Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Mkuu huyo Peri uliyemjibu naye ni kundi lao.Ni walewale wenye ID 10

Mkuu Molemo
jibu la maswali yangu ni walewale? Mimi ID yangu ni moja tu; nimekuuliza maswali madogo ya msingi huna majibu; ni kipengele gani cha katiba ya Chadema mh. Zitto amekikiuka kwa kutangaza malengo na azma zake za kisiasa?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Zitto Zuberi Kabwe hana nguvu hiyo anayodhani (na unayodhani) anayo! Fanya utafiti utabaini vijana wanaotaka mabadiliko walishaachana na Zitto kitambo tangu enzi za utetezi wa Dowans. Hana umaarufu huo unaojaribu kuutengeneza hapa. Kwanza alishinda ubunge kwa mbinde. Umaarufu wake kule kijijini Kigoma umeporomoka kwa kasi ya ajabu. Pili, mvuto wake wa kisiasa umepungua mno. Hayupo kwenye orodha ya watu wanaoaminiwa katika jamii hivi sasa (pamoja na vijitihada vyake vya kukataa posho na kadhalika). Hana tofauti na Jakaya. Amefulia kisiasa.

Uthibitisho wa kufulia, ni hizi kauli zake tatanishi wakati huu ambao wenzake wanahamasisha mabadiliko vijijini, yeye anahamasisha migogoro ya fikra (kuhusu vyeo) as if hilo ndilo jambo la msingi mwaka huu.

Kama kweli ana nia ya kugombea Urais, ni bora angefanya kazi ya ziada KUREJESHA IMANI ya wananchi kwake! Kwa sasa haaminiki! Na sijui kama hajui hilo. Watu wanamwona kama mtu MVURUGAJI, mtu ASIYEELEWEKA, kichwa ngumu, mpenda SIFA BINAFSI na Fisadi anayechipukia (rejea mkanganyiko wake kwa Dowans, Tanesco nk). Badala ya kupoteza muda wake na matangazo ya Urais, ni bora angeshughulika KUREJESHA IMANI.

Hakika hana nguvu hiyo. Na leo akiamua kuondoka Chadema, athari yake ni ndogo kuliko anavyojifikiria yeye.

Mkuu nakubaliana na wewe hana nguvu kisiasa kama unavyodai; je inakuwaje mtu ambaye hana nguvu kisiasa anawafanya hamlali kwa kumpiga madongo; je kinaogopwa kitu gani? Mimi nadhani ikiwa kama ni kweli hana nguvu za kisiasa basi mngefuata mkondo wa demokrasia badala kutumia nguvu nyingi kujaribu kumnyamazisha; hivi mathalani leo mh. Didas Masaburi atangaze atagombea uraisi kupitia CCM unafikiri kuna atavunja shughuli zake kujibizana naye?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Mkuu mimi napenda sana approaches za CHADEMA.

ZZK lengo lake ni kuleta mtafaruku katika CHADEMA ili apate sympathizers kisha ajitoe na probably sympathizers wamfuate huko aendekano.

Hilo litazigawa kura za CHADEMA kwa kuzifanya zipungue na kuiwezesha CCM kuua tembo kwa ubua

Tumuache tu ZZK akukuruke mbona kigezo cha umri tu kinamdisqualify
 
Naweza kusema nyie ni mitambo inayozalishwa pale LUMUMBA, tunawajua sana nyie ni wazandiki wanafiki
na wanyanganyi na kamwe hamtofanikiwa, najua kuwa mnapokea madau tofauti tofauti kama Pasco anawezidi dau

Hii kamwe haitawasadia na watanzania kamwe hatutayumba siku itafika tutachukua nchi yetu

Copy to Pasco, Ritz, zomba, Nnauye Jr, chama, Ecoli, OTIS, Kata nyodo, malaria SUgu (RIP), Jenifa, peri,

Mkuu
Narudia tena mimi ni mwanaccm huru naishi kwa kujitegemea; sitegemei ajira; posho; takrima ya aina yoyote ile kutoka CCM au serikali ya CCM; usikwepe kujibu hoja kwa kutumia uzushi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mimi nadhani ipo kila sababu ya Zitto kujiepusha na kauli kama hizi zenye mwelekeo wa kuleta tafrani; kwani haraka ya nini kama anahitaji urais si asubiri muda ukifika atatangaza nia yake na chama kitamsikiliza. Wasiwasi wangu hapa ni kwamba hizi kauli anazitoa katika hali ambayo inalenga kuleta mgongano kabla ya 2015, swali la kujiuliza je anafanya hivyo kwa masilahi ya nani?
 
Nilikuwa mpenzi wa Zitto kwa staili na aina yake ya siasa lakini tangu alipokuwa kwenye kamati ya Bomani naona kidogokidogo ameongeza vionjo vinavyofanya nianze kumfuta akilini.
 
Nimekuwa nikimheshimu sana Molemo humu Jf na nikiamini ni mpiganaji mahiri wa CDM. Hata hivyo, the way alivyojenga chuki binafsi dhidi ya Zitto na mbaya zaidi anaziexpress hadharani, kwa sasa namuona kama pandikizi hatari sana kwa chama. Molemo kwa makusudi kabisa amepotosha hii habari, kwa mfano anamlisha Mtei maneno kama vile kusema Zitto amekuwa mkaidi na hasikii. Ukiisoma stori, maneno hayo hayajatamkwa na Mtei. Kwenye kipengele cha Zitto kutaka katiba isimzuie mtu kugombea kwa umri, mzee Mtei ametumia neno "itaonekana" mbinafsi. Molemo akabadilisha na kusema "atakuwa" mbinafsi na mwenye uroho wa madaraka!!!
Naombeni nyie vijana wa CDM hapo makao makuu mtuambie kama chama chetu kina makundi, na nyie mnafuata kundi gani. Sisi tunatambua CDM hakuna makundi, tunawakubali viongozi wetu sawa, na binafsi naamini kati za Slaa, Mbowe na Zitto, yeyote akiwa raisi, nchi itakuwa imepata kiongozi bora. Acheni kutufarakanisha na Zitto...

Sihitaji kuheshimiwa na mtu kama wewe,kwani sijazoea unafiki.Unafiki na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa ndiyo umefikisha Taifa hapa lilipo.Siwezi kuunga mkono mtu yeyote asiye na hekima anayetaka kugawa CDM vipande vipande.Nakuambia wazi NO na haitatokea Asilani.Vyama vya hovyo hovyo vipo kibao na mtu yeyote anayependa vurugu aende huko kufanya vurugu zake.
Narudia ni bora tutawaliwe na CCM hata miaka mia moja ijayo kuliko kuruhusu wavurugaji kwa ukaidi na ubinafsi wao kutaka kuua chama.Wapo mashujaa waliokufa huku wakipigania chama na damu zao zinalilia haki Ardhini.
Kwa akili yako unadhani mtu yeyote akipingana kimawazo na watu wanaotaka kuvuruga chama basi ni lazima wawe wafuasi wa fulani au mapandikizi? Hiyo ni akili mgando iliyojengwa katika fikra za kimaskini na za ki-CCM.Kama wewe ni kundi la fulani basi usidhani watu wote ni wa hovyo hovyo au ni cheap kiasi hicho.
 
Ah wapi kijana gani anamkubali Zito mbinafsi na mroho wa madaraka mimi simpendi amekaa kiswahili na kimipasho mipoasho mbishi sijui kwa kua ni Muha kila kitu anajifanya yeye ndio anaweza mtu ameshindwa hata kuweka Mke nyumbani ndio ataweza kuongeza Nchi ZITO JIPANGE HAUKUBALIKI COMMENTS ZA FACE BOOK ZIKUDANGANYE Na njaa zako

Mkuu mimi;
Kama ni suala la mke ni moja ya vigezo vya kugombea uraisi basi Chadema ilifanya makosa sana kumsimamisha Dr. Slaa na mpaka sasa hivi Dr. Slaa anaishi na kimada; sasa sijui itakuwa ajabu gani Zitto naye atagombea akiwa hana mke; nadhani kama ni uroho wa madaraka waulize hao kina Mtei wanaofanya kila juhudi kumtaka asigombee; je wanamtengenezea nani njia?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
kwa taarifa yako cdm hawana ubavu wa kumtimua zkk,
wanajua kuwa ni jembe na anakubalika, ndomana wanagwaya.

Hao kina mdee, mnyika na lisu bado wachanga sana kwenye sasa na hawalingani hata kidogo na zkk.

Tukirudi kwa mbowe, uwezo wake ni mdogo sana,
ndomana hata bungeni anapwaya kama kiongozi wa kambi ya upinzani.
Wanaotoa hoja nzito huwa ni zkk na lissu kidogo.

Cdm wanajua uwezo mkubwa wa zkk ndomana wanatumia kilambinu kunyamazisha.

Msaafu wa Biblia wasema: "Acheni ngano na magugu vikue pamoja, wakati wa mavuno ndipo tutakapochambua ngano na kisha magugu kuyatupa." Tukiyang'oa magugu wakati yamechangamana na ngao kuna uwezekano wa baadhi ya ngano kung'oka na kutupwa jalalani pamoja na magugu.

Mbinu za uongozi uliotukuka na sheheni hekima na busara katu si kila mtu kumshughlikia namna ile ile. Mtakatifu Benedict wa Nursia mwanzilishi wa shirika la Watawa Wabeneditini duniani alisema: unapoosha vyombo, kuna vingine vinakutu, kuna namna ya pekee kuvishughulikia vyenye kutu visitoboke, ukiviparuza sana vitatoboka.
 
Chama kina wenyewe hicho. namshangaa sana Zitto kuwa amesahau hilo wakti wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho pale alipoamua kutaka kuchuana na Mbowe.

kazi ipo. nayakumbuka maneno au comment za Mtei kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya. Je kwa mtazamo ule Zitto atapita hapo.

Poleni sana.
 
Nilikuwa mpenzi wa Zitto kwa staili na aina yake ya siasa lakini tangu alipokuwa kwenye kamati ya Bomani naona kidogokidogo ameongeza vionjo vinavyofanya nianze kumfuta akilini.

Yes, kinachonishangaza kijana kukataa ushauri wa wazee, kama hawasikilizi hao nani atakayemsikiliza? Nakumbuka kulikuwa na tafrani za Zitto kuleta migongano kadhaa siku za nyuma kabla hajaenda kutibiwa India. Kuna siku hata mama yake mzazi alisema wazi hata vyombo vya habari vilimnukuru akisema, "Zitto si msikivu, mara kadhaa nimeshauri lakini hashauriki."

Kuna dalili za wazi Zitto kabwe akishaamua kitu ni yeye hakuna wa kumpinga, ndio maana tunaona pamoja na ushauri wote mzuri wa hapa JF katu hayuko tayari kushaurika na anaendelea na yale yale aliyokusudia ambayo si muda mwafaka.

Kwamba hajavunja katiba ya chama halina ubishi, lakini pamoja na hayo kuna taratibu nyingine za kichama ambazo zinatumika katika kuleta mshikamano na uwajibikaji wa pamoja. Kwa kinachoendelea siku uchaguzi wa Chadema utakapowadia na kuona Zitto anaenguliwa nafasi aliyo nayo sistashangaa maana kijana anayefaa siyo peke yake, kuna wengi sana sasa hivi tena wanaofaa na wenye kujitoa zaidi kwa ajili ya chama.

Hatuwezi kujenga hoja ya uwepo wa Zitto muda mrefu chamani kwamba yuko sahihi katika matamko na maamzi yake. Timu ya mpira iliyopanda daraja hatutegemea kwamba wachezajiwake wote ndio watakaofaa kupambana na kiwango cha ngazi ya ligi kuu. Ndio maana kunakuwa na usaili wa kiwango kinachotakiwa. Zitto aangalie hayo, avumaye baharini ni papa, lakini bila kufahamu wa kutosha kumbe kuna akina nyangumi.
 
Chama kina wenyewe hicho. namshangaa sana Zitto kuwa amesahau hilo wakti wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho pale alipoamua kutaka kuchuana na Mbowe.

kazi ipo. nayakumbuka maneno au comment za Mtei kuhusu tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya. Je kwa mtazamo ule Zitto atapita hapo.

Poleni sana.

Sidhani kama kuna tatizo hilo katika CHADEMA, kumbuka mbunge Rashid wa CUF amefukuzwa chamani kwa kuonyesha nia ya kutaka kugombea ukatibu Mkuu, kumbuka pia Mtungilei alifukuzwa TLP alipoutaka uenyekiti na pia ukumbuke katika CCM pia hakuna anayeweza kuthubutu kuchukua forma ya kugombea uenyekiti Taifa kumpinga mwenyekiti aliyepo!! ndani ya CDM Zitto alipewa nafasi na kamwe hakufukuzwa Chamani, kwa mantiki hiyo CDM haiko vile unavyotaka kutuaminisha!
 
Sihitaji kuheshimiwa na mtu kama wewe,kwani sijazoea unafiki.Unafiki na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa ndiyo umefikisha Taifa hapa lilipo.Siwezi kuunga mkono mtu yeyote asiye na hekima anayetaka kugawa CDM vipande vipande.Nakuambia wazi NO na haitatokea Asilani.Vyama vya hovyo hovyo vipo kibao na mtu yeyote anayependa vurugu aende huko kufanya vurugu zake.
Narudia ni bora tutawaliwe na CCM hata miaka mia moja ijayo kuliko kuruhusu wavurugaji kwa ukaidi na ubinafsi wao kutaka kuua chama.Wapo mashujaa waliokufa huku wakipigania chama na damu zao zinalilia haki Ardhini.
Kwa akili yako unadhani mtu yeyote akipingana kimawazo na watu wanaotaka kuvuruga chama basi ni lazima wawe wafuasi wa fulani au mapandikizi? Hiyo ni akili mgando iliyojengwa katika fikra za kimaskini na za ki-CCM.Kama wewe ni kundi la fulani basi usidhani watu wote ni wa hovyo hovyo au ni cheap kiasi hicho.

Mkuu Molemo
Naona umejibu kwa jazba na hamaki kubwa; hebu tuelemishe Zitto amevunja kipengele gani cha katiba ya Chadema? Nimekuuliza swali hili mapema sana jibu huna; nipe sababu nizijue kama ni kweli Zitto si mwadilifu hata mimi nitakusaidia kumpiga madongo kwasababu sipo tayari kuona Tanzania inaongozwa na mtu mwenye mapungufu ya kisiasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Molemojibu la maswali yangu ni walewale? Mimi ID yangu ni moja tu; nimekuuliza maswali madogo ya msingi huna majibu; ni kipengele gani cha katiba ya Chadema mh. Zitto amekikiuka kwa kutangaza malengo na azma zake za kisiasa?ChamaGongo la mboto DSM
Chama, naona kazi mliyopewa haitafamikiwa kamwe, kuiangusha Cdm ni ngumu sana, na ni kwa sababu wasomi ni wengi sana ndani y CDM, sasa tizama baada ya kuishauri serikali yenu namna nzuri ya kutekeleza sera zenu, kutwa..
 
Mbona wanaccm wengi wametangaza nia vijana kwa kwa wazee japo wanatupiana madongo kweli2 sembuse cdm. Ninyi cdm siyo malaika mbele ya mwenyenzi Mungu. Hii ndiyo mikiki na changamoto za politics. Watu wa aina ya ZZK wako hata ndani ya vyama vikubwa kama democratic na rep vyote vya usa. Cdm msipoteze muda wenu kumjadili zito agenda yenu ni moja tu m4c.
 
Chama, naona kazi mliyopewa haitafamikiwa kamwe, kuiangusha Cdm ni ngumu sana, na ni kwa sababu wasomi ni wengi sana ndani y CDM, sasa tizama baada ya kuishauri serikali yenu namna nzuri ya kutekeleza sera zenu, kutwa..

Nakubali sana Chadema kuna wasomi wengi na wewe ni mmoja wapo wa hao wasomi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Chama, naona kazi mliyopewa haitafamikiwa kamwe, kuiangusha Cdm ni ngumu sana, na ni kwa sababu wasomi ni wengi sana ndani y CDM, sasa tizama baada ya kuishauri serikali yenu namna nzuri ya kutekeleza sera zenu, kutwa..

Mkuu IsayaMwita nitakuja Kigamboni tuonane.
 
A stupid thinking capacity! Narrow minded...!

Mkuu Molemo
Punguza wahka muelemishe mhusika kama wewe si kijana wa Mbowe huna sababu hata moja kulipuka!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Molemo
Punguza wahka muelemishe mhusika kama wewe si kijana wa Mbowe huna sababu hata moja kulipuka!

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu Chama tuonane lini? Nataka tupange tuonane weekend ijayo.
 
Back
Top Bottom