hivi maana ya demokrasia ni nini? kwa nini watu wanaweweseka sana kwa Zitto Kabwe jutangaza nia yake? mara kadhaa amesema 'IWAPO CHAMA KITAMPA RIDHAA" sasa tunashindwaje kusoma na kuelewa maana ya haya maneno? je, yeye ni dikteta ya kwamba atajichagua mwenyewe? chama si kina kamati kuu halmashauri kuu na mkutano mkuu? hivi si ndio vikao vitakavyompitisha mgombea wa CDM? Kuanza sasa kumwekea kauzibe ni kuifinya demokrasia, pili ni kuwapa nafasi wale wenye hoja dhaifu za ubaguzi, mwacheni azungumze wajumbe ndio watapembua nani anafaa na nani hafai
hoja ya kwamba hajishughulishi kujenga chama pia yaweza kuwa disqualification factor kwake wakati muafaka utakapowadia, maana kila mtu si atajinadi? yeye ni nani, kafanya nini kwa chama na kwa taifa? kama zitto hashiriki M4C then wapinzani watatumia kete hiyo kumgaragaza, let nature follow its course jamani, mbona Barack Obama alionyesha nia ya kugombea urais wa Marekani toka 2004? au huko hawakujua demokrasia ni nini?