Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Una miaka zaidi ya 65, unajenga nyumba ya nini?

Mara nyingi wazee huwa wanafanya hivyo kwa sababu kuu mbili

1. Wanajenga kwa ajili ya vizazi vyao. Watu wengi wakifika umri huo huwa hawahitaji vingi, sana sana kuiacha familia yake vizuri. Kwa hiyo atajaribu kutengeneza ustawi wa familia yake
2. Kuna ndoto fulani ambazo hazikutimia, labda mtu alikuwa na ndoto ya kujenga nyumba tano lakini hakufanikisha, hivyo anajenga ili kutimiza ndoto zake
Akisha timiza ndoto, ndio inakuwaje?
 
Huu ni umri wa kupumzika na kutafakari yale yote uliyoyatenda katika ujana wako, kuanzia kimasomo, kimaisha, kikazi n.k

Ni umri ambao hauna tija tena katika uzalishaji; ndio maana wengi wakifikia huo umri hulazimishwa kustaafu. Swali, ni wangapi wako tayari kustaafu wakifikia huo umri?

Kustaafishwa maana yake, kwa huo umri wako hauhitajiki tena katika uzalishaji, bali unatakiwa kupisha nguvu mpya zenye ufanisi katika utendaji.

Hii inatafsiri, huo ni umri wa kukataliwa na jamii, na jamii ikikukataa unatakiwa kuwa karibu na muumba wako; sasa najiuliza swali kwa umri huo, unajenga nyumba ya nini, ikiwa jamii haikutaki na unakuwa umebakiza miaka michache ya kuonana na muumba?

Kiongozi , kwenye vipato vya ulimwengu wa tatu na hii mishahara ya walio wengi huku wanafamilia....na nafasi zilizonyingi wala hazina fursa ya kula kwa urefu wa kamba hivyo kupelekea baadhi ya wastaafu kutokuwa na Nyumba, hivyo sioni tatizo kujenga na hata kama ungekuwa na miaka 80?
Namaanisha unajenga nyumba ili wakaishi wengine kama na wewe unavyoishi nyumba walizo jenga wengine.
Sio kila kitu unafanya kwa faida yako mwenyewe...acha ubinafsi!!!
 
Kiongozi usisahau kuwa, kwenye vipato vya ulimwengu wa tatu na hii mishahara yenu ya walio wengi huku unafamilia....bila kula urefu wa kamba yako, unaweza jikuta unastaafu bila hata kuwa na kibanda, hivyo sioni tatizo kujenga na hata kama ungekuwa na miaka 80?
Namaanisha unajenga nyumba ili wakaishi wengine kama na wewe unavyoishi nyumba walizo jenga wengine.
Sio kila kitu unafanya kwa faida yako mwenyewe...acha ubinafsi!!!
Muda wa kumtumikia muumba na kutoa fungu la kumi bila kupunja wanaupata wakati gani?
 
Ilimradi unaona mambo yako yanakwenda basi Fanya unavyojua...Dunia hii ilivyo zipo namna nyingi Sana za kufurahia maisha, hatuwezi kupita njia moja.... possibilities ni nyingi Sana duniani.
 
Ilimradi unaona mambo yako yanakwenda basi Fanya unavyojua...Dunia hii ilivyo zipo namna nyingi Sana za kufurahia maisha, hatuwezi kupita njia moja.... possibilities ni nyingi Sana duniani.
Ukifikisha miaka 65+ furaha yako itakuwa ni nini?
 
Back
Top Bottom