Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi đź’”

Ukweli kuhusu Jane Urassa - mke aliyeuawa kwa risasi đź’”

Ila Kweka.! Nashauri kabla ya kuhusiana na mtu angalia jinsi anavyowatendea watu wengine.

Kuna watu hawatoi heshima kwa wazazi wao, ndugu na jamii inayowazunguka.
Wamejawa viburi na majivuno.

Sasa mtu kama huyu asiyejali kuhusu wazazi wake, vipi awaze kuhusu wewe.

Tukifatilia uhusiano wa Kweka na wazazi wake, kazini, majirani utakuta tu alikua mtu wa matatizo.

Ukatili wa hali ya juu kumuua mama watoto wako.
Kasome Uzi wa Robert Heriel Mtibeli msiwe na Vichwa kama vya panzi
 
Yote ya yote hata kama siamini ulichokiandika Aunt,ukweli ni kwamba jamaa alikosea kumuua mzazi mwenzake kisa mali.

Nje ya hayo mbona matukio yapo mengi na wanajamiiforums wengi wanapitia.

Ni vile wengi tunacomment kwa sifa na ni bongo zilizolala.
 
Kwamba upande wa aliyeua nao unatetewa?
Ndio lazima tutetee.

Kweka mpaka kufikia hatua ya kuua, lazima kuna kitu.

Na huwezi kuita taarifa za upande wa Jane facts bila kusikiliza taarifa za upande wa Kweka.

Taarifa za pande zote mbili lazima zisikilizwe kisha zilinganishwe kubaini ukweli ni upi.

Kwa sababu hapa kila ndugu atatetea upande wa ndugu yao.
 
Pengine aliamini nyumba isingejengwa. Tena ukute na alishaanza kuumwa.
Ila mie naona Jane angeacha hiyo hati isome majina ya kweka &Family, hadi huyo mtoto akifikisha 18yrs ndipo wabadilishe, km aliona kuna ishara za mume kuuza, basi angeenda hata mahakamani ili sheria na kanuni zifuatwe.
 
Unapotaka kubadlisha majina ya umiliki WA mali ni busara mkakubaliana usijifanye wewe ndo unawapenda sana watoto
Kuna hoja ya kupekua sana simu ya marehemu , Kuna harufu ya usaliti ndani yake.
Muhimu Kwa wanaume. Hasira ni hasara . Kuna maisha bila huyo
Mwisho. Mungu atamhukumu Kila mtu Kadili ya makosa yake
 
Hapo kwenye hoja ya 3,kwanza hakuna kitu kinaitwa hati ya nyumba ni hati ya kiwanja kama kweli kilikua cha jane maanake na document za kiwanja zingekua kwenye jina la jane sasa ilikuaje abadilishe kitu ambacho tayari kipo kwenye jina lake? Huoni kama kuna tatizo hapo
 
Siku hizi kuna hati ya pamoja kwa assets na mali mlizochuma pamoja

Hata hivyo kwa mujibu wa sheria, mali ambazo mke/mume alichuma kabla ya ndoa ni hiyali yake kuifanya ya pamoja ama yake pekee, japo inashauriwa itengwe na zile zilizochumwa ndoani/kwa pamoja

Hata hivyo, sioni haja ya assets hizo kuandikwa jina la baba ama Mama pekee wakati mnao watoto pamoja

Ni maoni yangu, Mali/assets ziwe zinaandikwa majina ya watoto chini ya uangalizi wa wazazi wote mume/mke

Ikitokea mkaachana/kutengana ni vyema Baba aondoke amwachie nyumba mke ili alee watoto

NB: Mtaka vyote kwa pupa, hukosa vyote ✍️
Kuna mahali nimesikia wakisema kuweka hati majina ya watoto kuna risks zake pia, watoto wakiwa watu wazima hiyo ni mali yao kisheria, wakiamua kuuza hata kama wazazi wapo hai wanaweza kisheria.(unajua tena watoto wa kizazi hiki)

Kila kitu kinatakiwa kuwa well calculated kwenye haya maisha.
 
Ila mie naona Jane angeacha hiyo hati isome majina ya kweka &Family, hadi huyo mtoto akifikisha 18yrs ndipo wabadilishe, km aliona kuna ishara za mume kuuza, basi angeenda hata mahakamani ili sheria na kanuni zifuatwe.
Alishaenda mahakamani, huyo jamaa ameletewa summons ya kuitwa akakimbilia kwao Moshi, mpaka aliporudi hiyo alfajiri kumuua.
 
Mara zote huwa nasema huku ndani, mwanaume kukosa akili ndio chanzo cha matatizo mengi kwenye ndoa sababu kuanzia kwenye uchaguzi wa mwanamke wa kuishi nae mwanaume unatakiwa kumsoma huyu mtu atakuja kubadilika au la

Hapa bwana Kweka alikosa akili tokea mwanzo kwa kukubali kujenga kwenye kiwanja cha mwanamke maana ndio makosa yalipoanzia
Ni kweli, nafikiri huo uamuzi wa kujenga kwenye kiwanja cha Jane aliujutia sana
 
Na niulize swali. kiwanja cha huyo mwanamke kilikuwa Moshi Kilimanjaro au nje ya Kilimanjaro?
 
Nadhani nilipo-bold umeelewa nilichokiandika,kama wanandoa mmekubaliana mke umenunua kiwanja then katikati ya safari mume akapata cent akaweka wazo mezani nataka ninunue kiwanja nijenge wewe mwenye miguu yako 25x25 Bunju uliyonunua chini ya 2mill ukamwambia usihangaike kuna kile kiwanja changu pale na sisi ni mwili mmoja jenga nyumba yetu ya familia......

Mumeo akajenga jumba la 100+ leo uone hana akili ukamwandikishe mwanao aged 15 chini ya usimamizi wako umemuona yeye aliyewekeza hela,akili,maarifa hana akili ya kuisimamia hiyo nyumba hadi uje kuisimamia wewe na mwanao wa miaka 15?hivi mna akili sawasawa kweli ninyi kinamama?
Sometimes risasi za vichwa ndio zina amsha akili.

Kama hii issue ya Kweka ni wake up call kwa wanandoa wengi sana.

Kila mtu yupo rada sasa!
 
Back
Top Bottom