mipango miji. Wapigwe marufuku.
 
Ahsante.

Mimi kulipishwa kodi halafu mwingine halipishwi inaniumiza kwa sababu mzigo wa kodi unakuwa mkubwa zaidi.

Tax base ya Tanzania (yani asilimia ya wananchi wanaolipa kodi) ni ndogo mno kwa hiyo kodi na tariffs mbali mbali zinakuwa kubwa. Tunaolipishwa kodi ni wale tulio kwenye uchumi rasmi tu, tunabeba mzigo wa wengine.

Waosha magari ovyo ovyo ambao hawasajili, hawalipi kodi, hawana leseni, wanatuumiza tunaowalipia. Wanachafua mazingira, mimaji kila mahali, wanaharibu mipango miji. Wapigwe marufuku.

Inapunguza vibaka!
 
Back
Top Bottom