Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Urais 2015: Mtei amshukia Zitto

Utasemaje Zitto anasababisha mpasuko ndani ya chama wakati wewe mwenyewe unaenda kumpiga ma bombardment Zitto kwenye media? Huko sio kupasua chama?
 
Zitto ni mbinafsi ana umimi hata ndani ya chadema.zitto haipiganii cdm anapigania maslah yake.jiulizeni ni kwnn katika ujenzi wa kuimarisha chama maeneo ya vijijini haonekani mkoa wa kigoma wenyewe ameshindwa kuitangaza chadema kwa hyo huyu ni tatizo ndan ya chadema tunamtaka zitto wa miaka mitano iliyopita bado ana nafasi ya kujirekebisha kurejesha heshima yake ya kisiasa kama mpinzani kimfumo,kimaono na kiitikadi tumshauri kijana mwenzetu kwa maslah ya chama na mustakabali mzima wa taifa hususani kipindi hiki chakuelekea 2015 katika ujenzi na matumaini mbadala kwa wananchi
 
Utasemaje Zitto anasababisha mpasuko ndani ya chama wakati wewe mwenyewe unaenda kumpiga ma bombardment Zitto kwenye media? Huko sio kupasua chama?
Mkuu unachanganya hoja yko n nn hapa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, aminia hao ni redio imani na wasanii wachache wa dar tu! wengi wamesha shitukia, manake wamesha ona wanaotesa/kuteseka ni waislamu wakristo na wapagani! na ufisadi hauchagui dini taifa wala rangi na lugha! Tembelea wafanyikazi na wakulima, pia mikoani uone elimu ya uraia ilivyo jikita!
Kama akili imeanza kuwaingia sawa,tuwe pamoja kuikomboa hii nchi,Ukristo na Uislamu ni kama Crosscutting ideas,hakuna familia/ukoo wa kitanzania ambao hakuna Mkristo au Muislam hasa kwa upande wa Tanzania bara,so hatupaswi kuangaliana kwa kigezo cha Udini,tuangalie nani atatusimamia kwenye mambo yetu,hii nchi ni ya kwetu sote,so lazima tuwe makini hasa 2015!
 
Sio Zitto anayeweweseka na picha za Kikwete ni Dr. Slaa ndio sababu yupo tayari kuwaona akina Mwangosi wakifa kwa tamaa zake uraisi.

Chama
Gongo la mboto DSM
Wewe sio bure una kasoro kichwani kwani aliyewauwa kina Mwangosi sio nyinyi maghama imekuwa ni Dr Slaa??? Wewe una chuki binafsi na Dr Slaa labda unaona tonge lako linaondoka, na ni kweli hatuachi unaondoka hata uje na sera za kina ZITO Kabwe kwa heri !!!!

 
Chadema bana; hacheni kutumbukia kwenye mitego ya CCM! Ina maana hamuamini katika utaratibu wa kumpata mgombea URAIS ulioanishwa na katiba ya chama?

Sioni sababu yoyote ya kumwandama Zitto, kwa kuwa mtu yeyote anaweza kukurupuka usingizini na kutamka anayotamka Zitto. Muhimu ni kuwa muda ukifika vikao vya chama vitaamua nani anafaa... hata kama watajitokeza wanachama mia wote wanataka kugombea nafasi hiyo. Hacheni wanachama wafunguke kuhusu ndoto zao, msifanye makosa wanayofanya CCM, kwa maana taratibu ziko wazi, na
Zitto anafahamu vizuri sana.
 
Ama kweli sikio la kufa.......................na asiye sikia la mkuu.................Poleni sana CDM yote hayo mliyataka wenyewe kila data muhimu mnampatia yeye kuiwasilisha mezani(bungeni) sasa anawapanda vinywani mwenu kazi kwelix2.In fact ZZK anawatania tu uraisi ni wa............
 
kwani kutangaza nia ya kugombea uraisi kuna tatizo gani.
demokrasia ya kweli nampa fursa kila mtu mwenye akili timamu na mwenye vigezo stahili kugombea uraisi.
sasa inakuaje zitto kutangaza nia kuna wanyima watu usingizi
 
zitto simkubali,ila mzee Mtei kufanya chama kama chake huwa sipendi sana..haswa anapoonesha hadharani anapambana na Zitto kwa gharama yoyote ile.

Zitto naye anaukamia urais wa 2015 utafikiri ana mpango wa kufa baada ya 2015. there's more uchaguzi to come jembe langu. vumilia kama mtoto wa bagamoyo. kama ipo ipo tu.

Zitto 2015
 
Mkuu chama,
Makundi kutoka Kaskazini kamwe hawawezi kuacha kupambana na Zitto, wakikaa kimya ni sawa kumuachia Nguruwe akuchomee mishikaki.

Zitto Kabwe, ana nguvu kubwa kutoka kwenye makundi ya vijana pamoja na wazee, sehemu kubwa ya Tanzania mikoa kama Dar es Saalam, Pwani, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Mwanza, Morogoro, Tanga, Bukoba, Mtwara, Lindi, Singida, Tabora, hawa wajumbe wote wa Chadema wapo upande wa Zitto Kabwe.

Sehemu za Kaskazini ni kweli Zitto hana nguvu zozote za kisiasa.

Ah wapi kijana gani anamkubali Zito mbinafsi na mroho wa madaraka mimi simpendi amekaa kiswahili na kimipasho mipoasho mbishi sijui kwa kua ni Muha kila kitu anajifanya yeye ndio anaweza mtu ameshindwa hata kuweka Mke nyumbani ndio ataweza kuongeza Nchi ZITO JIPANGE HAUKUBALIKI COMMENTS ZA FACE BOOK ZIKUDANGANYE Na njaa zako
 
Last edited by a moderator:
Mwasisi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Edwin Mtei amemuonya mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuacha kutangaza mambo ya Urais sasa kwani anasababisha mpasuko ndani ya CDM na badala yake ajikite kukijenga chama mpaka muda utakapofika ili chama kitoe utaratibu.

Mzee Mtei amesema amemshauri mara kadhaa Zitto umuhimu wa kutulia kama wenzake ndani ya chama na kukijenga chama lakini mbunge huyo amekuwa mkaidi na hasikii.

Pia Mzee Mtei amesema endapo mbunge huyo ataendeleza harakati zake za kutaka umri wa Urais ushuke hadi miaka chini ya 40 ili tu yeye apate nafasi ya kugombea basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia na mwenye uroho mkubwa wa madaraka.

Akijibu madai hayo ya Mzee Mtei, Zitto Kabwe amemuonya Muasisi huyo wa chama na amewataka wazee ndani ya CHADEMA kuheshimu Demokrasia na kusema anaamini ni yeye atakayeweza kuishinda CCM mwaka 2015 na anataka Mzee Mtei akiwa bado hajafa amshuhudie jinsi atakavyobadili nchi akiwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Source: Mwananchi Jumamosi.

Full Story

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Urais 2015: Mtei amshukia Zitto
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Saturday, 06 October 2012 07:38 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Moses Mashalla, Arusha na Boniface Meena, Dar

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amekitikisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa hatua yake ya kutangaza kuwania urais 2015, baada ya mwasisi wake, Edwin Mtei kumuonya kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama.


Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.
Kauli hiyo ya Mtei imekuja siku chache baada ya mbunge huyo kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.


“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.
Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 umekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.


Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.


Alisisitiza kwamba siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini akasema kuwa ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza.
“Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.


Huku akimwagia sifa mbalimbali Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, Mtei alisema kwa upande mwingine, Katiba ya Tanzania kwa sasa, inamnyima Zitto sifa za kuwania urais mwaka 2015 kwa kuwa hadi kufikia mwaka huo atakuwa amefikisha miaka 38, huku Katiba ikielekeza kuwa mgombea urais anatakiwa awe na miaka isiyopungua 40.


Alipoulizwa ya kwamba endapo uchaguzi mkuu ujao utafanyika huku Watanzania wakiwa na Katiba Mpya iliyopunguza umri wa kuwania urais, Mtei alisema endapo mbunge huyo atapambana kuhakikisha umri huo unapunguzwa, basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia.
“Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.”


Zitto apinga

Akizungumzia kauli hiyo ya Mtei, Zitto alisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.


“Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani,” alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.


“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.


Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”
Septemba 26, mwaka huu Zitto alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais mwaka 2015, alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200. Miongoni mwa maswali hayo lilihusu tetesi kwamba anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.
Katika majibu yake Zitto alisema: “Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.


“Nimefanya kazi kubwa katika ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka 10.
“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha.Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola. 



“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndiyo msimamo wangu. Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.


”
Alipoulizwa kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa Katiba alijibu: “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndiyo maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika Katiba Mpya.”


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


My Take:
Nadhani umefika wakati sasa wa Kamati Kuu kutoa mwongozo kuhusu suala hili. Hili suala la kila mtu kujitangaza kugombea Urais sasa linataka kupoteza mwelekeo wa harakati za CHADEMA kujijenga.

Imefika wakati wa M/kiti na Katibu mkuu wa chama kuongoza Kamati kuu kutoa hitimisho la jambo hili. Simaanishi kufukuza watu Hapana! Lakini itangaze muda muafaka wa wanachama kutangaza nia, kwani binafsi naamini DEMOKRASIA BILA NIDHAMU NI FUJO.

Afukuzwe tu anaalibu Chama,zito bwana eti awe Raisi Wema Sepetu 1st lady maajabu ya dunia
 
Zitto Acha tamaa kijana!! Wasikilize Wazee wanasenaje!
Ni lazima afanye jitihada atalipaje fedha za Rostam na lile Gari kubwa HUMMER alilopewa!? Nani atawalinda akina Jack ZOKA na IGHONDU!!?
HILI PANDIKIZI ZZK ling'olewe mapema hata ikibidi gharama kubwa ya kupoteza kura ikubalike!!
 
...“nimefanya kazi kubwa katika
ubunge, nimeleta mabadiliko
mengi kuanzia bungeni mpaka
jimboni. Nadhani inatosha na
hata nikiongezewa miaka
mingine sitaweza kufanya yale
yaliyonishinda katika kipindi cha
miaka 10. “Kama Mungu
ataniweka mpaka mwaka 2015,
sitagombea ubunge tena kwa
sababu kazi niliyofanya
inatosha.Natangaza rasmi kuwa
nitagombea urais kupitia chama...

...hapo ndo sikuelewi Zito unasema hata ukiongezewa miaka mingime hauwezi kuletea maendeleo zaidi katika jimbo lako,jimbo tu umefika kikomo na bado hali si nzuri sana ya kujivunia...je utaupata wapi tena uwezo wa kuiongoza mchi kama uwezo wako wa kuliongoza hilo jimbo ndo umeishia hapo?...
 
Kila jambo lazima lifanyike kwa utaratibu Ritz ,kwani hata huko CCM nani ametangaza kugombea urais kama anavofanya Kabwe? Pia nadhani Zitto hana nia ya kugombea urais kupitia CDM ,May be anaitumia CDM kujipatia/Kujiongezea umaarufu then aje kuchepukia CCM.Kama angekua na nia ya kugombea kupitia CDM angetafuta kwanza uungwaji mkono kwenye chama chake.Kibaya zaidi ni kwamba uungwaji mkono wake kwenye chama chake unazidi kushuka.Nahisi ni mvurugaji tu.

Mkuu Gracious na Mkuu Ritz mimi nakumbuka kwamba mwaka 2010 Zitto alitangaza kuwa atagombea Urais. Aliwaambia watu wa Kigoma kuwa hatarudi tena kuwaomba kura za ubunge mwaka 2015 bali kura za Urais. Kwa hiyo hapa ni kwamba Zitto amerudia tu kauli yake aliyoitoa takribani miaka 3 iliyopita. Mbona wakati anaitoa hiyo kauli wakati huo hakuna aliyemkemea au walidhani anatania tu? Mimi najua Zitto huwa hatanii kama walidhani anatania wakanyamaza basi na wanyamaze tu kama walivyonyamaza wakati ule.
 
safi sana .Nadhani zitto kabwe yupo sasa lakini kwa nini anze kukimbilia kujitangaza!afuate taratibu za chama.pia falisafa ya chama inasema nini?sec wazee wa cdm wamsaidie kiushauri.pia zitto mimi namwomba mambo yake awe anayamaliza....... kwenye vikao vya chama kwa kumpendekeza wafanye wao.ikija kwetu iwe tu kuadvice wajenge chama vijijini waende huko nanjilinjili,,namtumbo kwa shemeji,mbarali,mwika kwa mzee wa kilacha,muleba ,,idomu ,kwa mchemba,,busanda..then waje ideas zao hizo.
 
Zitto ni mbinafsi ana umimi hata ndani ya chadema.zitto haipiganii cdm anapigania maslah yake.jiulizeni ni kwnn katika ujenzi wa kuimarisha chama maeneo ya vijijini haonekani mkoa wa kigoma wenyewe ameshindwa kuitangaza chadema kwa hyo huyu ni tatizo ndan ya chadema tunamtaka zitto wa miaka mitano iliyopita bado ana nafasi ya kujirekebisha kurejesha heshima yake ya kisiasa kama mpinzani kimfumo,kimaono na kiitikadi tumshauri kijana mwenzetu kwa maslah ya chama na mustakabali mzima wa taifa hususani kipindi hiki chakuelekea 2015 katika ujenzi na matumaini mbadala kwa wananchi

Hahaha UMIMI wa ZZK haukiti wa mtu na mkwe wake....si unaona Mtei anavyompigania Mkwe wake?....tangu kipindi cha UENYEKITI mpaka sasa hahaha CHANAGA UNITED
 
Ah wapi kijana gani anamkubali Zito mbinafsi na mroho wa madaraka mimi simpendi amekaa kiswahili na kimipasho mipoasho mbishi sijui kwa kua ni Muha kila kitu anajifanya yeye ndio anaweza mtu ameshindwa hata kuweka Mke nyumbani ndio ataweza kuongeza Nchi ZITO JIPANGE HAUKUBALIKI COMMENTS ZA FACE BOOK ZIKUDANGANYE Na njaa zako

Mkuu vp kwani BABU alishawahi kuoa kweli tangu aache UPADRI? Au anakaa na VIMADA tu?
 
Mkuu! tafakari na hili! "mmekubaliana wote kwenda vitani, (M4C) Ili mkishinda vita mgawane nyara! Vita imeanza wewe umeanza visingizio na kuchachawa! huku unatamani kuwa kiongozi wa ushindi bila kushiriki vita!

Well said Mkuu, swali ni: Kwa nini Zuberi amefikia uhamuzi wa kutangaza nia ya kuwania URAIS mwaka 2015. Kama kweli wako wamoja na hakuna ubinafsi ndani ya CHAMA inakuwaje Dogo amehamuwa kuwa REBEL ndani ya CHAMA, kumbuka Zuberi si binadamu wa kukurupukia mambo kabla hajafanya analysis ya kutosha - mimi nafikili kuna matatizo kwenye hierarchy ya uongozi wa CDM si BURE.
 
Back
Top Bottom