Zito anatetea mafisadi si uliona pale TANESCO, hebu mpe nchi hii ya Tanzania uone kitu atafanya kama hakuuza hata makaburi ya babu yako????Mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo!!!
unaweza kuwa na point hapo mkuu, japo tunahitaji kupunguza jazba katika kujadili jambo hili, kwani
hili tatizo ni kubwa. Linaweza hata kuwa na mitizamo miwili: Linaweza likawa na mtizamo wa hisaikolojia, ambao si mzuri sana kwa Mhe. Zitto Kabwe, na Upande wa Kisiasa, ambao pia si mzuri kwa upande wake. Tatizo kubwa zaidi ni kwamba upande wa pili, ambao ni wa kisiasa, una athari kwa Chama pia kwa sababu hatima yake inaelekeza Zitto Kabwe afukuzwe kutoka katika chama haraka ili chama kianze mending damage miaka mitatu kabla ya uchaguzi.
Upande wa Saikolojia ni huu: Mtu mwenye inferiority complex iliyojificha katika nafsi yake--pengine kwa kujihisi anapungukiwa kitu fulani, ambacho kinaweza kuwa kujihisi ana sura mbaya, au impotent, au mapungufu mengine ambayo mtu anakuwa akijihisi kwa siri ya moyo wake, basi watu kama hawa hutafuta kufunika inferiority complex hiyo kwa kujikweza, kujitapa ama kutaka dunia ijue wao ni masihi fulani hivi. Hadi hapa tulipofikia, mimi binafsi naona dalili za Zitto Kabwe katika jitihada za kufunika inferiority complex zaidi kuliko kitu kingine.
Lakini katika matamko ya Kijana huyu, mimi binafsi naona dalili za tabia ya mtoto ambaye kakua bila father figure, na hivyo hana hofu ya mamlaka. Mtu kama huyu anaweza kuwa bomu sana katika jumuia ambayo inahitaji utii kwa mamlaka na mshikamano. Wataalam wa Management wanakiri papal system ni mfumo mzuri sana wa mafanikio ya uongozi wa kundi lolote. Matamko yanaonesha kuwa Zitto Kabwe anakosa utii na heshima kwa watu wenye mamlaka katika jamii. Huu ni mtizamo wa kisaikolojia, na unaelekeza afukuzwe kutoka kwenye chama haraka iwezekanavyo.
Mtizamo wa kisiasa unaashiria kuwa katumwa kuleta Chaos katika chama. Nao pia unaelekeza afukuzwe katika chama haraka. Kwa hivyo Zitto Kabwe afukuzwe kutoka Chadema na chama kiendelee na mikakati yake pakiwapo utii na mshikamano miongoni mwa viongozi na wanachama. Hili litatimua vumbi, lakini upo muda wa kutosha kutuliza vumbi hilo. Zitto aondolewe Chadema.