Urusi yajiandaa na Vita ya Tatu ya Dunia (WW3)

Urusi yajiandaa na Vita ya Tatu ya Dunia (WW3)

Hamna rais namkubali kama Vladimir putin.Africa tumekosa watu kama kina Putin.tungepata watatu tu Africa ingekuwa inatoa misaada ulaya na marekan
 
mkataba waliouvunja ni ule ambao marekani na urusi walikubaliana kuwa mrusi atakuwa akipeleka marekani makombora ya nyuklia yaliyochakaa ili mmarekani akayaharibu na ile uranium isiweze tumika tena katika silaha,pia marekani nao wanapeleka russia nao wanaharibu yale ya wa marekani,

sasa kumbe wakati warusi wanafanya kama walivyokubaliana,mrusi kagundua kumbe marekani yeye mjanja kweli,alikuwa akiyaharibu kwa namna ambayo mda wowote anaweza kureverce process na hiyo uranium ikaweza tumika upya katika mabomu,
ndo maana putin kasitisha huo mpango
sababu za kusitisha huo mkataba zipo wazi sana. Mrusi kasema hawezi kushirikiana na Mmarekani wakati marekani haonyeshi vitendo vya kiurafiki. Marekani anatumia lugha za kibabe na vikwazo dhidi ya urusi wakati huo huo anamuomba Urusi wapunguze silaha za nyuklia.
 
Issues sio hayafiki, intercontinental missiles zinafika bara lolote, issue ni ku penentrate ndani na kuleta madhara, America wana dome ya kuzuia makombora yasifikie ardhi yao thou sio lazima dome ziwe accurate 100%,Pili nchi za mwenzetu records nyingi zipo wazi ni chache inakua siri ya nchi hasa technology iliyotumika ila number ya vifaa wengi wanaweka ata man power yao, mfano nikuulize swali dogo tu Russia ana aircraft carrier ngapi na America wapi maana nisije kua nina urge na layman

Russia ina aircraft carrie moja tu na sababu zipo wazi. kijiografia Russia haina bahari kubwa kama US na hii ndio sababu pekee inayomnyima mrusi kuwa na Aircraft carrie nyingi. lakini amewekeza kwenye zana nyingi very modernized na nzito sana za baharini kama vile Corvettes ambapo Mrusi anazo 81 na Mmarekana hana hata 1.
 
Russia alikuja Syria kupigana kwa miezi michache tu ! lakini cha Ajabu takribani mwaka na siku kadhaa anashindwa kuja na Mbinu ya kumaliza vita isiyojulikana itaisha lini ambayo akiendelea kuwa kichwa ngumu itamgharimu mabilioni ya dola na kushindwa kuiendesha, hapo ndio utajua Russia sio mjinga kama hizo propaganda za WW3.
Russia anachoumiza dunia ni silaha za Nyuklia ila sio powerful kama mnavomjadili

hiyo style ya Russia ni sawa na dume anaomba kuingiza kichwa tuu kwa demu.. kumbe dude halina mabega kichwa kikizama na kiuno pia kinazama. Alitangaza kuwa anaenda Syria kwa miezi Mitatu lakini lengo lilikuwa kwenda kukaa syria milele ndio maana juzi senate ya Mrusi imepiga kura na kuruhusu kuwa sasa jeshi laweza kukakaa syria kwa muda wowote ule linaotaka.
 
Tulieni, hii ni nadhalia tu hakuna ww3, marekakani hapendi vita ambayo ana uhakika kuwa kombora linaweza kutua kwenye ardhi yake na kuua japo mtu mmoja ndani ya ardhi ya marekani, ndiyo maana huwa wanapenda kukimbilia kupigania hukohuko mchokozi aliko ili kuepuka maafa yasifike kwake, ndiyo maana walihamaki kupita kiasi ilipopigwa WTO na OSAMA. nDIYO maana hafanyi kitu chochote kwa Korea ya kaskazini kwakua anafahamu kuwa Korea ana bastola inayoweza kupiga Alaska na kwingineko ndani ya Marekani. Marekani itakuwa tayari kuondoka Syria tena kiulaini ili kuepuka balaa la mrusi na wenzake. Anafahamu kuwa korea wala URUSI hawana cha kupoteza kama vita ikitokea. marekani ina cha kupoteza kingi kwakuwa ina vitega uchumu vilivyotapakaa dunia nzima, starehe na maisha ya kifahari ya kila aina ukilinganisha na urusi, china, korea kask. Itakuwa vigumu Marekani kuvilinda vitu vyake vyote kama vita kubwa ikizuka. Isitoshe Marekani anafahamu kuwa Urusi imefanya maandalizi makubwa na ya muda mrefu ya vita ya aina ya nuclear kuliko marekani. marekani sio wajinga wanapoona maisha na mali zao ziko hatarini, ndio maana walikimbia Vietnam na Somalia walipoona idadi ya marekani wanaouawa inaongezeka.
Hata sikuelewi unachoongea.... mara Vietnam mara Somalia? wakati ukweli marakani ndio anaogopwa sababu ana wingi wa silaha na ana uwezo wa kupigana kushinda vita ni kuamua tu the issue ni civilian pekee ndio wanalindwa ila uwanja wa mapambano hamna wa kitunisha kifua na Marekani.... Ndio maana Historia za Zamani ukisikia Jeshi limeshinda ni hakuna msalie huko mtoto mzee sijui mama mjamzito mifugo n.k yote ni kisu tu... Ndio maana kuna watu wanajidai ati Hezbollah kamshinda Muisrael my as. ukitizama unakuta wanalia lia hasara kuu wamepata kuanzia ya watu na silaha wameishiwa... MAREKANI HIVYO HIVYO ANAWAKOMESHA BALAA wajinga huja na kusema MArekani haijawahi shinda vita.... kaa hivyo hivyo ujuipooze
 
Hahah hapo ulipomalizia ni kazi tu Ndo umeua hahah
Ndio maana England ishaona mapema na kujitoa umoja wa ulaya. Na yeye ndio anapokea kiwango kikubwa cha gesi kuingia ulaya ashaofia kushambuliwa hatari na ndio maana anajalibu kuwa pande zote
 
israel wana influence kubwa huko marekani kwasababu marekani wengi ni born again(walokole),wanaona israel ni kabila la mungu,na hivyo wanawajibika kulisaidia kwa hali na mali,
lakini katika mgogoro kati ya marekani na Russia,
israel hawezi kuegemea upande mmoja kamwe kwani israel na russia pia wana uhusiano mkubwa,idadi kubwa ya wananchi wa israel,asili yake ni urusi
Hahah asee we umechanganyikiwa, naipenda Russia lkn kudanganya eti wamarekani wengi ni born again ni uongo first class.
 
Si marekani na Russia wapigane halafu ulaya nayo iingilie halafu mashariki ya kati yani tena waharibiane miji yao vibaya yawe maafa makubwa kabisa na china na NK nao waingilie halafu na bara la America ya kusini iingilie kisha watumie nuclei wapoteza waanze upya uchumi kisha sisi Africa tubaki hivi hivi tuongoze uchumi wawe wanakuja kutudai madeni yao na kutuomba misaada

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Baada ya miaka10 tutakuwa maskini wa kutupwaaa
 
Jamani mmemsikia JOHN KERRY Leo akizungumza na waandishi wa habari huko Washington, jinsi anavyolialia kuhusu Vladimir Putin na Urusi take.

John Kerry hawezi kazi. Analia kwa UN anafikiri hatujui kuwa wao ndio haohao UN. Anachofanya ni kupotosha mass.
 
Jamani mmemsikia JOHN KERRY Leo akizungumza na waandishi wa habari huko Washington, jinsi anavyolialia kuhusu Vladimir Putin na Urusi take.
Hapo ndiyo basi tena. Obama anataka àmalize viziri sio kwa aibu. Wanaowasukuma marais wa marekani kuingia kwenye vita ni wenye viwanda na biashara ya silaha. Bila kulazimisha vita ajira na kodi vinatoweka, serikali ndo mnunuzi mkubwa wa silaha hizo na inanunua kwa mali itakayopatikana kwenye uwanja wa vita kama vile mafuta au madini. Marekani haendi kupigana sehemu ambayo hakuna utajiri hata siku moja. Makampuni ya madege na makombora ndo yanayoituma marekani ikapigane sehemu zenye mali au akapigane na kiongozi anaeonekana kubumbulisha dili. Kiongozi ambae haendi kupigana wanaweza hata kupanga kumdhuru apishe wengine. Marekani ni nchi ya wahuni waliokwenda kutafuta mali pale hawarembi. Pale kila kitu ni chakinyonyaji kila mtu ananyonywa vibaya sana kuanzia mwanamichezo, mfanyakazi, msanii, hadi mwanchi wa kawaida. Msanii akipata shilingi 100 kwa kazi yake ujue kuna aliyepata 1000 kwenye kazi yake hiyo
 
Karibu ulichoongea chote havina fact,

1. unasema najifanya mchumi uchwara kuliko Russia upo wrong sijifanyi ila vita ni automatic vinatia hasara na vikizidi lengo ulilojiwekea unaanza kutoa akiba yako... kuna makombora yalikuwa yanarushwa angani kutokea baharini yanapita juu ya anga la iran yanadondokea Syria nadhani walifanya twice ilaka kwao... wakaacha.

2.Hasara kama nilivyokuambia ukiplan vita unakuwa na bajeti yake so muda ukizidi unaanza kutoa silaha za akiba ndio hasara yake... same like Saudia kwa Yemen yaani ukiona mtu anaomba Mazungumzo ujue kesha zidiwa au hataki tena kuendelea kupata hasara. Sasa na Mmarekani kamstukia kamwambia no more mazungumzo endeleza kichapo umalize ugali wako...huku mboga imebakia mchuzi una chumvi nyingiiii😀😀😀😀

3.Urusi unaposema ina Wananchi wengi sana sijui umejisemea tu kama upo kijiweni sigimbi! Population ya Marekani ni zaidi ya million 320 na ushee na Russia ina Pupulation ya watu zaidi ya million 146 sijui ndio usichofahamu hicho na kama ulimaanisha idadi ya matajiri nchi hizo bado marekani yupo juu kwa ma billionaire tena wanalipa kodi sio Russia ni genge la Matajiri wakiongozwa na raisi wao

Marekani kulinda Maslai yake ipo kwenye Katiba yao na wanailinda katiba yao kwani ndio Jadi yao na kiongozi atakayeshindwa anajiuzulu tu anapisha mwingine... uzalendo..

Mkuu kusanya Nondo ndio uje i hope humu utajifunza Mengi sana ukishakubuhu kaongombee uongozi kwenye siasa utakuwa fit 2020
Kwahyo unataka kuniambia kwamba Moscow hawajajiandaa kwa hilo?
Huu ushabiki wa vijiwen unauleta pasipo hata kutathmini
 
Hata kama Alikiri but tuliona Marekani akijitoa na kuipisha Nato japo naye ni Mwanachama.... ila Lawama zote kaangushiwa British...

Nadhani Marekani anajuta kujiondoa kwani alistahili yeye kumuua Gaddafi anyway labda zile jamaa zilifadhiliwa na Marekani so zikawa zinatumika kama Remote controller tu
Dah! Hivi unachokiandika unakijua lakn au mihemko tu?
 
Kwahyo unataka kuniambia kwamba Moscow hawajajiandaa kwa hilo?
Huu ushabiki wa vijiwen unauleta pasipo hata kutathmini
kwa vyovyote vile vita ni ghali sana. Ndo maana Marekani hendi pigana sehemu ambayo haitarudisha gharama zake au lazima atafute mikia kama akina Blair wamsaidie gharama. Mpango wa Trump ni kuitawala tena Afrika ili kuzikomba kwa haraka mali zisizotumika ipasavyo au zenye mwelekeo wa kuinemeesha zaidi Urusi, ulaya au China kuliko Marekani
 
Back
Top Bottom