Umeumiza watu halafu unataka kuokoka bila kuwaomba msamaha uliowaumiza, hilo haliwezekani!

Mungu angekua katili kama unavyomuelezea hapo, dunia ingekuwa chungu sana kwa wakosefu. Ndo maana tunaambiwa M/Mungu ni mwingi wa Neema na Rehema. Pia M/Mungu ni baba wa wote.
anatudekeza lakini watu tumekuwa wagumum kiama chaja na hukumu itasindikizwa na maumivu makali sana na vilio watu wakisaga meno
 
Ni mwepesi wa ksamehe ukianza kuomba msamaha kwanza kwa uliowakosea kisha mkiweka mambo yenu sawa ndio uende kwake, huwezi mdhurumu mtu alafu uende kwa Mungu mwenye haki akusamehe , NEVER !!!! Huyo uliemdhulumu nae anamuomba Mungu
Kama uliyemkosea kafariki kabla hujamuomba msamaha inakuwaje?
 
Kama uliyemkosea kafariki kabla hujamuomba msamaha inakuwaje?
Jitahidi utafute mabaki yake (watoto wake) uwaeleze kila kilichotokea bila kuruka chochote kisha uwaombe msamaha, ukisaamehewa ndio uombe sasa msamaha kwa Mungu,

Ukikataliwa ama kama hujui alipo wala hujui mabaki yake yalipo hesabia ni deni linalosubiri hukumu
 
Mungu anaweza kukusamehe dhambi zako binafsi tu zisizodhuru wengine ama ambazo mmeshirikiana watu kwa hiari yenu bila kudhuru, mfano kulewa kivyako, umezini na kahaba, kujichua, n.k.

Hizo dhmbi zingine za kuwaumiza wengine yeye anahusika baada ya kuwaomba msamaha uliowakosea,
Andiko gani limesema haya?
 
Umewahi mpa Mungu sadaka au unawapa wachungaji wako?
Lengo la kutoa sadaka ni iende kwa lengo lililodhamiriwa, kama mchungaji kapiga sadaka hio ni dhambi yake ila kwenye kitabu cha Mungu muumini anaonekana katoa sadaka kwake, mzigo ataubeba huyo mchungaji aliefanya mambo yake gizani
 
Lengo la kutoa sadaka ni iende kwa lengo lililodhamiriwa, kama mchungaji kapiga sadaka hio ni dhambi yake ila kwenye kitabu cha Mungu muumini anaonekana katoa sadaka kwake, mzigo ataubeba huyo mchungaji aliefanya mambo yake gizani
Nimekuuliza ulishawahi mpa Mungu sadaka?
Mungu aliitumia kufangia nini hiyo sadaka?
 
Wanaopotoshaaaa ni hawa manabiiii machoko wa sasa eti nifatishe sala ya toba utasamehewa dhambi nyokoooo kabisa Mungu anafanyiwa pranks
 
Unampangia Mungu namna ya kutenda? Mwanamke Kahaba aliyevunja ndoa za watu wengi na kuwaumiza wengi, alipomuona Yesu alienda kumbusu miguu na kumpaka mafuta, Palepale Akasamehewa dhambi zake zote!
 
Ok ni vema basi tushauriane maana na mimi sijui kila kitu, kwa mtazamo wako unaonaje ?
Dhambi pekee isiyosamehewa ni kumkufuru Roho Mtakatifu. Zingine zote ukitubu na kuacha zinasameheka.

“Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.

— Mathayo 12:31 (Biblia Takatifu)
 
Nimekuuliza ulishawahi mpa Mungu sadaka?
Mungu aliitumia kufangia nini hiyo sadaka?
Nikitoa sadaka inayoenda kuongeza ukubwa wa jengo la kanisa ni kwamba kuna watu wengi zaidi tutaweza kusali kanisani

Nikitoa sadaka ya kwenda kusaidia wenye shida ni kwamba inaenda kupunguza shida zao, n.k.

Ni mambo yampendezayo Mungu

Tatizo linapokuja ni baadhi ya wachungaji kugeuza sadaka za kufanya yampendezayo Mungu kuigeuza kufanya anasa na kujilimbikizia mali,
 
Utasikia

fulani alikuwa jambazi hapo zamani kwa sasa kaokoka
Fulani alikuwa tapeli sugu hapo zamani kaamua kuokoka
Fulani alivunja ndoa za wengi hapo zamani kaamua kuokoka

NONSENSE, UJINGA!!

Mnakosea sana, Mnjidanganya, Mambo hayendi hivyo !!



1. TUACHE MASIKHARA KWA MUNGU WA HAKI

Ulikuwa jambazi umeibia watu, wameshindwa kuendelea kwajili yako, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowaibia

Ulikuwa mzinzi, umekuwa chanzo cha ndoa za watu kuvunjika, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa mme / mke uliemvunjia ndoa

Ulikuwa muuaji, umeua baba, familia zinateseka, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliewaulia baba

Ulikuwa dhulumati, umedhulumu watu, wanaishi maish ya dhiki, Mungu wa haki hawezi kukutakasa bila wewe kupata msamaha wa uliowadhulumu

2. MIFANO

Baada ya Daudi kushika madaraka nchi ikawa ina majanga, alipomuuliza Mungu nini chanzo, aliambiwa utawala uliopita wa Sauli uliua wana watu wa Gibeon hivyo waende kwao wayamalize,baada ya hapoataitakasa nchi, walipoenda huko wa Gibeon waliwambia wao hawataki dhahabu wala Silver, wanataka kulipiza kisasi, wawape wana wa Sauli wa kiume saba wawaue na walipofanya hivyo nchi ilitakaswa.

Mfano mwingine Yesu mwenyewe aliwaambia wanafunzi wake kwamba kabla ya kutoa sadaka kaweke kwanza mambo sawa na uliowakosea, pia alishauri patana na mshitaki wako kwanza kabla hamjafika kwa hakimu

Mfano mwingine wa zakayo alikumbuka dhambi zake na akasema atawarejeshea mara kumi aliowadhulumu, bda ya hapo ndipo aliweza kupokea wokovu

3. AGANO LA KALE LILIRUHUSU JICHO KWA JICHO, JIPYA JE ?

Agano la kale liliruhusu kulipiza jino kwa jino kama huo mfano wa kwanza wa kulipiza kisasi kwa kuua lakini haimaanishi agano jipya limefuta kila kitu, kilichobadilika ni kwamba mtu aliekukosea akija kukuomba msamaha haupaswi kulipizajino kwa jino, ni aidha umsamehe au kama roho inasita wewe mwambie wazi tu huwezi, hakuna haja ya kulipiza kwa jinsi alivyokuumiza

4. HAIWEZEKANI KUOKOKA BILA KUPATA TIKETI YA MSAMAHA WA ULIOWAUMIZA

Ni hivi, Mungu sio dhalimu,wewe unaweza kukuta umenitendea mabaya halafu unaenda kanisani kuokoka lakin unasahau mimi kila asubuh naamka na majereaha uliyoniachia aidha umeniibia duka nimefirisika, umeua watu wangu wa karibu naumia, umeniibia mke ndoa ilivunjika, umenidhulumu kiwanja sina nyumba, n.k.

Mungu hawezi kusahau uovu ulionifanyia kisa eti umebadilika, unaenda sana kanisani, unatoa sadaka (zikiwemo pesa ulizonidhulumu ), n..k NEVER !!!! Na kuhakikishia Mungu ni wa haki hata sikia sala yako ya kuokoka kama hutotubu maovu yako kwa uliowaumiza, Mungu haongeki !!!


5. MWISHO KABISA

Mwenyezi Mungu anachukizwa mno na dhambi, hakikisha unajizuia sana kutenda dhambi kuumiza wengine na ukifanya hivyo fanya uwezavyo uwaombe msamaha, ndio tiketi pekee ya kuomba msamaha kwa Mungu
Sawa .mkuu
 
Nikitoa sadaka inayoenda kuongeza ukubwa wa jengo la kanisa ni kwamba kuna watu wengi zaidi tutaweza kusali kanisani

Nikitoa sadaka ya kwenda kusaidia wenye shida ni kwamba inaenda kupunguza shida zao, n.k.

Ni mambo yampendezayo Mungu
Yanayompendeza Mungu lakini Sadaka yako humpi Mungu.
Maana Mungu hahitaji fedha zako ili kuitwa Mungu. Nchi na vyote viijazavyo ni mali hake, hana uhitaji. Sadaka zinatolewa kwa mchungaji wako, na ndie mtumiaji, Mungu hachukui hizo sadaka.
 
Unampangia Mungu namna ya kutenda? Mwanamke Kahaba aliyevunja ndoa za watu wengi na kuwaumiza wengi, alipomuona Yesu alienda kumbusu miguu na kumpaka mafuta, Palepale Akasamehewa dhambi zake zote!
Hakukuwa na taarifa kwamba alikuwa anaiba waume za watu ila nitalifanyia uchunguzi
 
Back
Top Bottom