Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Usafiri enzi zile Mwanza yetu

Unaongelea Santamaria za KIRUMBA za JUZI Hapa!? Za wale Watoto wa Mzee AWADH?

Watu wamepanda GEZA ULOLE! Gia Tatu!
Breki TOFALI halafu dereva Mzee Joseph Yuko GONGO 24/7!

Na ukiikosa hio unadandia TRANS AFRICAN BUS ya kwenda MUSOMA ukifika nyakato au Igoma haisimami, unalegezewa tu na dereva UNAACHIA Body mwenyewe!

Unasema nini wewe!

Wacha bana.

hahahah we jamaa kweli wa kitambo mwanza.
 
nimefungua thread kwa shangwe nikafikiri umeweka picha za treni.
jana nimefurahije Pinda kuturekebishia reli ya Dar-Mwanza. Raha sana kusafiri na treni.

back to topic: ok i dont know what u guys are talking about
 
We lzm utakuwa mchawi!
Ulijuaje hizi habari?

Au nyie ndio ile Mwitunga! Mliotoroka kule sengerema au mahina!
Manake na huko kwa wachawi ni mwisho!

Lami ya Pasiansi-Nyakato iliwekwa lini?
 
Hilo mkuu muulize yule mdaku babu upako Eiyer,
Mi niko viwanja vya wagalatia toka mwaka 89! Sipo mwanza.

Hahahah sawa sawa, ila usiwaripue wagalatia bana ndio wanaofanya dunia iwe na amani. 1989 au 2009?
 
Last edited by a moderator:
Kuna express moja (enzi hizo pale Mwanza daladala zikiitwa Express) ilikuwa ikiitwa KABOMBEE EXPRESS ikifanya safari zake Igoma-town. Hiyo ni mwaka 1984. Kwa kweli express hiyo ilikuwa nzuri sana na wanafunzi wa kipindi hicho tuliokuwa tunaipanda hatuwezi kuisahau pamoja na makondakta wake waliokuwa wastaarabu sana hata kwa wanafunzi ukilinganisha na express zingine. Express hiyo haikukaa Mwanza zaidi ya mwaka mmoja baadae tukasikia ilihamishiwa nadhani Dar. Wanafunzi tulisikitika sana. Route hiyo ya Igoma-town pia kulikuwa na Ngollo Express, Majestic Express, Sadoti Express, Josh Express, Nzegenuka, Bajber Express kwa uchache.
 
Mambo mpango> town-nyakato.
Ngosha> hii ilikua chai maharage, town-igoma
 
mwanza ya henzi hizo usafiri wa mjini tuliuita express sijui nani alituletea neno daladala magari hayakua mengi kama leo lakini kwa chai maharage tulitumia saa 1 kutoka miti mirefu mpaka igoma barabara ilikua vumbi kweli tumetoka mbali

Mkuu usidanganye, miaka hiyo Mwanza, Igoma mpaka Nyanguge ilikuwa lami iliyokuwa imejaa mashimo! Ogopa mashimo ya lami Wewe! Hivyo siyo kweli kwamba ilikuwa ya vumbi maana kuna sehemu zingine mnakuta kuna lami nzuri kabisa, mfano enzi hizo lami ya kati ya mabatini mpaka Mwatex ilikuwa bomba sana! Mashimo kwa mbali unayakuta kuanzia pale VETA mpaka Igoma!
 
Wadau wa rock city enzi zile mnakumbuka Mwanza hapakuwa na usafiri wa vipanya kama leo. Vipanya vilikuwa Mabatini na Kirumba tu lakini Igombe kulikuwa na min bus zikiitwa Toto Tundu, Mayeji na Jalijalalam, Igoma kulikuwa na Last Boy na Mkuyuni air Jordan.

Jaijalalam aka safari na muziki ...kuna busi liliitwa umoja wa wazee kutokana na kuchakaa kuanzia mjini mpaka igoma.Enzi hizo kabla ya chai maharage
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom