Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k

Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri?

Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji.

Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?
HUo ni mTazamo wako...Mzee Bakhresa ana umri gani?.....lakini mpaka leo anazidi kujenga na kuwekeza....
Hatuishi kwa ajili yetu bali kwa ajili ya wengine,,,LEGACY
 
HUo ni mTazamo wako...Mzee Bakhresa ana umri gani?.....lakini mpaka leo anazidi kujenga na kuwekeza....
Hatuishi kwa ajili yetu bali kwa ajili ya wengine,,,LEGACY
Hiyo legacy itakusaidia nini ukiwa umeondoka hapa duniani? au kuna kurudi tena?
 
Nikiwa mdogo nilidhani mtu mwenye hiyo miaka ni mzee na hawezi kufanya vitu vya maana kumbe ni kuzungukwa na baadhi ya watu wenye mitizamo kama mtoa mada,

baada ya kukutana na watu huku nje aseeh Kuna watu wako na miaka 70 na wanafanya kazi na bado wana Tazamia kufanya mambo makubwa nikaona fursa ndo hii ya kufunguka akili na kuutazama ulimwengu kwenye fursa,
 
Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k

Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri?

Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji.

Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?
Uwiiiiiiihhh.
 
Nikiwa mdogo nilidhani mtu mwenye hiyo miaka ni mzee na hawezi kufanya vitu vya maana kumbe ni kuzungukwa na baadhi ya watu wenye mitizamo kama mtoa mada,

baada ya kukutana na watu huku nje aseeh Kuna watu wako na miaka 70 na wanafanya kazi na bado wana Tazamia kufanya mambo makubwa nikaona fursa ndo hii ya kufunguka akili na kuutazama ulimwengu kwenye fursa,
Kwa umri huo unatafuta fursa ili iweje?
 
Hoja yako imekaa kibinafsi sana,

Ni sawa na kusema kua una umri wa miaka 65 unapanda mti wa matunda wa kazi gani?
Hata ukijenga Nyumba ukiwa na umri wa miaka 20 tu,unaweza kufa baada ya miezi kadhaa tu na Nyumba usiifaidi,

Kama uwezo wa kujenga upo,jenga tu haijalishi una umri gani,
kwani ukijenga Nyumba wakati una umri mdogo,una uhakika gani kua utaishi kwenye hiyo Nyumba yako kwa muda mrefu?

Love the life u live
Live the life u love.
Well said
 
Ili kuwa na sehemu itakayo nifanya nizidi kuwa na utulivu wa hali ya juu (inner peace)
Kama utulivu ulishindwa kuutafuta ukiwa kijana, kwa nini uhangaike hii mida ya jioni ya kuelekea kwa muumba? Ndio maana wanastaafishwa ikiaminika kwa umri ule, tayari ni reject
 
Mara nyingi wazee huwa wanafanya hivyo kwa sababu kuu mbili

1. Wanajenga kwa ajili ya vizazi vyao. Watu wengi wakifika umri huo huwa hawahitaji vingi, sana sana kuiacha familia yake vizuri. Kwa hiyo atajaribu kutengeneza ustawi wa familia yake
2. Kuna ndoto fulani ambazo hazikutimia, labda mtu alikuwa na ndoto ya kujenga nyumba tano lakini hakufanikisha, hivyo anajenga ili kutimiza ndoto zake
 
Wewe usijenge
Kula pombe mwanangu
Ponda mali kufa kwaja
Na ile hela ya kiinua mgongo sio ya kujengea au kufungulia biashara, bali ni hela ya kuripea mwili kutokana na changamoto za uzeeni.
 
kwamba ukijenga ukiwa na miaka 35 huwez kufa ndani ya miaka 2 mbele na nyumba ukaiacha kijana wa ngungu boy
Kupata kifo chini ya miaka ya kustaafu ni ajali, ila baada ya miaka ya kustaafu ni baraka za muumba.
 
Back
Top Bottom