Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

A stupid thinking capacity! Narrow minded...!

mkuu ungejibu hoja na sio kuwa na jazba.

Kuendelea kwenu kupiga porojo na kushindwa kujibu hoja japo moja ni kudhihirisha tunachoongea kina ukweli na nyie ni waongo.
 
CDM ni mabingwa wa kudai demokrasia nje ya chama, lakini ndani ya chama demokrasia ina utata mkubwa
 
Tujuze Mkuu huo muda wa kutangaza nia ya kuomba kuwa Raisi kupitia CHADEMA utafika lini? Maana kama Zito angekuwa anaufahamu asingekuwa anahangaika kutangaza sasa! Kimsingi huo muda uko tayari na ndiyo maana yeye kishatuonyesha NIA yake ya kuutaka URAISI wa JMT hivyo si kosa kwake. Anayotamka Mzee Mtei kumwambia Zitto kuwa ajenge Chama kwanza si sahihi mbona wakati ule Zitto anagombea Uenyekiti wa CHADEMA huyu Mzee alimjia juu Zitto kana kwamba ameguswa sehemu za SIRI kulikoni na CHADEMA?

shangaa.
 
mwanasiasa makini hawezi kuongelea mambo kama hayo ya kugombea urais kwani ni mapema sana sisi vijana tunajifunza nn kwake zito akiwa kama kiongozi? NINGEPENDA Zitto aongelee ni namna gani chama itukomboe na umaskini tulionao kumbe naye ni mojawapo kula rushwa huku anaongelea ushuzi usiotusaidia
 
Mkuu Molemo, alichofanya ZZK sio kutangaza kugombea urais kupitia Chadema, bali kutangaza nia ya kuiomba Chadema kumpitisha kama mgombea wa Chadema 2015!. Naomba sana utofautishe kati ya "kutangaza nia" na "kutangaza kugombea"!.

ZZK alipotangaza nia, mimi nilimuunga mkono na kutangaza nia ni jambo jema na jambo la kheri na nikatoa wito kabisa kuwa kila mwenye nia na aitangaze!, hivi kuna ubaya gani?. Hebu kanisome hapa Urais 2015 tusimlaumu Zitto; Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa ...

Lakini ZZK alipojitangaza rasmi kuwa hagombei tena ubunge na badala yake "atagombea urais kupitia Chadema" nilimpinga!. Nilimwambia wazi, that was wrong!, hakupaswa kujitangazwa, bali alipaswa tuu kuonyesha vitendo vya ki presidential candidate ndani ya chama, ili wenzake ndio wamuone na kumuomba agombee na sio kujipigia debe na hapa nilimtahadharisha Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!. Wenye uwezo wa kumtangaza mgombea ni Chama na sio mwan achama individual!.

Ila lazima mkubali, mkatae, ndani ya Chadema kuna double standards za hali ya juu!, kuna baadhi ya mambo yakifanywa na kina fulani ni halali, ila wakifanya kina fulani inageuka ningwa!.

Tatizo ni kuwa ndani ya mioyo ya wana Chadema wengi, wanaye mgombea wao mioyoni mwao, sio tuu kuwa mgombea huyo anakubalika sana kwao, bali anaabudiwa!. Kitendo cha ZZK kujitokeza anaonekana kama kumkufuru huyo mungu mtu anaye abudiwa!. Na kwa wasio jua, mimi naujua msimamo wa huyo mgombea wenu kipenzi kuhusu kugombea au kutogombea urais na usome hapa Msimamo wa Dr. Slaa Kwenye Urais 2015 ...

Unashauri kamati kuu itoe miongozo, hivi kumbe Chadema haina demokrasia ya kila mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote ni mpaka kamati kuu itoe miongozo!.

Tena kwa vile ZZK ni rafiki yangu, na kabla hata ya huo urais kuna uchaguzi wa viongozi wa Chadema, nitamshauri agombee tena Uenyekiti na this time hakuna kujitoa mpaka kieleweke!.

Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?. Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?, sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile", na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!, hivi huyo mgombea wenu kipenzi, kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.

ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba, atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa, atazivuna kura zote za CUF kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.

Nashauri, baada ya Mzee Mtei kukikabidhi chama kwenye "safe hands" za mkwewe, his advisory role yake ibaki limited kwa insiders tuu wa chama na sio ku express his public opinion publically as if chama bado ni chake!. Heshima yake kama muasisi ipo pale pale, lakini kwa sasa chama sio chake tena, sasa chama ni cha wanachama!, tena Mwenyekiti Mbowe anatakiwa kujipambanua kabisa kwa hili kuwa "amekata kabisa zile mothers apron strings" ili isje onekana kina Mzee Edwin Mtei ndio bado wanaendesha chama by proxy kupitia kwa wakwe zao!.

Ili chadema kuonysha ina "practice what it preach" lazima iache democracy i prevail!.
Go ZZK Go!.

Pasco.

WE Pasco unamdanganya rafiki yako Zitto.

anahusishwa Na chama kipya cha CHAUMA. kama anakubalika kama unavyodai si ajiondoe Chadema ahamie kwenye chama chake kipya wewe na wafuasi wake mkamuunge mkono huko huko alafu tuone mtafika wapi

mshauri ahamie CHAUMA alafu ndo tutajua anakubalika kwa kiasi gani
 
chadema bana,sasa huyu kiongozi anaamini kuwa chama chake ni cha kidini na kikabila,hiyo ni hoja ya ccm,na yeye anakubaliana nao kwasababu hayo maneno hapo chini yanathibitisha hilo.Kwahiyo yeye anakubaliana kabisa na hoja hizo,na solution yake yeye ni kwamba yeye ndiye mwenye uwezo huo wa kuifuta hiyo dhana.Hilo linaonekana kabisa kuwa chadema mnakubaliana naye ndiyo maana hakuna hatua zozote mnazochukuwa.Na hilo mkiliacha liendelee,mje kukurupuka close to 2015,mtakuwa mmeliwa kubwa.Chukueni hatua mapema,nilishasema kuwa mchukuwe maamuzi ya either kusuka ama kuonyoa,vyote vitakuwa na manufaa kwa chama chenu.
Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao...

Halafu kuonyesha kwamba hizo hoja za ukanda na udini anazishabikia dhidi ya chama chake kwa masalhi yake binafsi,kauli hiyo hapo chini ni ya kwake,kujionyesha kwamba anaonewa kwasababu either si mchagga,ama pia si mtu wa kaskazini.Kuna member humu ambao wanazungumza lugha hizo hizo lakini kwa ukali zaidi,ila zina kila symptons za huyo Zitto...
Zitto alisema: "Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.
As if chama chake kilisema kuwa watu wa Kigoma hawana uwezo wa kuwa marais...Hicho ni kijembe kuwa chadema(chama chake),ni chama kisicho na imani na wagombea wasiokuwa wa kaskazini ama wachagga.

CDM,kusema muendelee kunyamaza,bila kuchukuwa hatua ni sawa na mdharau mwiba ambapo mguu huota tende.Kunyamaza eti kusema yataisha yenyewe ndilo hilo hilo,msipoziba nyufa ni dhahiri mtajenga ukuta,inaweza ikawa too late kwenye ujenzi wa ukuta huo given the time factor.

Kama mnakubaliana na kiongozi wenu wa juu kuwa chama chenu ni cha kikabila,kidini na kikanda,chukueni hatua kuiondoa hiyo dhana.

Na kama hamkubaliani na kiongozi wenu huyo,pia chukueni hatua.Ndiyo maana ya kusuka ama kuonyoa,ndiyo maana ya kutokudharau tende,ndiyo maana halisi ya kuziba nyufa.

Pia anaamini kuwa ndani ya chama chake kuna udikteta...

Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa."



Kazi kwenu.
 
dada
wewe ni mtambo wa kutunga uongo.
zitto aseme lingine wewe upindishe lingine. una soni kweli kichwani mwako mudada

Wewe kweli umesoma thread unayochangia? Maneno hayo yako kwenye thread isome kwa umakini.
 
Mkuu nakubaliana na wewe hana nguvu kisiasa kama unavyodai; je inakuwaje mtu ambaye hana nguvu kisiasa anawafanya hamlali kwa kumpiga madongo; je kinaogopwa kitu gani? Mimi nadhani ikiwa kama ni kweli hana nguvu za kisiasa basi mngefuata mkondo wa demokrasia badala kutumia nguvu nyingi kujaribu kumnyamazisha; hivi mathalani leo mh. Didas Masaburi atangaze atagombea uraisi kupitia CCM unafikiri kuna atavunja shughuli zake kujibizana naye?

Chama
Gongo la mboto DSM

kweli kabisa..kama jamaa ameporomoka kisiasa,kwanini wasile wa mbuzi na kumuacha kijana ajinafasi.after all hiki si ni chama cha demokrasia?au kwao demokrasia ina maana ingine?
 
anafikiri watu wote ni wavivu wa kufikiri kama yeye.
Tunaona kinachoendelea, cdm wanadhihirisha rangi yao.
Kwa mtindo huu watajimaliza kabla ya 2015.

Uchaguzi ni mwaka huu hadi mnaleta kelele humu? Nyie vipi achanaeni na uroho wa madaraka, kwanza kijengwe chama hadi vijijini hayo mengineyo 2015.Vijana wa siku hizi mna taabu sana hasa mkivipata vihela vyenu vya rushwa kelele sana.
 
Eti
"watu wa kigoma msiwe wanyonge mnaweza kutoa rais"
-kama vipi aende hukohuko akawe rais wa LEKA DUTIGITE
 
kweli kabisa..kama jamaa ameporomoka kisiasa,kwanini wasile wa mbuzi na kumuacha kijana ajinafasi.after all hiki si ni chama cha demokrasia?au kwao demokrasia ina maana ingine?

Kelele za mbu zinakela, kwa hiyo lazima akae kimya.
 
Kama Zotto anaona anavyofanya ni sawa basi aachwe atangaze anavyotaka CDM iendelee na harakati zake za kukijenga chama. Wakati ukifika wanachama wataamua ni nani anafaa muda bado upo. Wale wote wanaofaa kugombea urais kwa tiketi ya CDM ikiwa ni pamoja na Zitto wachunguzwe kwa karibu. Kuwe na mkakati wa kufuatilia kwa karibu vitendo vya watarajiwa kugombea na yatakayojitokeza yatumike kuwapima wagombea. Hii ni muhimu sana hasa hili tatizo la rushwa lazima liangaliwe muda wote kwa kuwa rushwa imekuwa tabia sugu kwa wanasiasa wengi hapa Tanzania na si ajabu likjiingiza hata CDM!!!!
 
Wenzake wako mtwra, lindi, namtumbo, ngara n.k kwenye kuendeleza chama yeye anashinda kwnye matamasha ya LEKA DUTIGITE na kutangaza nia ya kuwa rais... Nasema akalale mbele
 
Sema vyo vyote lakini huyo mla rushwa hakuna labda uupe uraisi ndani ya jumba yako

unaweza kuthibitisha kuwa zkk ni mla rushwa?
Mbinu zenu za kujaribu kumchafua hazitofua dafu.
Zkk ni jembe la ukweli ndomana anawatia kiwewe.
 
Mkuu Molemo
jibu la maswali yangu ni walewale? Mimi ID yangu ni moja tu; nimekuuliza maswali madogo ya msingi huna majibu; ni kipengele gani cha katiba ya Chadema mh. Zitto amekikiuka kwa kutangaza malengo na azma zake za kisiasa?

Chama
Gongo la mboto DSM

Hivi wewe unafikiri tatizo ni Zitto kutangaza nia ya kuutaka urais? Labda kama hutaki kuelewa kutokana na hulka zako humu JF. Issue hapa ni Zitto na uhalali wa umri wake katika kugombea urais na yeye kila baada ya miezi mitatu kuwa anaibuka na kutangaza kuutakaka urais. Umri wake ni wazi haumruhusu na hiyo katiba mpya hakuna anayejua kama itaaccomodate huo umri wake wa miaka 39 hiyo mwaka 2015. Swali ni Je kama hana vigezo wala sifa kwa sasa inakuaje anatangaza kuutaka urais? Nini lengo lake hasa maana wenzake wote wako busy na ujenzi wa chama. Najua hutaelewa maana mara nyingi nimegundua ni hulka yako kutoelewa.
 
Back
Top Bottom