Nasibu Thabith
Member
- Feb 5, 2017
- 37
- 72
Mimi ni kijana mpambanaji, baada ya kupambana sana na kazi ya bodaboda kwa muda mrefu sasa nahitaji kuiacha na kufanya mishe nyingine, katika kuwaza sana kipi naweza kukifanya nikapata wazo la kufungua car wash.
Katika tembea zangu kuna sehemu kuna car wash ambayo jamaa ameshindwa kuiendesha kutokana na changamoto za mhusika mwenyewe, kuulizia nikaambiwa kodi yake ni 300,000 kwa mwezi na unatakiwa kulipia miezi 6 ambayo inakua ni 1.8m.
Hapa mfuko wangu unasoma 3ml.
Lengo la kuja kwenu ni kuomba ushauri kwa wenye uzoefu wa hii biashara ya car wash, je kwa pesa hii niliyonayo ninaweza fanikisha kuanza biashara hiyo?
Je kodi hiyo ipo sawa katika kazi hiyo? Ni vifaa gani napaswa nianze navyo?
Ni kipi napaswa kukijua zaidi kabla sijaingia huko, karibuni wana jamvi tujadili na kupeana madini ili tupate kujikwamua na kupata kusonga mbele.
Na mwenye idea nyingine ya mtaji kama huo naomba anaisaidie kunijuza ili nipate kufungua ubongo. Asanteni