Unataka kuolewa mdada umejipanga?

Unataka kuolewa mdada umejipanga?

Mazoea mabaya sn,ukimlamba mwanaume miguu sana na akajua unahitaji ndoa kuliko hata yeye anakimbia...mda mwingine wanawake tujitathmini tumeaminishwa kupenda status ya ndoa kuliko kuenjoy mapenzi na mwanaume husika,, hata akufanyie b.sh.it unavumilia tu ili uolewe jmn..not always akikosea na ye mchane live ama km vp walk away...atleast tishia japo...na mpende mwanaume jinsi alivyo ndoa ni matokeo ya mapenzi baina yenu..tupunguze kupenda harusi tupende ndoa na kuishi kwa amani
Si harusi tu bali harusi za kifahari halafu mwezi 1 chali wakati hata watoa michango hawajasahau pesa zao
 
Hao "wadada wa humu" wanaochamba waume zao unawajua wangapi? Au ilimradi tu nawe umechangia mada!!!
Anachambwa na huyo wakwake waliye okotana huko wakiwa wamelewa lakini waliotafutana kwa ustaraabu hawachambi wame zao
 
hahahahahahahahah! walah ndoa hizi khaaa!nilifanya bwana ile ya kupokea had koti siju nkumvua viatu,i kufungua vishikizo aliniuliza oya UMETUMWA NA CHADEMA EH???yaan niliishia kucheka hatari kwakwel kila mtu na ndoa yake
Kila shetani na mbuyu wake mie utasikia toa umbea huko unaiga mambo ya kwenye tamthilia unanipotezea muda kapike huko nile
 
Anatukana matusi mazito yani yanabebeka kwenye Lori la mchanga, haangalii mkubwa mdogo, ofisini wala wapi
Juzi kuna kina mama walikuwa wakimtukana konda yaani ukiwaona jamani na hizi dela wanazo vaa wamejichuna hao kama ndizi zile za kukaanga sasa zikaachwa na kuiva kisha zikachoma kwenye moto na maganda yake kwenye moto wa kuni waliishia kudharauliwa tu na watu, halafu watu wazima ila hao kwa wame zao lazima wakula vitasa
 
Juzi kuna kina mama walikuwa wakimtukana konda yaani ukiwaona jamani na hizi dela wanazo vaa wamejichuna hao kama ndizi zile za kukaanga sasa zikaachwa na kuiva kisha zikachoma kwenye moto na maganda yake kwenye moto wa kuni waliishia kudharauliwa tu na watu, halafu watu wazima ila hao kwa wame zao lazima wakula vitasa
Ha ha ha aah huyo dada nae ni noma, wakati ndo anafika kazini bado mgeni kuna jamaa alitaka kumuoa, kila kitu kimepangwa hadi ukumbi ushalipiwa jamaa akala kona a week before send off, nlimuonea huruma namuona innocent mmh kuja kumjua kumbe ilikua halali yake
 
Kila shetani na mbuyu wake mie utasikia toa umbea huko unaiga mambo ya kwenye tamthilia unanipotezea muda kapike huko nile
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Shunie, asante sana Kwa huu Uzi. Sote, waume kwa wake tunalo la kujifunza hapa. Kutoka kwa mtoa mada na pia kutoka Kwa wachangiaji. Inafaa sana kujifunza kwa mifano namna hii.
 
Wana masikio lakini hawasikii...wana macho lakini hawaoni...wana midomo na wanajua kuitumia vizuri
 
UNATAKA KUOLEWA? UMEJIPANGAAA?
NIMEIPENDA HII WADADA WENZANGU.

Akina Dada Wengi tunapenda Sana Kuolewa; Lakini Ni Wachache Sana Wanajua Namna Ya Kukaa MKAO WA KUOLEWA, Na Pia Namna Ya Kuchambua Kati Ya MWANAUME MUOAJI NA MWANAUME MUONJAJI!

Maua Yana Tabia Ya KUJIFUNGA, Lakini Yanajua Pia Muda Sahihi Wa KUCHANUA Na Kutoa HARUFU Inayowavutia NYUKI; Lakini Cha Ajabu Akina Dada Wa Digitali HATUJUI Haya, Tunazidiwa AKILI NA MAUA... Hii Ni Hatari Sana!

Ninapozungumzia Muda Wa UA KUCHANUA NA KUTOA HARUFU INAYOVUTIA NYUKI; Namaanisha Uwezo Wa Kutambua MAJIRA SAHIHI YA DADA KUOLEWA NA KUHAMA TOKA KWENYE KUNDI LA "MAUA YALIYOJIFUNGA" Yaani USICHANA Kuingia Kwenye Maua Yanayoingia Kwenye "UCHAVUSHAJI" Yaani Kuwa Mke, Mama Nakadhalika!

Nyuki Hawawezi Kuruka Kuja Kwenye UA LILILOJIFUNGA (Mdada Aliyekaa Mkao Wa KUTOONESHA DALILI ZA KUWA MKE), Bali Nyuki Huwa Wanaruka Kuelekea Kwenye MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU YA KUVUTIA!

Kama Dada, Kama Unaona Muda Wako Wa Kuolewa ULIOKUSUDIA Umekaribia, ANZA "KUCHANUA" Anza Kujenga Tabia Za Mke Na Si SISTA DUU Anayetafuta Mme.
Nyuki Wote Wanajua MAUA YALIYOCHANUA NA YENYE HARUFU NZURI; Vivyo Hivyo Kwa WANAUME WAOAJI, NAO WANAJUA BINTI GANI ANAFAA KUWA MKE!

Tabia Na Mfumo Wa Kuwa Mke HAUJENGWI NDANI YA NDOA; Unajengwa Ukiwa Bado Peke Yako, Unaanza KUPUNGUZA TABIA ZISIZOHITAJIKA KWENYE NDOA AMBAZO MABINTI WA KAWAIDA HUWA WANAKUWA NAZO.
Unaanza Kujenga Tabia Ya Kuwa Mama Mwenye Nyumba, Jifunze Kuwa Katika Namna Ya Mke Apaswavyo Kuwa.
Ukikaa Kwenye UHALISIA WA MKE ATAKIWAVYO KUWA; NYUKI WATAONA NA WATAKUJA, Halafu Wewe Ndiwe Utakayekuwa Na Kazi Ya KUCHAGUA YUPI KATI YAO NI MUOAJI NA YUPI KATI YAO NI MUONJAJI!

Kila Mwanadada Aliyekusudia Kuolewa Anaweza Kuolewa, Lakini Ni Lazima Uwe Na UFAHAMU WA KUTOSHA Kuhusu MKE Apaswavyokuwa Kabla Hauja-Attract Attention Ya Waoaji.

Mungu Awasaidie Akina Dada Wenye Nia Ya Dhati Ya Kuolewa Na Kuwa Na Miji Yenu[emoji120]

d06d90ffbb018061c2391b3ecac04743.jpg
Naona umeweka picha ya ua na nyuki ila aisee kuna watu wameoa maua kweli dah
 
Huwa nakubaliana sana na mawazo yako Bi Shunie nna uhakika kabisa we ni mwanmke bora sana
 
Unataka kuolewa? Umejipanga? Nimeipenda hii wadada wenzangu.

Akina dada wengi tunapenda sana kuolewa; lakini ni wachache sana wanajua namna ya kukaa mkao wa kuolewa, na pia namna ya kuchambua kati ya mwanaume muoaji na mwanaume muonjaji.

Maua yana tabia ya kujifunga, lakini yanajua pia muda sahihi wa kuchanua na kutoa harufu inayowavutia nyuki; lakini cha ajabu akina dada wa digitali hatujui haya, tunazidiwa akili na maua. Hii ni hatari sana.

Ninapozungumzia muda wa ua kuchanua na kutoa harufu inayovutia nyuki; namaanisha uwezo wa kutambua majira sahihi ya dada kuolewa na kuhama toka kwenye kundi la "Maua yaliyojifunga" yaani usichana kuingia kwenye maua yanayoingia kwenye "Uchavushaji" yaani kuwa mke, mama nakadhalika.

Nyuki hawawezi kuruka kuja kwenye ua lililojifunga (mdada aliyekaa mkao wa kutoonesha dalili za kuwa mke), bali nyuki huwa wanaruka kuelekea kwenye maua yaliyochanua na yenye harufu ya kuvutia.

Kama dada, kama unaona muda wako wa kuolewa uliokusudia umekaribia, anza "Kuchanua" anza kujenga tabia za mke na si sista duu anayetafuta mme.
Nyuki wote wanajua maua yaliyochanua na yenye harufu nzuri; vivyo hivyo kwa wanaume waoaji, nao wanajua binti gani anafaa kuwa mke.

Tabia na mfumo wa kuwa mke haujengwi ndani ya ndoa; unajengwa ukiwa bado peke yako, unaanza kupunguza tabia zisizohitajika kwenye ndoa ambazo mabinti wa kawaida huwa wanakuwa nazo.

Unaanza kujenga tabia ya kuwa mama mwenye nyumba, jifunze kuwa katika namna ya mke apaswavyo kuwa. Ukikaa kwenye uhalisia wa mke atakiwavyo kuwa; nyuki wataona na watakuja, halafu wewe ndiwe utakayekuwa na kazi ya kuchagua yupi kati yao ni muoaji na yupi kati yao ni muonjaji.

Kila mwanadada aliyekusudia kuolewa anaweza kuolewa, lakini ni lazima uwe na ufahamu wa kutosha kuhusu mke apaswavyokuwa kabla hauja-attract attention ya waoaji.

Mungu awasaidie akina dada wenye nia ya dhati ya kuolewa na kuwa na miji yenu[emoji120]
Shoga somo zuri sana na limeniingia.
ila kumbuka si kila ua lililochanua nyuki wanaweza lifata.
Kuna maua mengine yamechanua na yananukia, ila nyuki hawayasogelei.....ndio akina sie sasa.
Ndo yale yale ya mkakasi....
Mwenza espy, mume wetu MO11 alikuta ua lako liko saa 6 mchana au 12 jioni?
 
Back
Top Bottom