Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Moses Mashalla, Arusha na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | Oktoba 06, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amekitikisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa hatua yake ya kutangaza kuwania urais 2015, baada ya mwasisi wake, Edwin Mtei kumuonya kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

Kauli hiyo ya Mtei imekuja siku chache baada ya mbunge huyo kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.

"Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga," alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 umekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Alisisitiza kwamba siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini akasema kuwa ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza.

"Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua," alisema.

Huku akimwagia sifa mbalimbali Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, Mtei alisema kwa upande mwingine, Katiba ya Tanzania kwa sasa, inamnyima Zitto sifa za kuwania urais mwaka 2015 kwa kuwa hadi kufikia mwaka huo atakuwa amefikisha miaka 38, huku Katiba ikielekeza kuwa mgombea urais anatakiwa awe na miaka isiyopungua 40.

Alipoulizwa ya kwamba endapo uchaguzi mkuu ujao utafanyika huku Watanzania wakiwa na Katiba Mpya iliyopunguza umri wa kuwania urais, Mtei alisema endapo mbunge huyo atapambana kuhakikisha umri huo unapunguzwa, basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia.

"Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri."

Zitto apinga
Akizungumzia kauli hiyo ya Mtei, Zitto alisema: "Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa."

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

"Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani," alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.

"Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao," alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... "Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu."

Septemba 26, mwaka huu Zitto alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais mwaka 2015, alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200. Miongoni mwa maswali hayo lilihusu tetesi kwamba anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Katika majibu yake Zitto alisema: "Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.

"Nimefanya kazi kubwa katika ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka 10.

"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola.

"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndiyo msimamo wangu. Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.

"
Alipoulizwa kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa Katiba alijibu: "Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndiyo maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika Katiba Mpya."

My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
 
Pengine safari hii atasikiliza huu ushauri. Ameamua kwa makusudi kuwa CONFUSER.
Dawa ya watu wa namna ni kuwatimua mapema, ni bomu zito litakalolipuka mbele ya safari.
Hana nia njema, alikuwa mpambabaji, now he has changed, likely cz has interests to protect.
 
Zito anajidanganya sana,aache kuropoka,anakuwa kama hajaenda shule!,subiri muda ufike utangaze nia yako,sasa hivi jenga chama kwanza.
 
kwa kweli namsihi aangalie maneno ya busara ya wazee wanayompa na siyo kuropoka na kiongoz mzur anateuliwa na watu na siyo kusimama majukwaani na kujitangaza ovyo ovyo kwani jamni ikulu kuna nini
 
Tabia ya mtu haifichiki gharama tunayoipata sasa ya kusulubika ni matokeo ya kumchagua mtu aliyepigania urais kwa muda mrefu hata yeye alisema hayahaya maisha bora kwa kila mtanzania. Tutamchagua tumtakae muda ukifika ya nini kujiuza mwenyewe?
 
Mwasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Edwin Mtei amemuonya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuacha kutangaza mambo ya Urais sasa kwani anasababisha mpasuko ndani ya CDM na badala yake ajikite kukijenga chama mpaka muda utakapofika ili chama kitoe utaratibu.

Mzee Mtei amesema amemshauri mara kadhaa Zitto umuhimu wa kutulia kama wenzake ndani ya chama na kukijenga chama lakini mbunge huyo amekuwa mkaidi na hasikii.

Pia Mzee Mtei amesema endapo mbunge huyo ataendeleza harakati zake za kutaka umri wa Urais ushuke hadi miaka chini ya 40 ili tu yeye apate nafasi ya kugombea basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia na mwenye uroho mkubwa wa madaraka.

Akijibu madai hayo ya Mzee Mtei, Zitto Kabwe amewataka wazee ndani ya CHADEMA kuheshimu Demokrasia na kusema anaamini ni yeye atakayeweza kuishinda CCM mwaka 2015 na anataka Mzee Mtei akiwa bado hajafa amshuhudie jinsi atakavyobadili nchi akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Source: Mwananchi Jumamosi.

My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Kila mtu na nani mungine ukiacha zitto na mbunge wenu wa maswa??
 
Na ndicho kitu Mzee Mtei anashauri.Wapo watu makini kama kina Dr Kitila Mkumbo lakini kamwe huwezi kuwasikia wakiongea hovyo hovyo.

Lakini huyuhuyu Dr. Kitila Mkumbo kuna uzi humu humu jukwaani akimsifu ZZK 2015 kwamba ni mtu makini na asiyeyumbishwa. Bahati mbaya natumia simu ningekuletea hiyo post uione.
 
Unadhan Kamati kuu itampinga mtei wakat mkwe wao? huyo mzee hana lolote anataka mwanae akae ikulu sasa anaona zito ndo kikwazo chama cha familia na serikal mnataka ya family...pumzka we mzee mda wa vijana huu...zito kamua baba
NI kweli nakubalina na wewe kabisa ni family Kama vile mtoto ni mjumbe wa nec bagamoyo mama ni mjumbe wa nec mtwara na baba ni mwenyekiti wa Chama kwi! Kwi! Kwi! Kwi
 
Mwasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Edwin Mtei amemuonya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuacha kutangaza mambo ya Urais sasa kwani anasababisha mpasuko ndani ya CDM na badala yake ajikite kukijenga chama mpaka muda utakapofika ili chama kitoe utaratibu.

Mzee Mtei amesema amemshauri mara kadhaa Zitto umuhimu wa kutulia kama wenzake ndani ya chama na kukijenga chama lakini mbunge huyo amekuwa mkaidi na hasikii.

Pia Mzee Mtei amesema endapo mbunge huyo ataendeleza harakati zake za kutaka umri wa Urais ushuke hadi miaka chini ya 40 ili tu yeye apate nafasi ya kugombea basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia na mwenye uroho mkubwa wa madaraka.

Akijibu madai hayo ya Mzee Mtei, Zitto Kabwe amewataka wazee ndani ya CHADEMA kuheshimu Demokrasia na kusema anaamini ni yeye atakayeweza kuishinda CCM mwaka 2015 na anataka Mzee Mtei akiwa bado hajafa amshuhudie jinsi atakavyobadili nchi akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Source: Mwananchi Jumamosi.

My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.
Mimi nawashangaa sana kila siku mnamtaja zito,mnakumbuka KUBENEA ALISHASEMA ZITO ANAWASILIANA NA WA KINA NANI?Mbona watanzania mnasahau mambo haraka?
 
Ndani ya vyama vyetu vya siasa hakuna mtu yoyote yule mwenye hati milki ya ugombea wa udiwani, ubunge au uraisi

Mimi sidhan kama kuna haja ya sisi wana CDM kutumia nguvu nyingi sana kubishana na mwanasiasa mchemfu kama m_zito, sis tuendelee na shughuli za kukijenga chama, tumwachee tuu aendelee kupiga 'mayoe' adi achoke! 2015 kura ndizo zitakazo mnyamazisha! tena tutamnyamazisha adi kwenye ubunge ili akimbilie kwa wamagamba vizuri!
 
Na ndicho kitu Mzee Mtei anashauri.Wapo watu makini kama kina Dr Kitila Mkumbo lakini kamwe huwezi kuwasikia wakiongea hovyo hovyo.

Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012.

Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa.Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.

Wanaomuunga mkono Dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko Mbowe lakini pia kwamba Dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo Dk. Slaa anaweza kuwa Rais ajaye.

Kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa Mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao. My take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015.Source: Nilikuwa Uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu Kitila.

HUU UZI UNAUKUMBUKA????
 
Back
Top Bottom