secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,554
- 49,975
Wakikuongelea vibaya lazima nile nao Sahani Moja.Nje ya mada, nasikia mnanizogoa ila hamnitag jamani, shida nini.
Naomba ukiona nafanyika mada huko uniite nije nione mnaongelea nini 😂 😂
Wakikuongelea vibaya lazima nile nao Sahani Moja.Nje ya mada, nasikia mnanizogoa ila hamnitag jamani, shida nini.
Naomba ukiona nafanyika mada huko uniite nije nione mnaongelea nini 😂 😂
Wige ulipotelea wapi? Kitambo sana, woiiiih
Bila kumjulisha? sidhani kama hakujua, ila naamini alipingana na huo mpango wa kuweka majina ya watoto badala ya majina yao.Kwanini Jane alimilikisha nyumba watoto na yeye kuwa msimamizi bila kumjulisha mumewe! Sheria ya mirathi inasemaje kuhusu mali inayopatikana ndani ya ndoa hapa inahusu nyumba. Kiwanja ni cha Jane lakini alimtumia mume wake awekeze kisha amtose kwa kisingizio cha kiwanja ni chake, huu ni mchezo wa wachaga.
Uniite tuje tule nao sahani moja 😂Wakikuongelea vibaya lazima nile nao Sahani Moja.
Nimeshasikia mengi sana kuhusiana na mkasa huu, ila ki ukwel inaonekana marehem alikuwa mbinafsi sana, hakutaka nyumba iwe ya familia (baba, mama na watoto) ila alitaka iwe yake yeye na watoto pekee!
Inakuwaje mpo katka ndoa halaf baba ambae ni kichwa cha familia anatengwa katka umiliki, et kisa mwanamke ndo kanunua kiwanja na kujenga, mbona sis wanaume unapokua na mali zinahesabika ni mali za familia (na mke akiwemo)!?
Ila kuna wanaume wananyanyasika sana katka ndoa zao, sema machoz na maumiv yao hakuna anayeyajali!
MambooHabari Yako
Aunt mmoja aliwahi dhulumiwa na hao ndugu wa mume na wakwe aliuvaa umaskini hakuamini mpk aje asimame hakuna laana hakuacha na mume kamwachia watoto watatu ni miaka ya nyuma sio sasa....Duuuh! Kwani hizo mali zina utata hadi aogope ndugu wa mume? If mumewe akifariki??
Na amemuua nyumbani kwao na watoto wakiwepo 💔Mbinafsi ni mwanamme hapo. Unamuuaje mama wa watoto kisa nyumba? Jamaa hata arudi uraiani leo watoto wake hawawezi kabisa kua karibu nae tena
Unfortunately… these days tuna two versions of truth#FACT-CHECKING
Usidanganyike, mambo kwa ground yapo tofauti sana. Kwa ushahidi, tupitie ni yapi ya kweli na yapi si kweli kuhusu kifo cha Jane Maloo Urassa ⚰️ aliyeuawa na Laurence Kweka, mwanaume aliyekosa akili, busara na utashi wa kibinadamu.
View attachment 3686843
- Jane na Bw. Kweka waliishi kwenye ndoa kwa miaka 18 na miezi 8 na wana watoto 4 - KWELI
- Jane alikua mtumishi aliyeajiriwa, mwenye kipato chake binafsi, na elimu ya chuo kikuu (Masters) - KWELI
- Jane alimiliki mali binafsi alizotafuta kabla ya ndoa ikiwemo kiwanja kilichojengwa nyumba iliyoleta mgogoro - KWELI
- Jane alikua ameshaondoka hapo nyumbani kwenye migogoro kwa zaidi ya miezi miwili na kwenda kuishi kwa ndugu zake na alimuachia bwana Kweka nyumba na pamoja na watoto wote aishi nao - KWELI
- Mgogoro mkubwa ulijitokeza miezi kadhaa nyuma baada ya hati ya nyumba kutoka na majina ya watoto na Jane kama msimamizi mpaka pale mtoto wao wa kwanza atakapofikisha miaka 18 - KWELI
- Jane alitaka hati ya nyumba iwe kwa jina lake - SI KWELI
- Jane aliweza kutengeneza hati sababu kiwanja kilikua mali yake na bwana Kweka hakutaka majina ya watoto kwenye hati bali jina lake mwenyewe, sababu aliamini nyumba ameijenga kwa jasho lake - KWELI
- Jane alirudi nyumbani kwao masaa machache kabla ya kuuawa, kuwapelekea watoto wake chakula kwa sababu walikua wameishiwa na baba wa watoto alikua safarini Moshi - KWELI
PS:
Mtoto wao mkubwa aliyempigia simu mama yake ataishi kwa uchungu maisha yake yote, akijua bila ya simu yake, mama yao angekua hai leo.
View attachment 3686846
- Kabla ya mauaji, tayari kulikua na kesi polisi na ustawi wa jamii dhidi ya bwana Kweka kuhusu ukatili wa kijinsia na kumtishia mkewe maisha - KWELI
Vyanzo vya taarifa / Sources: (Ukija kubisha na wewe ulete vyanzao vyako)
Tofauti na mambo yanayoendelea mtandaoni na watu wanavyoleta mizaha kuhusu ukatili wa kijinsia na mauaji, Jane Urassa aliuawa kwa sababu alikua tayari kuachana na mume wake na kuhakikisha mali zao walizochuma pamoja zinabaki kwa watoto wao.
Alifanya vile ambavyo wanaume wanashauri humu jukwaani kwamba, using’ang’anie mali ambayo si yako, akampisha mwanaume kwenye nyumba yao, akaacha watoto bila kuwang'ang'ania na bado akauawa kikatili.
Hitimisho:
Jane alifikia mwisho kwenye maisha ya ndoa ila Mr. Kweka hakuwa tayari kuona mwisho wa ndoa yao pekee, alitaka pia kuhakikisha ni mwisho wa maisha yake pia - kusudi lake limetimia.
R.IP Jane 💔
Tupinge Femicide / mauaji ya wanawake
Alamsiki!
Tuseme sawa usemavyo, nani alimteua kuwa msimamizi wa warithi(watoto)?Bila kumjulisha? sidhani kama hakujua, ila naamini alipingana na huo mpango wa kuweka majina ya watoto badala ya majina yao.
Vipi anasemaje huko rumande? na kama kweli ana kansa basi atakufa kwa maumivu sana, sidhani kama magereza wana funds za chemo wala radiation 😂 😂Nawazoom tu
Wanaroho mbaya sana hawa.. ni wa mkaa na risasa tu.
Jane namfananisha na binti mmoja nilimtongoza 2010 ....akanikubali ila akawa ananipiga danadana hataki nimle na wakati huo alishakula pesa yangu ndefu sana ... na bado akawa anaendelea kunichuna baadae kidogo akaniambia hajisikii kuwa na mimi nikamwambia anirudishie pesa yangu akagoma...nikaenda kwa wazazi wake ndio wakanipa kwasababu niliwatishaSWALI (hasa kwa wanaume walioreply wakiunga mkono mauaji na huyu mama kwenye nyuzi zilizopita)
- JANE ALIKOSEA NINI?
- NI NINI KIFANYIKE ILI MAUAJI NA UKATILI KAMA HUU USIENDELEE KUTOKEA?
Nitakuwa nafanya hivyo, heshima lazima irudi mahala pake.Uniite tuje tule nao sahani moja 😂
Hili nalo neno, watoto wanaweza kujiamulia watakavyotaka wao na wazazi mliotafuta msiwe na usemi.Kuna mahali nimesikia wakisema kuweka hati majina ya watoto kuna risks zake pia, watoto wakiwa watu wazima hiyo ni mali yao kisheria, wakiamua kuuza hata kama wazazi wapo hai wanaweza kisheria.(unajua tena watoto wa kizazi hiki)
💯 📌Kila kitu kinatakiwa kuwa well calculated kwenye haya maisha.
💯Hapa Mnajadili umbea tu wahusika ndio wanajua kilichowakosanisha