sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Hello wanajamvi, great thinkers.
Wiki chache zilizopita kuna babu yangu upande wa mama alifariki
Katika mali alizoacha kuna nyumba na warithi ni watoto zake akiwemo mama yangu, mama wadogo zangu wawili na wajomba zangu wawili.
Sasa tatizo linapokuja ni kwamba hakuna anaetaka kurithi hio nyumba kwa sababu nyumba hii babu alikuwa anafanya matambiko yake kulingana na tamaduni za kabila, maana babu alikuwa yupo katika koo ya kichifu
Ni nyumba yenye eneo kubwa kiasi na ipo maeneo ya mjini.
Hofu kubwa ni juu ya hayo matambiko yake aliyokuwa akiyafanya, na hata kina ndugu waliokuwa wakiishi nyumba hio kila moja kaondoka baada ya msiba kwa hofu ya hayo matambiko yake.
Sasa hapa kilichobaki ni kufanya maamuzi juu ya hii nyumba maana kila moja anaogopa kuishi humo,
je iuzwe hata kwa hasara, ipangishwe kwa wapangaji ili watuambie ama kuna kuhofia, iwekwe dhamana kwenye mkopo wa benki waiuze wenyewe au kifanyke kipi.