Kama ukitaka kuwa fair dunia nzima hasa ya wanyonge isimame nyumna ya mrusi. Huyu bwana mkubwa ni chimbuko la maovu mengi kuanzia Mashariki ya kati, amerika ya kusini na kaskazini, afrika. Yuko nyuma ya migogoro ya wayahudi na waarabu ambacho ndicho hasa kiini halisi cha ugaidi unaotusumbua hivi sasa. Kusema ukweli.... we acha tu, hata kule marekani kwenyewe hakuna raha, wamarekani wengi wanaishi kama wakimbizi huku mabwanyenye wachache saaaana wakihodhi kila kitu. Wamarekani wa kawaida kama mimi wanasota sana ndani ya nchi yao wenyewe, wengi wanalazimika kufanyakazi kwa masaa 18 kwa siku, wengine wanalazimika kuishi kwa njia ya ushoga (unaolewa hata kama wewe ni mwanaume) ili upate mahali pa kulala, kula, kutibiwa na mahitaji mengine. Asiyefanyakazi na asile kwelikweli. Masikini hawapewi elimu ili waendelee kuwa cheep labour, na kweli wengi hawakusoma, kama akitaka ajinasue lazima afanye sanaa ya kiukweli sio kama hii ya akina nanihii hapa kwetu wanaoimba kwa kubana pua na uso kuonekana kama wanang'olewa kucha zao kwa kileo. Yaani kule ni fanya saa au acha kabisa (all or none) hakuna half way.