Biashara kukodisha magari Mbeya na taxi

Selwa

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
543
524
Ataenzisha biashara ya Uber au Bolt Mbeya atapata pesa sana, pamoja na magari executive ya kukodisha.

Mimi kila nikiwa na kazi kule inagharimu ofisi yangu million 5 kusafirisha dereva na magari mabosi yaende kule ili kuwazungusha, sasa sisi wafanyakazi wengine tukifika tunabaki hohe hahe, hakuna magari ya kukodi kuzunguka kwenye mizunguko yetu wala taxi.

Taxi za mkoa wa Mbeya ni mbovu na zimezeeka mno huwezi kupanda ukiwa na roho ndogo. Wajasirimali mfikirie hili. Pamoja na kuwa na taxi mbovu bado unachajiwa bei za ajabu.

Unaweza lipa 30,000 hadi 40,000 umbali wa mwenge- posta tena. Kukodisha kwa siku gari mbovu mbovu imechoka mtu anataka 100,000 hapo ni mzunguko wa jiji dogo kama sinza.

Kwa kweli wenye mahoteli mbeya angalieni hili pia, muwe na magari kwajili ya wateja wenu kutuzungusha, tutalipa. Unaweza jikuta kwa wiki umetumia 250,000 kwenye usafiri tu. Inaumiza sana wageni tunapara shida.
 
Shida ya jiji la Mbeya ni mzunguko mdogo wa fedha, kwa hiyo hizo biashara unazozitaja haziko viable kufanyika, ndio maana hakuna anaeanzisha. Mbeya ni kama jiji-kijiji, shughuli za kiuchumi na mizunguko iko so limited, sasa hauwezi ku compare na jiji kama la Dar. Hivyo, hizo biashara za bolt au taxi au gari za kisasa za kukodi haziwezi kuwa profitable, ndio maana wafanyabiashara wanaogopa kuzianzisha.
 
Mkuuu Mbeya ni ushamba tu. Hili hitaji lipo. Nimekuja huku mara nyingi na makampuni kibao wote tunapata shida hio, inatugharimu million 20 usafiri mbeya kwa mwaka, nikicheki na wenzangu wa kampuni nyingine nao hivyo hivyo, ilifika wakati tulipanga kununua gari likae huku ila sasa unaweka kwa nani muaminifu.

Hitaji lipo na ni kubwa. Leo hii akianzisha mtu kesho wakinga wote wataanzisha. Ikifika saa moja usiku hamna usafiri popote sio basi wala bajaji. Alafu unaitwa mji.
 
Mkuuu Mbeya ni ushamba tu. Hili hitaji lipo. Nimekuja huku mara nyingi na makampuni kibao wote tunapata shida hio, inatugharimu million 20 usafiri mbeya kwa mwaka, nikicheki na wenzangu wa kampuni nyingine nao hivyo hivyo, ilifika wakati tulipanga kununua gari likae huku ila sasa unaweka kwa nani muaminifu. Hitaji lipo na ni kubwa. Leo hii akianzisha mtu kesho wakinga wote wataanzisha. Ikifika saa moja usiku hamna usafiri popote sio basi wala bajaji. Alafu unaitwa mji.
Mbeya sehemu gani mkuu usafiri saa 1 usiku hamna? Nilikua huko wiki iliyopita nimekaa siku 6
 
Kama una gari binafsi hauwezi kuelewa sisi ambao tunatoka mikaoni na tunakaa uyole ikifika saa moja hauna usafiri
 
Nimesema nimetumia daladala,bajaji na gari binafsi(la mwenyeji wangu).

Bajaji hadi saa 2 usiku nilikua napanda. Sikupingi labda kutakua kuna maeneo yana hiyo changamoto.
 
Ikifika saa moja hamna usafiri mjini ni nadra sana. Hii ni maeneo posta. Mabasi na bajaji mpaka uende mafiati kabwe au mwanjelwa
Sasa fikiria mtu ambae yuko posta anatembea umbali gani kufika vituo vikuu afu fikiria ni mgeni hata hajui hivi vituo.
 
Ataenzisha biashara ya Uber au Bolt Mbeya atapata pesa sana, pamoja na magari executive ya kukodisha.

Mimi kila nikiwa na kazi kule inagharimu ofisi yangu million 5 kusafirisha dereva na magari mabosi yaende kule ili kuwazungusha, sasa sisi wafanyakazi wengine tukifika tunabaki hohe hahe, hakuna magari ya kukodi kuzunguka kwenye mizunguko yetu wala taxi.

Taxi za mkoa wa Mbeya ni mbovu na zimezeeka mno huwezi kupanda ukiwa na roho ndogo. Wajasirimali mfikirie hili. Pamoja na kuwa na taxi mbovu bado unachajiwa bei za ajabu.

Unaweza lipa 30,000 hadi 40,000 umbali wa mwenge- posta tena. Kukodisha kwa siku gari mbovu mbovu imechoka mtu anataka 100,000 hapo ni mzunguko wa jiji dogo kama sinza.

Kwa kweli wenye mahoteli mbeya angalieni hili pia, muwe na magari kwajili ya wateja wenu kutuzungusha, tutalipa. Unaweza jikuta kwa wiki umetumia 250,000 kwenye usafiri tu. Inaumiza sana wageni tunapara shida.
mkuu mara nyingi hayo makapuni yakifika mnapenda sana kutumia gari za aina ipi ili tuchungulie fursa vizuri
 
Ikifika saa moja hamna usafiri mjini ni nadra sana. Hii ni maeneo posta. Mabasi na bajaji mpaka uende mafiati kabwe au mwanjelwa
Sasa fikiria mtu ambae yuko posta anatembea umbali gani kufika vituo vikuu afu fikiria ni mgeni hata hajui hivi vituo.
Sawa mkuu,pole ila ungekua specific ningekuelewa.
 
Back
Top Bottom