Baada ya biashara ya urembo wa magari sasa nipo natazamia hizi zifuatazo.

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wakuu Habari za siku ?

Natumai wengi ni wazima wa afya na wenye kuumwa mpate kupona na kuendelea na mapambano.

Baada ya kuingia kwenye biashara ya urembo wa magari, kiukweli nimejifunza vitu vingi. Ikiwemo changamoto zake na jinsi biashara nzima inavyoendeshwa.

Biashara hii imenifungulia milango mingi na kujuana na watu mbalimbali na kutengeneza chaneli nzuri na mahusiano na wateja wengi

Mwanzo kabisa nilikuwa nafikiria projekti ya biashara ya makontena yale ya kuivishia Ndizi. Nikafanya mchanganuo nikaona hii gharama zake ni kubwa zaidi.

sasahivi naomba kuuliza kwa mtu mwenye ufahamu wa biashara ya.

•kuchinja magari
•biashara ya kuosha magari(car wash)

Kama kuna mtu anatokea mpanda, kahama karibuni sana haya ndio maeneo ninayotazamia zaidi.

La mwisho kwa mfanyabiashara wa dar es salaam mwenye mzigo wa Perfume za ikeda kwa bei ya jumla naomba tuwasiliane.
 

Attachments

  • 8E11551B-DA07-4143-8BFB-84B3C2AE6566.jpeg
    8E11551B-DA07-4143-8BFB-84B3C2AE6566.jpeg
    1.3 MB · Views: 11
  • 5E4A9ABC-41FA-44B6-BC6E-9B212CD131D3.jpeg
    5E4A9ABC-41FA-44B6-BC6E-9B212CD131D3.jpeg
    1.1 MB · Views: 11
  • 9E8337BD-7328-47A3-9AC0-85EB59C92D16.MOV
    23.1 MB
Hivi mkuu hizi ikeda Kuna kipindi zililalamikiwa kuwa zinaleta maumivu ya kichwa au wajanja walikuwa waneingilia business
 
Back
Top Bottom