Unapojenga nyumba ya kuishi fikiria sana mahitaji yako halisi, vyumba vitatu vinatutesa wengi

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
kipindi hiki cha likizo, mimi kama mwalimu ili kupunguza zarau maana tunaonekana walimu ndio watu maskini na hatuna akili nchi hii,so kama kawaida likizo hii nimendelea kufanya biashara zangu za mazao na nimejikuta nipo zambia , hulka yangu napenda kudadisi na kujifunza vitu vipya, nilichojifunza kwa mwenyeji wangu huko zambia ni hiki, " ujenzi wa makazi uzingatie sana mahitaji badala ya muenokano wa nje"baada ya biashara nilimtembelea mwenyezi wangu kwenye makazi yake mapya, nilichokikutA ni nyumba mbili moja kubwa with 4 rooms na vikolo kolo vingine, jiko, dinning, store, sitting rooms, na nyumba ya pili ni chumba sebule tena kina paa mbili tu, nyumba ndogo ameifanyia finishing ya maana sana,na ile kubwa anaendelea kufanya finishing,

So nilimuliza why amejenga nyumba mbili, majibu yake yalinifurahisha, anakwambia nyumba kubwa ile kwa ajili ya watoto, wageni na wengine wanaoshi hapo, nyumba ndogo ni kwa ajili yake tu na mkewe, na hiyo nyumba ndogo pana sofa mbili ndogo, zuria, tv ukutani na mtungi pembeni na ukutani ni vile vikabati vya siku hizi ( casas) , nilipomuliza why alifany hivo , majibu yake yalikuwa ni haya, mji wangu wa kwanza nilijenga nyumba moja yenye vyumba vinne, kutokana na uwepo wa familia na vitu vingi vingi ndani ya nyumba nilijikuta master bedroom yangu ilikuwa kama store, na chumbani ndiko huwa natumia muda mwingi kwa siku, so mpangalio wa hovyo wa vitu mle ndani uliochangiwa na udogo wa nyumba nilijikuta mara naamka asubuhi kichwa kinauma , stress na kila nikipima hospital inaoneka siumwi chochote ,

Baada ya hii hali ya kuumwa kijuridia , nilitembelewa na rafiki yangu alikagua makazi yangu na kunishauri nifanye ujenzi huu, na nikwambie ukweli chumba unacholala kikiwa cha hovyo , mpangilio wa hovyo kinachangia stress na kumwa umwa hili sikulijua hadi nilipotembelewa na rafiki yangu ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya akili", aliyenishauri na kufanya nifanye ujenzi huu, chumbani kwangu kwa sasa hakuna tofauti na room za hotelin tu, kuna kabati za nguo , meza ndogo baasi ,

Nimejikuta nalala mahali pazuri na hata msongo na matatizo ya kichwa kuumwa kichwa asubuhi yamepungua, hilo ndilo limenifanya niandike uzi huu, unapojenga fikiria zaidi mgawanyo wa nyumba ndani sio muenokano wa nje , tuliojenga bila kuzingatia mahitaji halisi tunajutia ila ndio hivo kipato hakiruhusu kujenga nyumba nyingine
 
nashauri kwa tanzania hii !
tanzania ardhi ni kubwa kama hupo mjini tengeneza nyumba inayoweza kumudu familia yako kwanza alafu ikifika mda tengeneza nyumbani kwetu huko kijijini ili ukizeeka wajukuu na watoto wako wanakuja kupumzika.

huku ukiwa na shamba na mifugo ukisubiri kifo !.

tujifunze kwa wachaga na wahaya
 
kipindi hiki cha likizo, mimi kama mwalimu ili kupunguza zarau maana tunaonekana walimu ndio watu maskini na hatuna akili nchi hii,so kama kawaida likizo hii nimendelea kufanya biashara zangu za mazao na nimejikuta nipo zambia , hulka yangu napenda kudadisi na kujifunza vitu vipya, nilichojifunza kwa mwenyeji wangu huko zambia ni hiki, " ujenzi wa makazi uzingatie sana mahitaji badala ya muenokano wa nje"baada ya biashara nilimtembelea mwenyezi wangu kwenye makazi yake mapya, nilichokikutA ni nyumba mbili moja kubwa with 4 rooms na vikolo kolo vingine, jiko, dinning, store, sitting rooms, na nyumba ya pili ni chumba sebule tena kina paa mbili tu, nyumba ndogo ameifanyia finishing ya maana sana,na ile kubwa anaendelea kufanya finishing,

So nilimuliza why amejenga nyumba mbili, majibu yake yalinifurahisha, anakwambia nyumba kubwa ile kwa ajili ya watoto, wageni na wengine wanaoshi hapo, nyumba ndogo ni kwa ajili yake tu na mkewe, na hiyo nyumba ndogo pana sofa mbili ndogo, zuria, tv ukutani na mtungi pembeni na ukutani ni vile vikabati vya siku hizi ( casas) , nilipomuliza why alifany hivo , majibu yake yalikuwa ni haya, mji wangu wa kwanza nilijenga nyumba moja yenye vyumba vinne, kutokana na uwepo wa familia na vitu vingi vingi ndani ya nyumba nilijikuta master bedroom yangu ilikuwa kama store, na chumbani ndiko huwa natumia muda mwingi kwa siku, so mpangalio wa hovyo wa vitu mle ndani uliochangiwa na udogo wa nyumba nilijikuta mara naamka asubuhi kichwa kinauma , stress na kila nikipima hospital inaoneka siumwi chochote ,

Baada ya hii hali ya kuumwa kijuridia , nilitembelewa na rafiki yangu alikagua makazi yangu na kunishauri nifanye ujenzi huu, na nikwambie ukweli chumba unacholala kikiwa cha hovyo , mpangilio wa hovyo kinachangia stress na kumwa umwa hili sikulijua hadi nilipotembelewa na rafiki yangu ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya akili", aliyenishauri na kufanya nifanye ujenzi huu, chumbani kwangu kwa sasa hakuna tofauti na room za hotelin tu, kuna kabati za nguo , meza ndogo baasi ,

Nimejikuta nalala mahali pazuri na hata msongo na matatizo ya kichwa kuumwa kichwa asubuhi yamepungua, hilo ndilo limenifanya niandike uzi huu, unapojenga fikiria zaidi mgawanyo wa nyumba ndani sio muenokano wa nje , tuliojenga bila kuzingatia mahitaji halisi tunajutia ila ndio hivo kipato hakiruhusu kujenga nyumba nyingine
Huyo mwenyeji wako hasemi ukweli. Chanzo cha stress zake sio nyumba labda ana malue lue mengine.

Nyumba ya vyumba viine na makolo kolo kibao bado kichwa kinamuuma? Au kwa sababu ana hela nyingi ndio anaturingishia? Ingekuwa hivyo wakazi wa Dar woote wangehamia milembe
 
Back
Top Bottom