Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Asiyesikia la mkuu huvunjika guu! Mwacheni ang'ang'anie hicho anachong'ang'ania!

Ila najua, Zitto anapenda kutawala katika maongezi ya kisiasa kwa kuibua hoja zitakazofanya ajadilike na sehemu kubwa ya majadiliano ya kiasiasa, huwezi kutaka Urais huku ukiwa huna sifa ya umri!

Naamini hana nia ya kugombea Urais kama anavyodai, ila najua anataka kuhama katika jimbo la Uchaguzi kwenye kiti cha Ubunge, na nasikia anataka kuja kwenye Jimbo la Kinondoni.

Pia, kingine ninachofahamu ni kuwa Zitto anautaka Uenyekiti wa Chadema, hivyo anachokifanya sasa kuongeza umaarufu wake kwa hoja ya kuzuga ya kutaka kugombea Urais.

Tukiacha kujadili hoja yake hii ambayo siku zote amekuwa akilitumia gazeti la Mwananchi (hapo nyuma alikuwa akimtumia Ramadhani Semtawa wa Mwananchi, ila sasa kabadilisha mwandishi), tutakuwa tumefanya jambo zuri sana.

Kwa maana nyepesi ni kujaribu kuamua kumpuuza kwa hizi porojo zake za kujiongezea umaarufu kwa kulitumia gazeti la Mwananchi.
 
Matumaini yangu yote yalikuwa kuwa CHADEMA ingejipanga ili ichukue dola 2015 kiulaini kwa advantage ya CCM kuwa ktk makundi lakini huyu bwanamdogo Zitto ananinyong'onyesha sana. Hivi hajui ni wakati gani CHADEMA ilihitaji utulivu wa ndani ili nguvu zote zielekezwe kupambana na CCM-POLICY-TBC na CUF. Ila, mamangu ZITTO mshenzi na mpuuzi.
 
Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,

Mzee mtei umekataza, nini! Na wewe unafanya.nini ...??? Mbona ushatangaza nia hapo
 
mkuu, kwa taari yako cdm kuna makundi kama ilivyo ccm.

Jaribu kufungua macho yako zaidi, utajua mengi yalofichikana.

Binafsi napenda mabadiliko ktk nchi yetu, lakini nataka mabadiliko ya kweli yasiyo na hila wala ujanja ujanja.
Fungua macho mkuu na utajua mengi yalofichikana.

Inaeleweka haya ndiyo mnataka wananchi wayaamini lakini haitawezekana. It is too late now.CDM kinaaminika sana ndiyo maana pamoja na propaganda zote zinazotumika na hata mitutu ya bunduki inayotumiwa na dola dhidi ya CDM bado wananchi wako nyuma wakiwa na matumaini mengi.Naamini wengi wako tayari wavije jasho na damu lakini CDM idumu
 
Na huyo mtei anaempigia chapuo mkwewe ?
Mbowe ndo kamuomba mkwewe amsemee kwamba naye anataka kugombea jamani!
Bora zitto anaejisemea mwenyewe.anajimudu.
Mwanaume wa kweli ni jasiri

Hongera msemaji mkuu wa kundi la huyu jamaa.
 
Wewe Peri huyo mlevi tu hamsumbui mtu,mwambie urais no labda kamati za bunge
 
Wewe Peri huyo mlevi tu hamsumbui mtu,mwambie urais no labda kamati za bunge

muda utatujibu kama ni mlevi au la, kashamwambia mtei asubiri aone atakavyo chukua nchi, yetu macho.

Kingine cha kujiuliza, iko wapi busara ya mtei, kwanini anajibizana nae kwenye media?
Haoni anazidi kukibomoa chama?

Zkk anathaminika cdm pale anapotoa hoja nzito za kuibana serekali kama alivyotaka kumuondoa pinda jambo lililopelekea baraza la mawaziri kuvunjwa, anapotaka kuitumia nafasi yake kikatiba mnambania na kumuita mlevi.
 
Mkuu naamini zike ID zako 19 umezitumia ipasavyo leo kwenye hii Post...Endelea....

mkuu Malemo ingekuwa busara ukajibu hoja kwa hoja, masuala ya id sio kinacho jadiliwa hapa.

Hizo chenga unazopiga zinadhihirisha jinsi mnavyo kimbia ukweli mchungu msiopenda kuusikia.
 
Mkuu naamini zike ID zako 19 umezitumia ipasavyo leo kwenye hii Post...Endelea....

mkuu Malemo ingekuwa busara ukajibu hoja kwa hoja, masuala ya id sio kinacho jadiliwa hapa.

Hizo chenga unazopiga zinadhihirisha jinsi mnavyo kimbia ukweli mchungu msiopenda kuusikia.
 
mkuu Malemo ingekuwa busara ukajibu hoja kwa hoja, masuala ya id sio kinacho jadiliwa hapa.

Hizo chenga unazopiga zinadhihirisha jinsi mnavyo kimbia ukweli mchungu msiopenda kuusikia.

Tuntemeke bana.
Siwezi kujadiliana na mtu mwenye ID 19 na anayelipwa na Magamba.
 
Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

"Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani," alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.

"Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao," alisema Zitto.

@Zitto mkuu wangu ya nini haya lakini?.. mbona unajishusha kiasi hicho kuonyesha jeuri ya Ujana ambayo inatupa picha mbaya sana wengine kutaka ubishini ambao hauwezi kukusaidia lolote zaidi ya kuonyesha hujakomaa kisiasa. Uhuru huwezi kunyimwa isipokuwa sio kila fikra zina hekima na busara. Unatakiwa kupima maneno yako wewe utumie hekima hata kama unamwona mama yako amekaa uchi..
 
Tuntemeke bana.
Siwezi kujadiliana na mtu mwenye ID 19 na anayelipwa na Magamba.

kweli umeishiwa hoja, mi hata tuntemeke simjui unang'ang'ania kunipachika jina.

Sasa nimeamini mmefualia kwa hoja, mnaanza kupiga porojo kama magamba.

Mabadiliko ktk nchi yetu bado sana, cdm inahubiri isichokifanya.
Mpaka 2015 itazidi kujidhihirisha rangi yake halisi.
 
NAUNGANA NA WANA JF WENGINE KUWA ZZK NI MBINAFSI SANA. MARA ZOTE HUPENDA KUJIPAMBANUA KIBINAFSI-BINAFSI SANA. Swali:
1.Hivi ktk chama hakuna taratibu/vigezo vya kumpata mgombea wa urais?

2. Hivi ZZK katumia vigezo vipi kujua kuwa anafaa kuwa rais wa nchi hii ?
3. Je kwake hoja ya kukijenga chama sio ya msingi au anajua kuwa iwe chadema au kwingineko.............atagombea Urais bila ujengaji wa chama?
4. Hivi nia ya Urais hutangaziwa kwenye magazeti siku hizi au................?
5.Ikulu kuna nini mpaka kijana povu linamtoka kiasi hicho kuhusu urais?

Aidha, kama jimboni kwake katekeleza ahadi kwa asilimia 100% basi ahamishie nguvu kwenye majimbo mengine ya wana-CHADEMA. Urais ni pamoja na kuwaunganisha watu kwa ujumla wao na mali kufikia lengo kusudio. sasa ZZK kama kwenye level ya chama umekuwa mbinafsi kiasi hiki vipi ukiwa rais? ZZK Urais ni pamoja na kuwa na BUSARA NA HEKIMA AMBAVYO WEWE HIVI UNAPUNGUKIWA SANA. KUWA NA AKILI NA KUJENGA HOJA SIO PEKEE VIKUJAZE KIBURI. Usitutie aibu wasomi vijana.


Ndani ya vyama vyetu vya siasa hakuna mtu yoyote yule mwenye hati milki ya ugombea wa udiwani, ubunge au uraisi

Mimi sidhan kama kuna haja ya sisi wana CDM kutumia nguvu nyingi sana kubishana na mwanasiasa mchemfu kama m_zito, sis tuendelee na shughuli za kukijenga chama, tumwachee tuu aendelee kupiga 'mayoe' adi achoke! 2015 kura ndizo zitakazo mnyamazisha! tena tutamnyamazisha adi kwenye ubunge ili akimbilie kwa wamagamba vizuri!
 
Huyu mzee Mtei hata chama chake kinajitenga naye. Akitoa maneno yake yasiyo na busara Mnyika anakuja kutoa tamko kuwa maneno hayo yasihusishwe na chama. Sasa imefika wakati huyu mzee si wa kumsikiliza tena, maneno yake ni kama nyimbo za mayenu tu...
 
Tuntemeke bana.
Siwezi kujadiliana na mtu mwenye ID 19 na anayelipwa na Magamba.

Acha kujipa majukumu ya mods mambo ya ID hayakuhusu jibu hoja unatafuta pakukimbilia.
 
mkuu Malemo ingekuwa busara ukajibu hoja kwa hoja, masuala ya id sio kinacho jadiliwa hapa.

Hizo chenga unazopiga zinadhihirisha jinsi mnavyo kimbia ukweli mchungu msiopenda kuusikia.

Hoja zitoke wapi wakati kiboko kaishafika wanalia na mods, chezea NTUNTEMEKE.
 
Ni vita inayoletwa na wabaya wa CHADEMA, nawasihi wana CHADEMA watulie.
 
Back
Top Bottom