sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Tanzania inapitia kipindi kigumu cha mpito katika dhana ya uwajibikaji unao chagizwa na ukosoaji wa serikali na malipo ya wakosoaji toka serikalini.
Ibara ya 8 ya katiba ya JMT kwa ujumla wake imetoa uhalali wa madraka ya serikali yatatokana na mamlaka ya wananchi na serikali msingi wake mkuu ni ustawi kwa wananchi wake.
Ikiwa mamlaka na madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi kwanini sasa wenye mamalaka wamekuwa wakiwashughulikia walitoa madaraka na mamlaka hayo pindi utendaji mbovu wa serikali unapojadili kwa misingi ya ukosoaji.
Hakuna asiyejua kuwa janga la Taifa kwa sasa ni deni la taifa linakuwa kwa kasi sambamba na maendeleo finyu katika miradi ya maendeleo.
Taasisi ya kwanza kuliona jambo hili ni chombo cha uwakilishi wa wenye kutoa mamlaka na madaraka ya serikali(wananchi) kwa maana ya bunge kushugulikiwa na serikali kwa kauli ya aliyekuwa Spika wa Bunge Ndugai kuwa serikali inakopa sana kiasi nchi yetu itapigwa mnada, kila mmoja anajua saga alilokutana nalo Spika Ndugai.
Wengi walishangilia anguko la Ndugai,lakini hakuna aliyetazama kwa jicho la mwewe. Maanake anguko la Spika ni anguko la bunge kushindwa kuisimamia serikali na kuishauri bila kujali aina ya kauli iliyotolewa.
Bahati mbaya sana mihimili mmoja ukafanikiwa kuudhoofisha mhimili ambao ni chombo cha wananchi,maanake nini wananchi wanaotoa mamlaka na madaraka ya serikali wamewajibishwa kwa chombo chao kusindwa kusimama imara kuhahakisha bunge lina kuwa imara kusimamia matakwa ya wananchi kwa kuishauri na kuisimamia serikali.
Bunge,chombo cha uwakilishi wa wananchi kikageuzwa party caucus ya CCM kumsulubu kiti cha Spika. Hii kitaalamu wananchi wamedhoofishwa na kuwa wanyonge sana kuhoji utendaji wa serikali
Kwa mantiki hii separation of power iko wapi katika utekelezaji misingi ya utawala bora.
Je kuna haja ya kuendelea kuwa na bunge linaloweza kushugulikiwa na serikali na kuacha adhima ya bunge iliyo ainishwa kikatiba!! Tujadili kwa maslahi mapana ya Taifa letu