Dhambi ambazo huwezi tubu peke yako bila kushirikisha watumishi wa Mungu

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,160
22,665
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, au ukiota unazini ndotoni na mtu au watu usiowafahamu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

Kuzini na mke wa mtu, faini ya juu ni kulipa Mahari aliyotoa muoaji Ili akusamehe, kushirikisha mtumishi ni kutumia BUSARA ya Mungu Ili muibiwa mke aridhie kukusamehe kutomlipa, au akupunguzie faini.

(Mithali 6:20-35,) UZINZI hufunga NAFSI, Amri ya Mungu usizini (Kumbukumbu la torati 5:1-21)

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko. ( Mwanzo 38:9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kumwaga shahawa nje ya uke makusudi Ili asizae na mke aliyepewa.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. mwanzo 38:9-10, Onani aliuwawa Kwa dhambi hiyo, ( kumbukumbu la torati 5:1-21) Amri za Mungu Usiue.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA utoe sadaka, uvunje NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho iondolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya. Mbinguni huingii ng'o!! (Mwanzo 38:1-25) Mungu alimwua Onani Kwa kumwaga shahawa nje ya uke Ili asizae na mke wa marehemu kaka yake.
Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. ( Mwanzo 38:9-10, (Mithali 6:20-35)Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe na Mungu.

(1 Wakorintho 6:9-11), (Ufunuo wa Yohana 21:8) (Mzo 38:9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kutenda Tendo la NDOA kinyume.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli ,beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

(Kumbukumbu la torati 5:1-21) Usiue ni Amri ya Mungu.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

(Mwanzo 38-9-10) Mungu alimwua Onani Kwa kutenda kinyume na Utaratibu wa Tendo la NDOA na taratibu za UZAZI alizoweka Mungu.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi. ( Acts 9:3-6) Sauli alikuwa mwuaji, Yesu alimwelekeza aende Kwa mtumishi.

(Kumbukumbu la torati 5:1-21) Mungu ameamrisha " Usiue".

11. IBADA ZA SANAMU, KUSHIRIKI IBADA ZA WAFU NA KUTOA SADAKA KWA MIZIMU KIMILA NK NK.

Kushiriki Ibada za KIMILA na Kutoa sadaka Kwa Roho za kishetani za Mababu, ni DHAMBI pia, ni kufungwa ni Utumwa ambao huwezi kujifungua pekeako.

(Mithali 6:20-35) kifungo Cha NAFSI sababu Ibada ya sanamu ni UZINZI kiroho mbele za Mungu, ( UFUNUO 21:8, (1 korinthians 6:9-11) watendao uchawi na Ibada ya sanamu watatupwa Jehanum.

Ukiamua kuacha na kuokoka, hatua inayofuata ni kushirikisha watumishi kukusaidia kukutenga na madhabahu hizo.

Sadaka ni LAZIMA, sababu, Ulimwengu wa Nuru na Giza sadaka ni inevitable. Amen

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

NB: Si DHAMBI zote zinahitaji kuona mtumishi wa Kweli kukusaidia kufunguliwa pingu za dhambi, ni baadhi ya dhambi ambazo Zina vifungo na attachment na maagano ya kipepo na kishetani.

ANGALIZO: Sadaka tutoazo Si Kwa ajili ya kununua Muujiza, au kununua Msamaha wa Mungu, Yesu msalabani alikwisha maliza yote Kwa Damu yake msalabani. Sadaka tunatoa kama shukrani tu na kuonyesha Upendo Kwa Yale Mungu alikwisha tutendea.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim, U-Tube., Promover Tv channel U-Tube.

Ikiwa hujampokea Yesu kuwa BWANA na Mwokozi wako, fuatisha Sala hii,

EE YESU, NINAKIRI KWAKO KUWA MIMI NI MWENYE DHAMBI, NINAOMBA UNISAMEHE, ULIFUTE JINA LANGU KATIKA KITABU CHA HUKUMU,ULIANDIKE KATIKA KITABU CHA UZIMA, NINAOMBA UWEZO WA KUSHINDA DHAMBI, NIWEZESHE NIISHI MAISHA MATAKATIFU.

Ameen
 
Mnajiiiiiiiipa presha .Nan kakwambia Mungu ana formalities za kibinadam zaid namna hii!!???

Ujue anayekuondolea hatia sio kutubu mbele za mtu. NI Holly spirit, period!!!! Hii kwenda mbele za watu imekaa kisailolojia tu ili ku bust iman yako ila hata sio lazima wala haina ukwel...
 
Alisema hivi, pazia la hekalu lilipasuka kuruhu hata wasio wachungaji wala makuhani kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwenye kiti cha Rehema. Sharti uingie na damu na jina la Yesu Kristo. Acheni kutaabisha watu wa Mungu. Kinachofuta dhambi sio ombi la mchungaji, ni Damu ya Yesu tu. Wote tu makuhani Kwa Mungu wetu.
 
Wachungaji mnatengeza kila namna ya kupata pesa umekazania sana katika sadaka
Ikiwa Mungu alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo awe sadaka ya kutukomboa,

Nani wewe usitoe sadaka. Sadaka ni Kwa ajili Yako, usidhani unamfaidisha Mchungaji.

Elia alilishwa na Mungu kupitia kunguru, usidhani watumishi wa Mungu wanategenea sadaka zako.

Na usijidanganye ukaenda Kutoa sadaka ya wizi, au ya kutapeli madhabahuni, utaondoka na LAANA.

Ubarikiwe.
 
Alisema hivi, pazia la hekalu lilipasuka kuruhu hata wasio wachungaji wala makuhani kuingia Patakatifu pa Patakatifu kwenye kiti cha Rehema. Sharti uingie na damu na jina la Yesu Kristo. Acheni kutaabisha watu wa Mungu. Kinachofuta dhambi sio ombi la mchungaji, ni Damu ya Yesu tu. Wote tu makuhani Kwa Mungu wetu.
Yaani uzini na mke wa Jirani Yako sirini halafu utubu sirini?

Mwombee Mungu Roho mtakatifu akufunulie aloyasema mwenyewe kabla ya kupinga.
 
Salaam shalom.

INTRODUCTON.

Imeandikwa, Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na haki, hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote.( 1 Yoh 1:9).

Dhambi ni kutotii, kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu. Na Roho mtakatifu yupo kutukumbusha dhambi zetu Ili tuzitibie Ili tuendelee kuwa WATAKATIFU.

DHAMBI AMBAZO KAMWE HATIA YAKE HAITAKUONDOKA HADI USHIRIKISHE WATUMISHI WA MUNGU ILI UOMBEWE UKIAMBATISHA NA SADAKA YA UKOMBOZI NI ZIFUATAZO:

1. ZINAA NA UASHERATI.

UASHERATI ni kufanya Tendo la zinaa na mtu nje ya NDOA asiye mkeo au mumeo.

UZINZI ni kufanya tendo la uchafu, zinaa kabla ya Kuoa au Kuolewa.

Ukizini na mke wa mtu au mume wa Mtu, usijidanganye kuwa ukitubu sirini utasamehewa, HATIA itaendelea kuwepo Hadi uwatafute watumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi. Watumishi Wana BUSARA ya kusuluhisha dhambi hiyo pande zote mbili Ili ufunguliwe.

2. USHOGA.

Ikiwa uliwahi kuwa shoga, ukaamua kuacha, kamwe usitubu sirini na kuishiwa hapo, USHOGA huambatana na mapepo na kufungwa NAFSI, mfungwa kamwe hawezi jifunguanpingu mwenyewe, unawahutaji watumishi wa Kweli Ili UOMBEWE na kuwekwa huru, sadaka ni LAZIMA Ili itolewe huko.

3. USAGAJI.

Mwanamke pia aliyewa kufanya dhambi hiyo, huwezi kufunguliwa na Utumwa na HATIA hiyo pekeako Kwa kutubu sirini, nenda Kwa watumishi wa Kweli, Ukiwa na sadaka ya Ukombozi.

4. PUNYETO/ KUJICHUA.

Ikiwa uliwahi kujichua, ukaamua kuacha, unahitaji kwenda Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli Ukiwa na sadaka ya Ukombozi Ili ufunguliwe, Mpiga PUNYETO ni mfungwa, ni mke au mume wa Roho chafu katika Ulimwengu wa Roho, hivyo kufunguliwa ni LAZIMA itoe sadaka, ivunjwe NDOA chafu hiyo ya kiroho na hati ya NDOA chafu ya kiroho ionfolewe, usipofanya hivyo, unajidanganya.

Mbinguni huingii. Neno Hilo hapo juu ni ROHO. Amen.

5.MWANAMKE KUOA MWANAMKE/MWANAUME KUOA MWANAUME MWENZIE.

Kutubu dhambi hii sirini bila watumishi wa Mungu ni kujidanganya. Chukua sadaka, nenda Kwa mtumishi, Sema Kweli Ili UOMBEWE na kufunguliwa, NDOA haramu ivunjwe na ufungwa wako kiroho uondolewe. Amen.

6. ORAL SEX.

Ikiwa uliwahi kushiriki oral sex, kunyonya au kuramba Kwa mdomo sehemu za Siri za mwanamke au Mwanaume na ukatambua ni DHAMBI, ukaacha, Bado u kifungoni.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli wa Mungu ufunguliwe.

7. ABORTION./ UTOAJI MIMBA/ KUFUNGA UZAZI/ KUTUMIA VIDONGE VYA KUPANGA UZAZI.

Kimbia haraka Kwa mtumishi wa Mungu wa Kweli beba sadaka kulingana na uwezo wako, UOMBEWE ufunguliwe.

Ukipuuza Utakataliwa GETI la Mbinguni.

9. IKIWA ULIWAHI TUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME/ KIKE.

Chukua sadaka, mwone mtumishi wa Kweli UOMBEWE na kufunguliwa.

10. MAUAJI.

Ikiwa uliwahi kuua bila kukusudia ,ukahukumiwa JELA ukatoka, ikiwa uliua Kwa Siri na hukubainika, ikiwa ulishiriki kuua, usijidanganye kuwa unaweza kutubu sirini, HATIA Ili ikuondoke uwe na Amani, Tafuta kiongozi wa Mungu wa Kweli mwenye BUSARA za Mungu, akuongoze Cha kufanya, utoe pia sadaka ya Ukombozi.

HITIMISHO.

Dhambi nilizotaja hapo juu, ni baadhi tu ya dhambi ambazo huwezi tubu pekeako, zimetajwa sawasawa na Ruhusa ya Roho mtakatifu Kwa mtumishi wake sawasawa na ufunuo wake apendavyo.

Mungu awabariki.

Source: Nabii Justine Ibrahim.

Amen.
Hakuna mwanadamu anayeweza kusamehe dhambi isipokuwa mungu...Kipi bora mtu ajulikane na wanadamu kuwa ametubu au ajulikane na mungu ajuaye mawazo ya mtu?...Kizazi cha nyoka kinataka kujishibisha kwa kumkufuru mungu..Yafaa ufungiwe jiwe shingoni ukatoswe baharini muovu wewe!
 
Mnajiiiiiiiipa presha .Nan kakwambia Mungu ana formalities za kibinadam zaid namna hii!!???

Ujue anayekuondolea hatia sio kutubu mbele za mtu. NI Holly spirit, period!!!! Hii kwenda mbele za watu imekaa kisailolojia tu ili ku bust iman yako ila hata sio lazima wala haina ukwel...
Roho mtakatifu ndiye aliyetoa ujumbe huo kupitia mtumishi wake.

Kabla ya kupinga, ikiwa umejazwa Roho mtakatifu, omba akuthibitishie ikiwa ujumbe huo umetoka kwake au la.
 
Hakuna mwanadamu anayeweza kusamehe dhambi isipokuwa mungu...Kipi bora mtu ajulikane na wanadamu kuwa ametubu au ajulikane na mungu ajuaye mawazo ya mtu?...Kizazi cha nyoka kinataka kujishibisha kwa kumkufuru mungu..Yafaa ufungiwe jiwe shingoni ukatoswe baharini muovu wewe!
Anayesamehe dhambi ni Mungu.

Mtumishi wa Mungu ni chombo chake na msaada wa kukufungua pingu wewe uliye mtumwa.

Amen
 
Wachungaji sasa walivyo wambea, unaamua utubu dhambi zako masikini unamwambia nilitoa mimba.....anapaza sauti sasa kanisa zima oooooh shika raba shikaa raba umeuaaa kiumbe cha mungu kanisa zima linaguna haaaaaa.

Kwendeni huko Mungu angekua anatangaza hivi maovu yetu ingekuaje.
 
Ikiwa Mungu alimtoa mwanawe wa pekee Yesu kristo awe sadaka ya kutukomboa,

Nani wewe usitoe sadaka. Sadaka ni Kwa ajili Yako, usidhani unamfaidisha Mchungaji.

Elia alilishwa na Mungu kupitia kunguru, usidhani watumishi wa Mungu wanategenea sadaka zako.

Na usijidanganye ukaenda Kutoa sadaka ya wizi, au ya kutapeli madhabahuni, utaondoka na LAANA.

Ubarikiwe.
Kwanini ufaidike wewe kwa dhambi za mwenzako?Kumbe ww unapenda watu wafanye dhambi upate sadaka..Kutoa sadaka ni sawa ila mwenye kuhukumu ndye anayesamehe dhambi za watu ndio nyny mnatoaga siri za watu nje wakija kwenu..Tubuni na kumwelewa kristo.
 
Aisee kama ni hivyo basi kazi ipo! Nilijua nikipiga magoti na kutubu ile kweli kabisa halafu natafuta wahitaji nawasaidia imeisha hiyo,kumbe mpaja nije na bahasha mkononi.
Si DHAMBI zote Hadi uende Kwa mtumishi, ni baadhi.

Mfano, huwezi kufirana, kuua au kuzini na mke wa Jirani Yako halafu ukatubu sirini, dhambi hizo hapo juu Zina mikataba na vifungo vya kipepo ambavyo lazima uhusishe Mtumishi.
 
Back
Top Bottom