Naomba kujuzwa biashara ya kuosha magari (car wash)

Burden47

New Member
Sep 12, 2019
3
9
Habari wakuu,

Naomba kwa mwenye ufaham wa biashara ya car wash,anipe Ushauri ni kiasi gani cha fedha kinatosha kuanzisha biashara ya kusha magari ya saizi ya kati?

kama kutakua na mchanganua wa budget nzima itakua vizuri.

Nina milioni 4 je inatosha?
 
Presha Mashine nzuri 1.2m-1.5m

Woover(vacum cleaner) 300K- 500k

Tank atleast 3000 litre 400K(sina hakika na hii bei) ukiweza nunua lenye ujazo mkubwa zaidi ni vizuri.

Vitambaa, brush, normal polish, wax, sabuni hivi tenga 50k-100k na haitoisha.

Eneo inategemea na ulipo.

NB: upatikanaji wa umeme na Maji ni wa muhimu sana kuzingatiwa.
 
Presha Mashine nzuri 1.2m-1.5m

Woover(vacum cleaner) 300K- 500k

Tank atleast 3000 litre 400K(sina hakika na hii bei) ukiweza nunua lenye ujazo mkubwa zaidi ni vizuri.

Vitambaa, brush, normal polish, wax, sabuni hivi tenga 50k-100k na haitoisha.

Eneo inategemea na ulipo.

NB: upatikanaji wa umeme na Maji ni wa muhimu sana kuzingatiwa.
shukrani sana kaka
 
Umepata ushauri mzuri sana kutoka kwa Half American. Ila naongezea hili, hakikisha mashine (pressure washer) isiwe chini ya 2600PSi utanishukuru kwa hilo. Mi nina car wash nikanunua mashine ya 1200psi yaani nguvu ya kutoa uchafu ilikuwa ndogo sana. Ikabidi niingie gharama mara mbili maana nilinunua mashine nyingine. Ni vizuri umeomba ushauri kwanza.
 
Biashara nzuri niliwahi fanya mwaka 2017 Mwenge, Dar es Salaam…..

Ujinga wa hii biashara ni rubber za pressure pump kufa mara kwa mara na haichukui week 3 na inazengua tena…..sikubahatika mafundi waaminifu na kila nikipeleka kwa fundi kkoo gharama za matengenezo na spare si chini ya 120,000 hapo bado usafiri

(nakumbuka nilipata hadi demu kwenye uber nikiwa narudi na mashine yangu nyumbani na huyo demu akaja kuwa mwanangu sanaa hadi leo hii, maisha kitu cha ajabu sanaaa )

Haya njoo kwenye challenge za wafanyakazi wengine miyeyusho kwenye hesabu mara wanataka ujira uwe pasu pasu kwa mauzo. Yani kama kuosha nnje na ndani ni 10,000 wapuuzi wanataka kuchukua 5,000 nzima na huku mimi ndio nalipa gharama za pango, umeme, sabuni, repair za mashine, gharama za serikali ya mtaa (takataka probably kuna vi gharama flan vina rise tu).

Kama utakomaa mwenyewe ukiwa na msaidizi ni sawa na kuwa mkali kwenye hesabu wafanyakazi wapumba.vu sana ndio maana mkoloni alikuja africa na kiboko kuna watu bila viboko hawaendi.

Haya njoo kwenye wateja wa kulia lia kuna wateja wanataka service nzuri alaf hela ya kijinga hawafiki bei. Hii nayo uangalie.

Inawezekana ila biashara sio rahisi. Jipange.
 
Back
Top Bottom