Mkuu Molemo, alichofanya ZZK sio kutangaza kugombea urais kupitia Chadema, bali kutangaza nia ya kuiomba Chadema kumpitisha kama mgombea wa Chadema 2015!. Naomba sana utofautishe kati ya
"kutangaza nia" na "kutangaza kugombea"!.
ZZK alipotangaza nia, mimi nilimuunga mkono na kutangaza nia ni jambo jema na jambo la kheri na nikatoa wito kabisa kuwa kila mwenye nia na aitangaze!, hivi kuna ubaya gani?. Hebu kanisome hapa
Urais 2015 tusimlaumu Zitto; Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa ...
Lakini ZZK alipojitangaza rasmi kuwa hagombei tena ubunge na badala yake "atagombea urais kupitia Chadema" nilimpinga!. Nilimwambia wazi, that was wrong!, hakupaswa kujitangazwa, bali alipaswa tuu kuonyesha vitendo vya ki presidential candidate ndani ya chama, ili wenzake ndio wamuone na kumuomba agombee na sio kujipigia debe na hapa nilimtahadharisha
Urais wa ZZK 2015: Ngoma Ikivuma Sana...!. Wenye uwezo wa kumtangaza mgombea ni Chama na sio mwan achama individual!.
Ila lazima mkubali, mkatae, ndani ya Chadema kuna double standards za hali ya juu!, kuna baadhi ya mambo yakifanywa na kina fulani ni halali, ila wakifanya kina fulani inageuka ningwa!.
Tatizo ni kuwa ndani ya mioyo ya wana Chadema wengi, wanaye mgombea wao mioyoni mwao, sio tuu kuwa mgombea huyo anakubalika sana kwao, bali anaabudiwa!. Kitendo cha ZZK kujitokeza anaonekana kama kumkufuru huyo mungu mtu anaye abudiwa!. Na kwa wasio jua, mimi naujua msimamo wa huyo mgombea wenu kipenzi kuhusu kugombea au kutogombea urais na usome hapa
Msimamo wa Dr. Slaa Kwenye Urais 2015 ...
Unashauri kamati kuu itoe miongozo, hivi kumbe Chadema haina demokrasia ya kila mwanachama yoyote kugombea nafasi yoyote ni mpaka kamati kuu itoe miongozo!.
Tena kwa vile ZZK ni rafiki yangu, na kabla hata ya huo urais kuna uchaguzi wa viongozi wa Chadema, nitamshauri agombee tena Uenyekiti na this time hakuna kujitoa mpaka kieleweke!.
Hivi nyinyi wapenzi wa Chadema, bado hamjajua ZZK ndio mtaji wenu pekee wa ushindi 2015?. Jee mnajua CCM itamsimamisha Membe?, sasa kwa vile huyo mgombea kipenzi wetu na Membe hawana tofauti katiuka zile kampeni za "kivile", na hamjajua kwa mujibu wa katiba mpya, ili chama kishinde urais wa JMT, lazima kipate angalau theluthi moja ya kura za Visiwani!, hivi huyo mgombea wenu kipenzi, kwa siasa zetu "zile", hizo theluthi ya kura kutoka visiwani zinatokea wapi?!.
ZZK anakubalika sana kutokana na kuendesha "strategic politics" kwa urafiki wake na January Makamba, atazivuna kura zote za vijana wa CCM!, kwa urafiki wake na Jussa, atazivuna kura zote za CUF kule visiwani. Kwa usomi wake, atazivuna kura zote za vijana/wasomi na wataka badiliko ya kweli with clear goals na right strategies!.
Nashauri, baada ya Mzee Mtei kukikabidhi chama kwenye "safe hands" za mkwewe, his advisory role yake ibaki limited kwa insiders tuu wa chama na sio ku express his public opinion publically as if chama bado ni chake!. Heshima yake kama muasisi ipo pale pale, lakini kwa sasa chama sio chake tena, sasa chama ni cha wanachama!, tena Mwenyekiti Mbowe anatakiwa kujipambanua kabisa kwa hili kuwa "amekata kabisa zile mothers apron strings" ili isje onekana kina Mzee Edwin Mtei ndio bado wanaendesha chama by proxy kupitia kwa wakwe zao!.
Ili chadema kuonysha ina "practice what it preach" lazima iache democracy i prevail!.
Go ZZK Go!.
Pasco.