Unafanyaje mpenzi wako aki'FLIRT'?

Unafanyaje mpenzi wako aki'FLIRT'?

babu Dc leo niko tech & gadgets swtlo wangu Kaizer kaniambaie nisiingie kabisa huku hadi msimu wa sikukuu upite kisa nisije wazibua wengine maskio wakaanza kukaba za sikukuu kwa wakaka wa jf.


Ndo mnahashuana na Kaizer bila hata haya??

Mbona mie najua Kaizer ni mali ya mtu??

Au nyie mnaamini kuwa kuhashuana ni ruksa?


Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Asilimia kubwa ya watu walio kwenye ndoa, uboyfriend/ugirlfriend walianzaga kwanza na FLIRTING!!!
Usiendekeze hii kitu kama unae waubani wako.Hii ni sawa na kumtupia kuku punje mojamoja ya mahindi ili umkamate kwa kitoweoooo! be aware
 
Beeeeeee!! Babu Dark City unaniita?


Haya Lily, ukuje uwe secretary wa kutunza kumbu kumbu...

Ni mambo gani mtu akifanya mtasema kuwa anaenda kwenye kuhashuana ki..Y2K au ki-dotcom???

Sie orodha yetu ni rahisi sana...kucheza na wajukuu, shemeji zako na wachumba wengine wengine....Na ni kucheza tu, halafu kwenye public...hakuna mambo ya kunusishana harufu za miili kwa web cam au kusimuliana kuhusu kaniki tulizovaa!!

Nataka nitunze hii orodha ili wajukuu watundu kama akina Kongosho wakianza fujo zao niwaripoti kwa kwa mume ya komando King'asti, a.k.a Paw..(hili jina sijui alipewa na nani...haki ya nani linatosha kufukuzia watoto wakalale)!!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Ndo mnahashuana na Kaizer bila hata haya??

Mbona mie najua Kaizer ni mali ya mtu??

Au nyie mnaamini kuwa kuhashuana ni ruksa?


Babu DC!!

babu mie huku simo jamani.

halafu si unakumbuka maneno ya snowhite ambayo mm niliyaongezea msuli juu ya mtu kukosea kwenye uzi wa MMK?? najua unayakumbuka manake ulitumiminia malike ya kufa mtu. kwa kuzingatia koment ile naomba nisiseme lolote. UTU UZIMA DAWA BABU.
 
Last edited by a moderator:
Flirtrng may lead to cheating,naomba niweke waz,among the lads ambao tulianza kuflirt kidogo kidogo,majority of then tume end up cheating nao.so hakuna kumruhusu mum sup kuflirt,because am already a victim of flirt.


Nimekugongea like ya nguvu kwa sababu umetoa msaada mkubwa kwa kuweka data za kutosha....

Nimepata live confirmation kwamba, immunity ya Babu kwenye haya mambo iko juu kiasi cha kutosha!!

Hakuna kuhasuana hashuana katika viwanja vya ugenini....its reserved kwa ajili ya Bibi!!

Babu DC!!
 
Haya Lily, ukuje uwe secretary wa kutunza kumbu kumbu...

Ni mambo gani mtu akifanya mtasema kuwa anaenda kwenye kuhashuana ki..Y2K au ki-dotcom???

Sie orodha yetu ni rahisi sana...kucheza na wajukuu, shemeji zako na wachumba wengine wengine....Na ni kucheza tu, halafu kwenye public...hakuna mambo ya kunusishana harufu za miili kwa web cam au kusimuliana kuhusu kaniki tulizovaa!!

Nataka nitunze hii orodha ili wajukuu watundu kama akina Kongosho wakianza fujo zao niwaripoti kwa kwa mume ya komando King'asti, a.k.a Paw..(hili jina sijui alipewa na nani...haki ya nani linatosha kufukuzia watoto wakalale)!!

Babu DC!!

With honor nitakuwa secretary wako lakini hayo mengine not richabo, asante Babu DC.
 
babu mie huku simo jamani.

halafu si unakumbuka maneno ya snowhite ambayo mm niliyaongezea msuli juu ya mtu kukosea kwenye uzi wa MMK?? najua unayakumbuka manake ulitumiminia malike ya kufa mtu. kwa kuzingatia koment ile naomba nisiseme lolote. UTU UZIMA DAWA BABU.

Nitumie link basi teacher nikazimue hizi akili za 1947!!
 
Daaaa umenichekesha sana Kongosho ila flirt ina nguvu sana na tena hii utumika kuwanasa hasa wanawake wenye matatizo kwenye mahusiano yao, ukimwambia mara mbili mambo ambayo ahambiwi na mwenza wake hakika ni rahisi kunasa!

He he he, nina Phd ya kurushana roho, wakati sifanyi chochote


Hakuna kitu kinaudhi kama 'divided attention' ama mtu kuwa 'present but not available'
Lazima aone PM ya kaka shemeji, naifungua afu najidai naenda kuchukua maji ya kunywa

Naweza kuwa niko kwenye shuka nimejifunika gubigubi na simu yangu nacheeka.

unasikia mtu anapumua hapo pembebi kama Faru
 
women are so much more subtle about flirting clues that men need to really pay attention. Ladies, men are not used to women flirting with them. An overwhelming majority of men said they would just love it if a woman would talk to them first or at least express a larger clue that you were interested in checking them out. #
 
Zama hizi inabidi kuwa makini sana katika hili kuhashua. Na tatizo kubwa ni kuwa hakuna tofauti sana na namna nyingine za 'kuapproach'! Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa ama kutuma wrong signals au kutafsiri signals ndivyo sivyo. Ndio mara kadhaa unasiki wadada wakisema "fulani ananitaka" wakati kumbe jamaa alikuwa ana hashua tu!
 
558878_383446798402705_1019052456_n.jpg


Haya sasa,

Wako wapi anaosema kuwa hausho ni tamu?? Utamu uko wapi sasa?

Naamini jamaa alipewa nafasi ya kujieleza kabla ya kuwahishwa kwenye permanent house!!


Sasa wewe Mkuu The Boss, haya mambo unayaelewa??

Mie nimeshindwa kujua nasimama wapi aisee.... especially kuhusu hausho la kisasa....hadi watu wanafikia kuwekana nusu mringoti kwenye web cam au kupeana sauti za kulegeza magoti kwenye simu?

Enzi zetu tulikuwa hatuli ugali kwa picha ya samaki bwana..ukimtaka samaki basi unachukua ndoana, unaenda mtoni na kumvua....kisha unajilia kwa raha zako..

Huu mchezo utatuharibia watoto na wajukuu ...halafu nchi ibaki ukiwa utadhani imepita genocide!!

Flirting kumbe ni hatari zaidi ya ebola!

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Haya sasa,

Wako wapi anaosema kuwa hausho ni tamu?? Utamu uko wapi sasa?

Naamini jamaa alipewa nafasi ya kujieleza kabla ya kuwahishwa kwenye permanent house!!


Sasa wewe Mkuu The Boss, haya mambo unayaelewa??

Mie nimeshindwa kujua nasimama wapi aisee.... especially kuhusu hausho la kisasa....hadi watu wanafikia kuwekana nusu mringoti kwenye web cam au kupeana sauti za kulegeza magoti kwenye simu?

Enzi zetu tulikuwa hatuli ugali kwa picha ya samaki bwana..ukimtaka samaki basi unachukua ndoana, unaenda mtoni na kumvua....kisha unajilia kwa raha zako..

Huu mchezo utatuharibia watoto na wajukuu ...halafu nchi ibaki ukiwa utadhani imepita genocide!!

Flirting kumbe ni hatari zaidi ya ebola!

Babu DC!!


Tatizo la flirting linaanzia kwenye experience
mtu kama amewahi sex na watu alio flirt nao
ataamini vipi its safe kwa mkewe/mumewe??????
 
Tatizo la flirting linaanzia kwenye experience
mtu kama amewahi sex na watu alio flirt nao
ataamini vipi its safe kwa mkewe/mumewe??????


Ahsante sana mkuu...

Hapa sasa umetupa walau kauli ya kuleta matumaini..Kwamba watu wanaweza kuflirt na kuachana salama...

Ila hii inaweza kutokea kama wahusika walifikai ile level ya kileo...hadi kuoneshana hazina zao kwa web cam au kupeana vionjo vya vocal kwa simu??

Babu DC!!
 
Pamoja na kwamba tumejadili mengi sana kuhusu haya mambo ya kuhashuana, ila nadhani ni vizuri tukasaidiana kwa kuchora mstari (arbitrary and imaginary) kama inawezekana ili na sie wa 1947 tujue hasa tumesimama wapi...

Sina mashaka na mahashuo yetu ya zamani..., ila haya vijana wa dotcom inawezekana ni editions mpya kwa sababu hawa jamaa wameamua kucustomize kila kitu.

Naomba sasa mnisaidie kwa kuniwekea mambo ambayo mtu akiyafanya basi tusema na kujua kuwa huyu sasa anafanya hashuo la kileo (flirting)!!

Wapi dada mkuu Kongosho, teachers gfsonwin Gaijin, system analyst EMT, Komando wa AK47 King'asti, wazee wenzagu Asprin, @FP, snowhite, Mtambuzi, Blaki Womani na wajukuu wote .. Madame B, Erickb52, Preta, Mamzalendo na pacha wake Arushaone, Lily Flower (usijekusema zile habari za nyuki wa bucha)....

Twende kazi sasa....


Babu DC!!


Babu nikujulishe tuu kuwa kuna "rules" mpya za kuhashua katika dunia ya sasa. Nitaelezea tuu rules mpya za upande kiume. Akina Gaijin na Kongosho wataelezea za upande wa kike.

Kwa kifupi sheria zimebadilika ili kwenda fasta na "politically correct" ya "wild and woolly dating" ya dunia ya leo. Unaweza kumsifia mfanyakazi mwenzako kuhusiana na nguo aliyovaa, macho yake, alivyoumbika kwa nyuma? Wakati unamsifia unaweza kumgusa kwa nyuma? Vipi kifuani kwake? Ni zipi hizo sheria mpya?

Kwanza kabisa kabla ya kwenda kwenye hizo rules mpya kuna preliminary issues need to ironed out. Kwanza, inabidi kutofautisha kati ya "creepers" na "flirt". Whilst creepers stalk you down, flirt "plays" with your mind to arouse your interests. Flirts are self-aware and know when they've crossed a line. Creepers are not aware or don't care about crossing the line. Babu enzi zenu kulikuwa na creepers?

Pili you have to play it very cool. Huwezi kumrukia bibi kizee na kusema "Wow! Umeumbika kwa nyuma! Can we blah blah?" Pia tofauti na zamani wanawake wa kizazi cha leo wana-drive na wanapiga kura pia. Kwa hiyo, kuwa makini sana unapovuka barabara. Hakikisha green light za kuvukia ziko on.

Tena tofauti na zamani ambako hata hukukuwa na green lights, siku hizi zimewekwa wazi kabisa. Ugongwe mwenyewe. Pia ukitaka kupigiwa kura ya ushindi achana na uhashuo wa majukwaani. Uhashuo wa one to one ndiyo mpango wa kileo. Twende kwenye rules.

Rule namba moja, tumia strengths (siyo weaknesses) za mwanamke against her. Kama akisema ana boyfriend, mwambie wewe ndiyo boyfriend wake. Kama akisema ameolewa na akikuonyesha pete yake, itoe pete kwenye kidogo, ivalishe kwenye kidogo chako, halafu mwulize nani sasa ameoa? (huko ukiflash kidole chako chenye hiyo pete). Kama una kidole kikubwa mno, I am afraid, wahusika will have consider amending the new rules. lol.

Kama akisema kuwa uache kuwa "creep", mwimbie verses zote za wimbo wa TLC unaoitwa "Creep". Babu mpaka hapo, naona hii rule mpya inaweza kukushinda. lol. Kama akisema ataita polisi mwambie, wewe mwenyewe ni polisi na kuwa yuko under arrest, kwa kuwa too sexy. Ila hii ya under polise arrest nasikia wadau wanataka kuifanyia mabadiliko iwe "umetekwa na nakupeleka kwenye ule msitu wa….." Still debate kwa wadau kama hiyo amendment inafaa.

Kwa hiyo babu nasikia zamani mlikuwa mna-approach mwanamke kwa kuangalia their weaknesses halafu mnazichakachua na kuwa strengths. Vijana wa kileo wana-attack kwa kutumia strengths za mlengwa. Kamwe usimvike mwanamke strength ambayo hana. Kila mwanamke ana strength Fulani. Take your time to look for it and use it effectively.

Rule namba mbili, keep it simple. Forget about the pick up lines. Msalimie tuu kawaida, mwulize jina lake (of course utakuwa tayari unajua jina lake). How does it feel to have her in the palm of your hand? Good I bet.

Rule namba tatu, what do you share in common with the woman? Hutajua unless umwulize. Anapenda ngono? Hey, nauliza tuu. Lol. Aina gain ya ngono? Babu tofauti na zamani siku hizi kuna aina nyingi za ngono. So, the more specific she is the better, usije ukakuta anapenda ambazo hupendi halafu mkashindwa kuhashuana.

Wanawake wa sasa siyo wale wa wakati wenu Babu, na wengi hawataogopa kukuambia aina za ngono wanazopenda. We are talking about women emancipation here. It is everywhere mpaka kwenye ngono.

Rule namba nne, changanua intensity ya uhashuo wako uendane na intensity ya mwanamke. Dunia ya leo wanawake wanatofautiana sana. Ni mwanamke mwenye aibu kwa nje lakini kwa ndani ni chui kwenye sita kwa sita? Mwulize mapema kabisa if this is the case. Ni "party girl" ambaye anaonekana mtu ambaye mnaweza kulewa wote na kusahau anakupenda au kukuchukia kiasi gani? Tafuta majibu ya haya maswali toka kwake directly.

Ni mwanamke ambaye anaweza tuu kuwa amebeba tochi ya "free love" kama ilivyokuwa inafanyika kwenye "orgies" enzi zenu Babu? Hutajua unless umwulize. Uliza, uliza, uliza na uliza tena kuhusiana fantansies zake za kimapenzi na uwezekano wa yeye kuzitimiza na wewe. Hii itakusaida ku-draw a line mapema kabisa. Always kumbuka kutabasamu.

Rule namba tano, kumbuka kucheza na scenarios za kuhashua kichwani mwako kabla ya kutumia kwa mwanamke in real life. Hii itakusaidia kujiandaa. Kwa mfano, umemwa approach mwanamke na kumwambia in a flirting way, "Wanna f**k?" halafu akajibu "HELL NO" au akakupa jibu baya zaidi (unajua uswahilini kwetu tena). Utafanya nini? Kama unajua niambie.

Rule number sita, always keep youself updated na codes zinazotumika kwenye uhashuo wa kileo.

Rule namba saba, hii ni rule ya enzi zenu babu. Bado relevant kwa kizazi cha sasa. The rule is wanawake wanapenda sana dolphins. Natumaini unailewa hii rule.

Mwisho niongezee tuu kuwa with the fast changes in the flirting industry, hizi zinaweza kuwa outdated by kesho au kesho kutwa. So, keep youself updated. Kuwa close na wajukuu zako.
 
uzi umeenda sana huu!lakini siwezi kuacha japo kutia neno!maana nami doh!nina mijituhuma kibao humu katika hili
Sijui pengine niko tofauti au sijui maana sahihi ya hii!
mi naflirt sana na watu sana mno!iwe ofisini au humu!lakini naflirt sana pia na mume wangu!
ni aina flani ya mawasiliano niliyonayo na watu walio karibu yangu!labda pengine ndo mana haijawahi kunikuta nikawa mhanga!
katika kumbukumbu zangu sijawahi kutokewa na mtu niliyewahi kuflirt nae!(sijasema ndo muanze sasa)
ila i find it normal na ni aina yangu ya kutafsiri kuwa niko karibu na huyo mtu!
sijui pengine niko sawa au siko sawa?mwenzi wangu pia hujua kuwa naflirt na believe me hatujawahi kuingia kwenye mgogoro wa aina yoyote kwa sababu ya aina ya mawasiliano nafanya na marafiki zangu hasa humu JF.
well kwa upande wangu post huishia pale ninapomaliza kuandika na kusoma!na maisha yanaendelea !
The Boss kuja hapa milkshake na threesome inaweza kuzua balaa ujue!
Boflo wapi wewe bana mimi love u ujue
Kaizer mwal anajiandaa kuingia darasani umeshaandaa peni na daftari,leo kuna ile topic yetu ya cross multiplication
Asprin kom and do ze nidful mwalimu anahitaji wa kufuta ubao please!
Allien ile date yetu iko pale pale!i hope umeshapata ile dress code tuliyokubaliana
jouneGwalu leo ntakuwa shift mpaka ya usiku for u!usiniangushe please!
platozoom ile album nimekutumia ujue ndo mpango mzima ,are yu ready?
SASA KAMA HII YOTE NI CHEATING mbona ntakuwa na balaa mie!lol
 
Back
Top Bottom