Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Mbona inajulikana wazi kabisa kuwa Molemo ni kijana wa mbowe.

Yeye atakuwa anajiaminisha kuwa kijana wa Mbowe. Binafsi sidhani kama Mbowe atakuwa 'ameandaa vijana wake'... Kama Mbowe anataka kujivunia vijana wake, basi namba moja atakuwa Zitto...
 
Mbowe anapiganiwa na Mtei
Slaa anapiganiwa na Josephine
Zitto anapiganiwa na wananchi
 
zito ni jembe la ukweli, ndomana cdm wanamgwaya.
Si umesikia alivyomjibu mte, kamwambia watch me...

Hahahaa.....
Hapo mbowe na slaa viroho vinawadunda.

Hakuna ushindani wowote kati ya Zitto upand mmoja na CDM upande mwingine.
 
Nimekuwa nikimheshimu sana Molemo humu Jf na nikiamini ni mpiganaji mahiri wa CDM. Hata hivyo, the way alivyojenga chuki binafsi dhidi ya Zitto na mbaya zaidi anaziexpress hadharani, kwa sasa namuona kama pandikizi hatari sana kwa chama. Molemo kwa makusudi kabisa amepotosha hii habari, kwa mfano anamlisha Mtei maneno kama vile kusema Zitto amekuwa mkaidi na hasikii. Ukiisoma stori, maneno hayo hayajatamkwa na Mtei. Kwenye kipengele cha Zitto kutaka katiba isimzuie mtu kugombea kwa umri, mzee Mtei ametumia neno "itaonekana" mbinafsi. Molemo akabadilisha na kusema "atakuwa" mbinafsi na mwenye uroho wa madaraka!!!
Naombeni nyie vijana wa CDM hapo makao makuu mtuambie kama chama chetu kina makundi, na nyie mnafuata kundi gani. Sisi tunatambua CDM hakuna makundi, tunawakubali viongozi wetu sawa, na binafsi naamini kati za Slaa, Mbowe na Zitto, yeyote akiwa raisi, nchi itakuwa imepata kiongozi bora. Acheni kutufarakanisha na Zitto...

mkuu, kwa taari yako cdm kuna makundi kama ilivyo ccm.

Jaribu kufungua macho yako zaidi, utajua mengi yalofichikana.

Binafsi napenda mabadiliko ktk nchi yetu, lakini nataka mabadiliko ya kweli yasiyo na hila wala ujanja ujanja.
Fungua macho mkuu na utajua mengi yalofichikana.
 
we ulitaka aandike nini ujue kuwa ni points?
Hamjaweza kujibu hoja hata moja mnabaki kubwabwaja.
Acheni demokrasia itawale, msitake kumkandamiza zkk, yeye kama mwanachama wa cdm ana haki kikatiba ya kugombea.
Mnajua anakubalika, ana uwezo na anahatarisha nafasi ya dr mnaempenda.
Sasa subirini, bado ngoma nyingine inakuja kati ya mbowe na dr slaa, hapo ndo mtaelewa nia na madhumuni ya kuanzishwa cdm.

Kama mtei hakua tayari kuona zkk anapambana na mbowe kwenye uenyekiti. wakamtaka ajitoe kabla ya kupigiwa kura, kwanini hawakuacha demokrasia ifanye kazi yake?

Tafsiri yake ni kuwa watatumia mbinu chafu zaidi ya hizo pindi mbowe na dr slaa watakapo chukua fomu kuomba ridhaa ya chama ili wagombee.

Mtei yuko tayari kumlinda mkwe wake kwa gharama yexote ile.

Wewe ulitaka pandikizi ndo liwe mwenyekilti wa chama makini kama CDM. CCM wametumia kila njia lakini wamefail. Na hataweza kuangusha japo hata nukta ya CDM.
 
zito ni jembe la ukweli, ndomana cdm wanamgwaya.
Si umesikia alivyomjibu mte, kamwambia watch me...

Hahahaa.....
Hapo mbowe na slaa viroho vinawadunda.

Zitto, katisha vibaya kina Molemo, povu linawatoka ovyo.
 
Last edited by a moderator:
Wazee walisema, mtu mwenye tamaa na sura mbili huwa anajulikana mchana hata akifanya mambo hayo usiku akijificha-jificha mbele ya watu.

Hakuna haja ya kupoteza muda. CHADEMA wanatakiwa kulijadili hili suala na kumuadhibisha mara moja mtu anayeongelea nafasi ya Urais wakati haiko wazi sasa. Hili ni jaribio la uhaini.

Mimi sina imani tena na huyu kijana na kwa kweli hafai si kwamba hana uwezo wa kuongoza bali anauwezo pia wa kuwa mbinafsi, mwenye tamaa na mchonganishi hivyo ataliingiza Taifa katika janga endapo ataendelea kupewa nafasi yoyote hata ya ubunge. Haiwezekani mtu akawania nafasi ya kuwaongoza nchi kwa fujo namna hii hata kabla kipenga hakijapulizwa! Wafukuza upepo wanaowahi kuondoka kwenye mstari kabla ya kipenga huwa wanapewa yellow card na wakirudia mara ya pili ni red bila mjadala.

Matukio ya Zitto yametosha sasa (mnakumbuka alivyowazuga wenzake Kigoma jukwaani hadi eti kutoa chozi la mamba) ili aonekane anapendwa sana Tanzania zima kuwa Rais). Sasa hata kadi zimeisha mifukoni mwa refa apewe black card iliyobaki na sindikizwe na askari kuelekea anakotaka kwenda. Trick ya kumsubilia aendelee kuongea haya mambo na kuwaona wanaomshauri kuwa hawataki demokrasia itaweza kuki- cost CHADEMA.

Mbona CHADEMA ina watu makini sana? Ukiachilia mbali Dr. Slaa, kwa vigezo vyote Zitto anapigwa chini pia kwa mbali na Mbowe, Mnyika, Lissu hata Mdee maana hao wana sifa za uongozi na hawana sifa ya tamaa na kubadilika badilika vitu vinavyomtafuna huyu kijana.
 
Nimekuwa nikimheshimu sana Molemo humu Jf na nikiamini ni mpiganaji mahiri wa CDM. Hata hivyo, the way alivyojenga chuki binafsi dhidi ya Zitto na mbaya zaidi anaziexpress hadharani, kwa sasa namuona kama pandikizi hatari sana kwa chama. Molemo kwa makusudi kabisa amepotosha hii habari, kwa mfano anamlisha Mtei maneno kama vile kusema Zitto amekuwa mkaidi na hasikii. Ukiisoma stori, maneno hayo hayajatamkwa na Mtei. Kwenye kipengele cha Zitto kutaka katiba isimzuie mtu kugombea kwa umri, mzee Mtei ametumia neno "itaonekana" mbinafsi. Molemo akabadilisha na kusema "atakuwa" mbinafsi na mwenye uroho wa madaraka!!!
Naombeni nyie vijana wa CDM hapo makao makuu mtuambie kama chama chetu kina makundi, na nyie mnafuata kundi gani. Sisi tunatambua CDM hakuna makundi, tunawakubali viongozi wetu sawa, na binafsi naamini kati za Slaa, Mbowe na Zitto, yeyote akiwa raisi, nchi itakuwa imepata kiongozi bora. Acheni kutufarakanisha na Zitto...

Mkuu nimekubaliana na hayo yote ila moja tu kwamba CDM hakuna makundi. Katika vyama vya siasa makundi ndio uhai wenyewe wa chama. Bila kusuguana hakuna kani! Mkuu CDM kuna makundi.
 
Wazee walisema, mtu mwenye tamaa na sura mbili huwa anajulikana mchana hata akifanya mambo hayo usiku akijificha-jificha mbele ya watu.

Hakuna haja ya kupoteza muda. CHADEMA wanatakiwa kulijadili hili suala na kumuadhibisha mara moja mtu anayeongelea nafasi ya Urais wakati haiko wazi sasa. Hili ni jaribio la uhaini.

Mimi sina imani tena na huyu kijana na kwa kweli hafai si kwamba hana uwezo wa kuongoza bali anauwezo pia wa kuwa mbinafsi, mwenye tamaa na mchonganishi hivyo ataliingiza Taifa katika janga endapo ataendelea kupewa nafasi yoyote hata ya ubunge. Haiwezekani mtu akawania nafasi ya kuwaongoza nchi kwa fujo namna hii hata kabla kipenga hakijapulizwa! Wafukuza upepo wanaowahi kuondoka kwenye mstari kabla ya kipenga huwa wanapewa yellow card na wakirudia mara ya pili ni red bila mjadala.

Matukio ya Zitto yametosha sasa (mnakumbuka alivyowazuga wenzake Kigoma jukwaani hadi eti kutoa chozi la mamba) ili aonekane anapendwa sana Tanzania zima kuwa Rais). Sasa hata kadi zimeisha mifukoni mwa refa apewe black card iliyobaki na sindikizwe na askari kuelekea anakotaka kwenda. Trick ya kumsubilia aendelee kuongea haya mambo na kuwaona wanaomshauri kuwa hawataki demokrasia itaweza kuki- cost CHADEMA.

Mbona CHADEMA ina watu makini sana? Ukiachilia mbali Dr. Slaa, kwa vigezo vyote Zitto anapigwa chini pia kwa mbali na Mbowe, Mnyika, Lissu hata Mdee maana hao wana sifa za uongozi na hawana sifa ya tamaa na kubadilika badilika vitu vinavyomtafuna huyu kijana.

Mkuu Zitto anakuwa mhani kwa kusema kwamba anautataka urais kupitia CDM?

Kama hana vigezo si mmpuuze tu?
 
Kwa maoni yangu nadhan zito anakosea na anapoelekea atayumbisha chama coz inaonekana ameshalewa sifa za watanzania wanao ongea bila kupiga kura. Ajipange
 
Tunaposoma habari hizi tuwe wapana wa kusoma mwenendo wa siasa na usanii wa CCM kwa vyama vya upinzania nchini. Nilivyoandika mada kadhaa kuhusu Zitto hivi karibuni na wengi kutaka kuninyofoa macho sababu ya kutonielewa tu.

Walianza na kumtumia mzee wa Ngonjera, aka mzee wa mipasho Shibuda, wakaona watu tumedharau na kana kwamba hatuoni kama kuna kitu kinaendelea.

Kwa mtindo ule ule wamemleta Zitto kabwe kwa staili ya kipekee kwa kutangaza kabisa kutogombea Kigoma kwa malengo ya kujiandaa kugombea urais. Hili linaonekana kuwatikisa wapenzi wengi wa Chadema ingawa viongozi wa juu kwa nafasi mbalimbali wametoa kauli zinazoashiria kwamba kulishulughulikia hilo si wakati wake kama ifuatavyo:

  • Mbowe: Hatufugi kambi ya waroho wa madaraka ila waendesha vuguvugu la mabadiliko kwa sasa.
  • Edwin Mte: Zitto si wakati wake, kwa sasa ni kukijenga Chama na wakati ukiwadia atakuwa na nafasi.
  • Jibu la Zitto ni kukazia kauli yake ambayo inaelekea wazi kujenga makundi ndani ya Chama
​
Zitto baada ya kusafiri kwenda Ethiopia kwenye msiba wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo akiongozana na Rais Kikwete amerudi na nguvu mpya ya kutangaza kujiondoa kutogombea Ubunge Kigoma na kujianda kwa ajili ya Kugombea Urais. Njia mbili zilimpasua filsi msamba (samahani kwa niliyotamka), na pia mtu huwezi kuwatumikia mabwana wawili, na mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

Chunga kauli yangu hii.

  • Ignore Zitto Kabwe kama ilivyofanyika kwa Shibuda ndio ushindi wenye kutumia akili, kuendelea kumjadili na akiona mizengwe inampeleka kusikotegemewa ataanza kuchafua hali ya hewa. Tumejifunza mengi toka kwa akina Kafulila, Kabour Walid na wengineo.
  • Uongozi wa Juu Chadema endeleeni na mwendo mlio nao bila kuhangaikia hoja ya mmoja binafsi kuhangaikia urais wakati muda haujafika. Atakapoona anadharaulika na watu kutotia maanani anayohangaikia hali itajirudia kama ya Shibuda.
  • Don't trust persron, trust chama cha siasa.

Wanasiasa si wa kuwaamini, wengi ni ndumila kuwili, muhimu angalia nyendo za mtu na mwache alivyo, kwani wakati ni ukuta, wapenda mabadiliko wakilitilia maanani wanaowatumia watu hao serikali na CCM wanafurahia kazi yao kufanikiwa.
 
Mkuu nimekubaliana na hayo yote ila moja tu kwamba CDM hakuna makundi. Katika vyama vya siasa makundi ndio uhai wenyewe wa chama. Bila kusuguana hakuna kani! Mkuu CDM kuna makundi.
Hili neno "CHADEMA hakuna makundi" sijui ni kwanini linang'ang'aniwa sana na wajenga hoja wanaoamini kuwa ni wao pekee wanaitetea CHADEMA. Au wao hudhani makundi maana yake ni "wavunja chama"? Makundi kwenye vyama ni lazima ni kama vile maji kwa samaki!!
 
Hakuna haja ya kupoteza muda. CHADEMA wanatakiwa kulijadili hili suala na kumuadhibisha mara moja mtu anayeongelea nafasi ya Urais wakati haiko wazi sasa. Hili ni jaribio la uhaini.

wenye tamaa na mchonganishi hivyo ataliingiza Taifa katika janga endapo ataendelea kupewa nafasi yoyote hata ya ubunge. Haiwezekani mtu akawania nafasi ya kuwaongoza nchi kwa fujo namna hii hata kabla kipenga hakijapulizwa!

Mbona CHADEMA ina watu makini sana? Ukiachilia mbali Dr. Slaa, kwa vigezo vyote Zitto anapigwa chini pia kwa mbali na Mbowe, Mnyika, Lissu hata Mdee maana hao wana sifa za uongozi na hawana sifa ya tamaa na kubadilika badilika vitu vinavyomtafuna huyu kijana.

kwa taarifa yako cdm hawana ubavu wa kumtimua zkk,
wanajua kuwa ni jembe na anakubalika, ndomana wanagwaya.

Hao kina mdee, mnyika na lisu bado wachanga sana kwenye sasa na hawalingani hata kidogo na zkk.

Tukirudi kwa mbowe, uwezo wake ni mdogo sana,
ndomana hata bungeni anapwaya kama kiongozi wa kambi ya upinzani.
Wanaotoa hoja nzito huwa ni zkk na lissu kidogo.

Cdm wanajua uwezo mkubwa wa zkk ndomana wanatumia kilambinu kunyamazisha.
 
Moses Mashalla, Arusha na Boniface Meena, Dar | Mwananchi | Oktoba 06, 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amekitikisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa hatua yake ya kutangaza kuwania urais 2015, baada ya mwasisi wake, Edwin Mtei kumuonya kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

Kauli hiyo ya Mtei imekuja siku chache baada ya mbunge huyo kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 umekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Alisisitiza kwamba siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini akasema kuwa ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza.

“Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.

Huku akimwagia sifa mbalimbali Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, Mtei alisema kwa upande mwingine, Katiba ya Tanzania kwa sasa, inamnyima Zitto sifa za kuwania urais mwaka 2015 kwa kuwa hadi kufikia mwaka huo atakuwa amefikisha miaka 38, huku Katiba ikielekeza kuwa mgombea urais anatakiwa awe na miaka isiyopungua 40.

Alipoulizwa ya kwamba endapo uchaguzi mkuu ujao utafanyika huku Watanzania wakiwa na Katiba Mpya iliyopunguza umri wa kuwania urais, Mtei alisema endapo mbunge huyo atapambana kuhakikisha umri huo unapunguzwa, basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia.

“Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.”

Zitto apinga
Akizungumzia kauli hiyo ya Mtei, Zitto alisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

“Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani,” alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.

“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”

Septemba 26, mwaka huu Zitto alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais mwaka 2015, alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200. Miongoni mwa maswali hayo lilihusu tetesi kwamba anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.

Katika majibu yake Zitto alisema: “Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.

“Nimefanya kazi kubwa katika ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka 10.

“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola.

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndiyo msimamo wangu. Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.

”
Alipoulizwa kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa Katiba alijibu: “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndiyo maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika Katiba Mpya.”

My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Mimi kama mwana chadema, naona kama vyombo vya habari hasa gazeti la Mwananchi linaleta uchochezi na wakati mwingine kwa vile liliishajijengea sifa ya kuaminiwa, sasa linatumia nafasi hiyo kupotosha. Kuna sehemu nimeweka wino mwekundu katika maandishi ya gazeti ... yeye anachosema ni kuonesha nia ni jukumu la chama kumpitisha au la.

Katika gazeti la mwananchi la Ijumaa, mwandishi ameandika uongo juu ya mjane wa Mwangosi kwa kusema kuwa rambirambi zake hazipati na hana namna ya kuwasiliana na Dr. Slaa... Kumbe mwandishi alimwuliza kama ana namba ya dr slaa, akasema hana... basi mwandishi akaenda kuandika maneno yao ya uongo. Sijajua "interest " ya gazeti katika michakato hii. Nadhani kuonesha nia wataonesha wengi, lakini atakayepewa ridhaa ni mmoja.

Quality does not get old
 
Mkuu pole sana naona wewe ni new comer hapa JF 2011 inawezekana huwajui hawa jamaa
siku zote ni supporter was CCM leo ndo wamekuwa supporter wa Zitto?

Ukijibu hoja zao ni kama umeingia choo cha kike

Copy to Ritz, Pasco, chama, Ecoli, Kata nyodo, OTIS

Mkuu usikwepe hoja ya msingi; mimi ni CCM na pia mtu ninayeamini sana demokrasia; ninachohoji ni kitu gani hasa kinachowafanya muwe hamlali usiku na mchana kumpiga madongo Zitto? wote humu JF hamna jibu la msingi zaidi ya kutumiwa kisiasa.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wazee walisema, mtu mwenye tamaa na sura mbili huwa anajulikana mchana hata akifanya mambo hayo usiku akijificha-jificha mbele ya watu.

Hakuna haja ya kupoteza muda. CHADEMA wanatakiwa kulijadili hili suala na kumuadhibisha mara moja mtu anayeongelea nafasi ya Urais wakati haiko wazi sasa. Hili ni jaribio la uhaini.

Mimi sina imani tena na huyu kijana na kwa kweli hafai si kwamba hana uwezo wa kuongoza bali anauwezo pia wa kuwa mbinafsi, mwenye tamaa na mchonganishi hivyo ataliingiza Taifa katika janga endapo ataendelea kupewa nafasi yoyote hata ya ubunge. Haiwezekani mtu akawania nafasi ya kuwaongoza nchi kwa fujo namna hii hata kabla kipenga hakijapulizwa! Wafukuza upepo wanaowahi kuondoka kwenye mstari kabla ya kipenga huwa wanapewa yellow card na wakirudia mara ya pili ni red bila mjadala.

Matukio ya Zitto yametosha sasa (mnakumbuka alivyowazuga wenzake Kigoma jukwaani hadi eti kutoa chozi la mamba) ili aonekane anapendwa sana Tanzania zima kuwa Rais). Sasa hata kadi zimeisha mifukoni mwa refa apewe black card iliyobaki na sindikizwe na askari kuelekea anakotaka kwenda. Trick ya kumsubilia aendelee kuongea haya mambo na kuwaona wanaomshauri kuwa hawataki demokrasia itaweza kuki- cost CHADEMA.

Mbona CHADEMA ina watu makini sana? Ukiachilia mbali Dr. Slaa, kwa vigezo vyote Zitto anapigwa chini pia kwa mbali na Mbowe, Mnyika, Lissu hata Mdee maana hao wana sifa za uongozi na hawana sifa ya tamaa na kubadilika badilika vitu vinavyomtafuna huyu kijana.

Correct 100%
 
Back
Top Bottom