Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,737
- 92,175
VIPAOMBELE VIKUU VYA MWANAUME MWENYE UMRI WA MIAKA 30+
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
1. Kila umri unavipaombele vyake. Umaana wa maisha unauleta wewe kupitia vipaombele vyako.
2. Ili ufanikiwe utahitaji kuzingatia vipaombele kulingana na umri wako, fursa zinazokuzunguka, mbinu, uwezo na vipaji uvyako.
3. Kwa miaka 30+ kijana au mwanaume anatarajiwa kuwa na vipaombele vikuu vifuatavyo;
a. Kuangalia na kulinda Afya yake.
I. Afya ya Mwili kwa Kula lishe bora, kunywa maji ya kwa kitaalam, kufanya mazoezi ya mwili. Kupumzika kwa Wakati.
ii. Afya ya kiakili. Kwa kusoma makala kama zakina Mtibeli hata kama wakati mwingine hauzipendi, kusoma vitabu, kujifunza ujuzi mpya, kutalii katika mazingira mapya. N.k pia kuepuka mambo yanayoharibu afya ya akili kama Stress zisizo na kichwa wala miguu, marafiki wasio na akili wala maarifa yasiyokua. Kila Siku wanazungumzia mambo yaleyale yaliyopita.
iii. Afya ya kiroho. Kwa kufunga walau mara moja kwa wiki au mwezi, kusali walau asubuhi na jioni au mara moja kwa Siku.
Kujitakasa kiroho, kuchamba roho, walau mara moja kwa mwezi.
Afya ya kiroho hurahisisha harakati zako za Kila Siku za utafutaji. Na huzuia watu wabaya ambao kimwili huwezi kuwatambua.
iv) Afya ya kihisia. Moyo wako unahitaji kuwa na Amani na furaha. Afya ya kihisia itatokana kwa kufanya mambo mema na mazuri. Kufanya kazi unayoipenda. Kuishi vizuri na watu wanaokuhusu ikiwemo wazazi, mkeo/mumeo na watoto, Wakwe n.k.
Tafuteni Amani na watu wote. Hiya ni Kanuni ya afya ya moyo(kihisia)
B) Kufanya KAZI
Hiki ni kipaombele cha pili kikuu. My friend huwezi ishi maisha kwa heshima na furaha kama huna kazi.
Na huwezi kufanya kazi kwa ufanisi kama hauna afya njema.
Ili ufanye kazi kijana wa miaka 30+ utahiyajika mambo yafuatayo;
I) Afya njema
ii). Elimu, Ujuzi na maarifa kwa kazi husika
iii) Mawasiliano na huduma Bora kwa Wateja wako.
iv) Elimu ya Fedha ili uweze kumudu na kuzalisha maradufu mapato ya kazi yako.
v) uwezo wa kuunda mtandao wenye tija.
vi) uwezo wa kubadilika kulingana na muktadha na mazingira.
C) Kujenga Familia Bora na Imara.
Hiki ni Kipaombele Cha Tatu Kikuu.
Unahitaji familia kwa sababu Mbalimbali. Lakini sababu kuu ni kama ifuatayo;
I) Usaidizi wa ndoto zako.
Familia ndio nguzo muhimu ya ndoto zako.
Umri wako hapa Duniani hautazidi miaka 100. Kumaanisha possibility ya kutotimiza malengo yako ni asilimia Mia moja.
Familia itakusaidia kutimiza malengo yako hata ukiwa haupo.
Familia kubwa hutumia Familia kama silaha ya kuu ya mwisho na backup ya kutimiza malengo ya kizazi.
ii) Kupata Mahitaji ya Kimwili na kihisia bila kujivunjia heshima.
Mtu asiye na familia automatically ni Mhuni kwa sababu mahitaji ya msingi ya kimwili kama Ngono atayapata kwa kujidhalilisha na kuvunja maadili Fulani.
Sex ni moja ya basic need kwa mwanadamu
iii) Kuacha Urithi wa Dunia.
Familia ndio njia halali na Bora ya kuacha urithi wa kizazi chako. Kikiwa tayari ndani ya mfumo wenye nguvu.
Watoto wanaozaliwa bila familia hujikuta katika wakati mgumu. Kwani wapo nje ya mfumo. Ni kama mimba zilizotungia nje ya mfuko wa uzazi.
iv) Himaya
Mwanaume huoa ili apate himaya yake. Mfalme asiye na Malkia ni mfalme asiye na Milki.
D) Kujenga Jina lenye Heshima.
Katika umri wa miaka 30 ndio kipindi cha kusawazisha makosa ya kitabia na maadili uliyoyafanya ukiwa na miaka 15-29.
Katika umri chini ya miaka 30 jamii inakuchukulia kama mtoto, damu changa unayeweza kufanya makosa kwani ni umri wa kujaribu na kujifunza.
Lakini miaka 30+ huu sio umri wa kuleta utoto wako au kujifanya mtoto.
Ni umri wa kubisha Mlango na kuingia kwenye majukumu ya mwanaume na Baba.
Jamii haitakusamehe ukifanya mambo ya kijinga katika umri huo.
Chochote utakachofanya kitakulebo.
e). Utambulisho.
Umri huo ni umri wa kujenga utambulisho kwenye Jamii yako. Wewe unafanya kazi gani?
Sio umri wa mizaha au ushabiki wa kitoto kama watoto wa chini ya miaka 30.
Huo ndio umri wa kuitwa Pastor Fulani,
Fundi Fulani,
Mwalimu Fulani,
Dokta Fulani,
Kiongozi Fulani
Mwandishi fulani.,
Dereva Fulani
Afande Fulani, n.k.
Sio umri wa kujiita AKA za kitoto ambazo hazihusiani na kazi yako au taaluma yako
f) Kuwa na Anuani yako, makazi.
Huo umri lazima uhakikishe unajitegemea. Unasehemu ya kuishi hata kama ni chumba kimoja.
Hata kama ni kijumba cha mabati au nyasi. Kujitegemea ni kujitegemea.
Kuliko uishi kwa dadaako au kakaako au ndugu au wazazi kwa umri huo ni Bora uparangane.
Kujitegemea ni kujitawala. Utawala ni Moja ya nguzo ya uanaume.
Huwezi kuwa mwanaume kama bado maisha yako yanategemea MTU mwingine ili uishi.
Kuna Wale wanakuambia je kama wazazi wananyumba nyingi. Sawa.
Mwambia Babaako mwenye hizo nyumba akukodishie nyumba yake wewe uwe unampa pesa. Huo ndio uanaume. Sio upende vya burebure kupewa pewa. Sio dalili nzuri na wanaume waliokomaa hawakogi hivyo
Aiseeh! Mtibeli Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam