Tulieni, hii ni nadhalia tu hakuna ww3, marekakani hapendi vita ambayo ana uhakika kuwa kombora linaweza kutua kwenye ardhi yake na kuua japo mtu mmoja ndani ya ardhi ya marekani, ndiyo maana huwa wanapenda kukimbilia kupigania hukohuko mchokozi aliko ili kuepuka maafa yasifike kwake, ndiyo maana walihamaki kupita kiasi ilipopigwa WTO na OSAMA. nDIYO maana hafanyi kitu chochote kwa Korea ya kaskazini kwakua anafahamu kuwa Korea ana bastola inayoweza kupiga Alaska na kwingineko ndani ya Marekani. Marekani itakuwa tayari kuondoka Syria tena kiulaini ili kuepuka balaa la mrusi na wenzake. Anafahamu kuwa korea wala URUSI hawana cha kupoteza kama vita ikitokea. marekani ina cha kupoteza kingi kwakuwa ina vitega uchumu vilivyotapakaa dunia nzima, starehe na maisha ya kifahari ya kila aina ukilinganisha na urusi, china, korea kask. Itakuwa vigumu Marekani kuvilinda vitu vyake vyote kama vita kubwa ikizuka. Isitoshe Marekani anafahamu kuwa Urusi imefanya maandalizi makubwa na ya muda mrefu ya vita ya aina ya nuclear kuliko marekani. marekani sio wajinga wanapoona maisha na mali zao ziko hatarini, ndio maana walikimbia Vietnam na Somalia walipoona idadi ya marekani wanaouawa inaongezeka.