Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Mwingine mara aseme amewekewa maneno mwingine oooh naunga mkono mwenyekiti basi mradi wameongea hawa watu bw!!
 
mtei_kabwe.jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu Mh Zitto Kabwe(kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na Mwasisi wa Chadema Mzee Edwin Mtei .
Na Moses Mashalla, Arusha (email the author)

"Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao kwani ndiye chaguo la wengi," alisema Mtei.

MWASISI wa Chadema,Edwin Mtei amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa sasa.

Kauli hiyo ya Mtei inakuja siku kadhaa baada ya kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba Dk Slaa awanie tena urais katika uchaguzi ujao huku yeye akijiondoa katika orodha ya viongozi watakaowania nafasi hiyo kupitia Chadema.

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto anapaswa kumwachia Dk Slaa apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao kwa kuwa ndiye chaguo la wengi.

"Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao kwani ndiye chaguo la wengi," alisema Mtei.
Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.

Alisema kila mmoja ndani ya chama amekuwa na hisia na mawazo tofauti lakini msimamo wake kwa sasa ni kumtaka Dk Slaa awanie nafasi hiyo ya urais na si Zitto. "Kila mmoja na hisia na maoni yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera," alisema Mtei.

Hata hivyo, Mtei alisema Zitto ana haki ya kuonyesha demokrasia yake ndani ya chama kwa kutangaza kuwania uraisi mwaka 2015 na ndiyo maana halisi ya chama chao.
"Kuonyesha hisia si dhambi, kila mtu ana hisia zake hata yeye (Zitto) ana sababu za kuonyesha hisia zake," alisema Mtei.

Hata hivyo, alionya kuwa kila mmoja mwenye hisia za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao anapaswa kusubiri mchakato wa mchujo wa majina utakaofanyika ndani ya chama muda mwafaka ukiwadia.
 
[h=5]""" kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo."""""""""""[/h]IMEKAA LINI AU NDO UKASKAZINI
 
Habari za kupikwa zimekuwa nyingi hata kunukuu imekuwa sio kigezo tena cha kuipa uzito.
 
Sasa mtei ndo anapanga nani awe mgombea uraisi ama?? Atuachie sie wananchi na wanachama waamue...hapo mtei anaharibu chama
 
.........
Na Moses Mashalla, Arusha (email the author)

.................

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto anapaswa.................

Gazeti gani ?.

Mkuu Chanzo cha habari hii ni kipi/gazeti gani?
 
watu kama kina Mtei ingawa wako upinzani mawazo yao yamekaa kiccm sikuelewa kwanini walimshawishi Zitto asigombee uenyekiti amwachie Mbowe na pia wanamtaka asigombee Urais maswala hayo walipwasa wawaachie wanachama wafanye maamuzi kiuhalisia tunajua Dr.Slaa anakubalika kugombea urais lakini matamshi kama ya Mtei yanahochea mgogoro ambao haupo
 
Naamin dr slaa ndiyee aliyee onyeshaa njia na upinzani hali wa kwelii kwa hiyoo tumpeniiii mdaaa mwinginee wa kuongozaaa vijanaa wengiiii wamekuwaa wajuzii na kutoogopaa kwa sababu wa msimamoo wa dr
 
Huu mchezo wa kutunga posts unakera sana, kuna watu wanatamani kuwe na mgogoro chadema kwahiyo suala la zitto kuisha kimapatano kwao ni maumivu makubwa, na bado maCCM huu mwaka mtaburuzwa mpaka mchubuke kabisa
 
Source: Gazeti la Mwananchi; Mtei amtaka Zitto Kabwe asigombee urais 2015 - Siasa - mwananchi.co.tz

MWASISI wa Chadema,Edwin Mtei amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa sasa.

Kauli hiyo ya Mtei inakuja siku kadhaa baada ya kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwamba Dk Slaa awanie tena urais katika uchaguzi ujao huku yeye akijiondoa katika orodha ya viongozi watakaowania nafasi hiyo kupitia Chadema.

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto anapaswa kumwachia Dk Slaa apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao kwa kuwa ndiye chaguo la wengi.

“Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao kwani ndiye chaguo la wengi,” alisema Mtei.
Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.

Alisema kila mmoja ndani ya chama amekuwa na hisia na mawazo tofauti lakini msimamo wake kwa sasa ni kumtaka Dk Slaa awanie nafasi hiyo ya urais na si Zitto. “Kila mmoja na hisia na maoni yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera,” alisema Mtei.

Hata hivyo, Mtei alisema Zitto ana haki ya kuonyesha demokrasia yake ndani ya chama kwa kutangaza kuwania uraisi mwaka 2015 na ndiyo maana halisi ya chama chao.

“Kuonyesha hisia si dhambi, kila mtu ana hisia zake hata yeye (Zitto) ana sababu za kuonyesha hisia zake,” alisema Mtei.

Hata hivyo, alionya kuwa kila mmoja mwenye hisia za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao anapaswa kusubiri mchakato wa mchujo wa majina utakaofanyika ndani ya chama muda mwafaka ukiwadia.
 
ushemeji ukizidi mahali popote pale hatimae ni kuzaa mikikimikiki.
 
Nachokiona hapa ni kukosekana kwa UVUMILIVU, USIKIVU, na wakati mwingine nikutokujua nchi yetu inaenda wapi? Tunakipeleka wapi chama chetu. Suala la urais linaona ndo lengo la wanasiasa wetu. Kwa upande wangu nadhani tufanye kazi ya kuwatumikia watanzania badala ya kujadili urais tu.

Chadema tunapaswa kuonyesha utofauti na vyama vingine hasa CCM ambao kwao ugomvi wao ni vyeo ambavyo vimewafanya wamesahau kuwatumikia watanzania.

Pia kugombea vyeo ndivyo vimelisababishia taifa kukumbwa na RUSHWA na UFISADI. Mwisho nashauri kujadili agenda za kitaifa.
 
Back
Top Bottom