Fahamu: Mara nyingi Wabunge hupeleka maoni yao binafsi bungeni badala ya maoni ya wananchi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,220
103,815
Huu ni mwendelezo wa mada zangu za kuwatambuza juu ya mizizi ya mambo ya hovyo yanayoendelea serikalini na nchi kwa ujumla.

Bunge ni Chombo cha uwakilishi wa Wananchi kama Ibara ya 62 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inavyotumika:

“Kutakuwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambalo litakuwa na sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Rais kama sehemu moja ya Bunge atatekelezza yote aliyokabidhiwa na katiba hii. Sehemu ya pili ya Bunge itakuwa ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kitakuwa na madaraka, kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii”

Kimsingi, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi. Kwa kuwa haiwezekani wananchi wote kukusanyika mahali pamoja na kufanya maamuzi muhimu katika uendeshaji wan chi, uwakilishi hauna budi kuwepo. Hii inamaanisha kwamba Wabunge wanapokuwa Bungeni hutekeleza majukumu yao kwa niaba ya wananchi.

Hii inamaanisha kuwa mbunge atawajibika kupeleka maoni ya wananchi bungeni katika namna mbalimbali.

Mbunge anaweza kupokea maoni ya wananchi katika namna mbalimbali ikiwepo mikutano ya hadhara, vikao na wadau mbalimbali ikiwepo serikali za vijiji na wilaya, au mawasilisho katika ofisi ya mbunge.

Zaidi ya yote mbunge ni mjumbe wa baraza la madiwani la Halmashauri na mjumbe wa Kamati ya Fedha. Hivyo kupitia madiwani ambao ni wawakilishi wa kata anaweza kupata maoni ya wananchi na kuyazungumzia bungeni.

Hali ni tofauti kwa bunge lenu. Mara nyingi wabunge huwasilisha maoni binafsi kadri akili zake zinavyomtuma badala ya maoni ya wananchi.

Wabunge wengi hawana muda wa kufanya mikutano kama anavyofanya Paul Makonda sasa ambayo ni fursa ya kuwasikiliza.

Zaidi ya yote Wabunge wengi hawana muda wa kuhudhuria vikao vya madiwani Halamshauri.

Jiulize swali dogo tu, baadhi ya mambo ya hovyo yaliyowahi kupitishwa pale bungeni, Je mbunge wako nani alimtuma kupitisha?

Je, kikokotoo na tozo za hovyo nani aliwahi kumtuma mbunge wako akazipitishe bungeni? Je aliwahi kuja hata kwenye kikao cha baraza la madiwani au Kamati ya Fedha akachukua maoni yao? Amewezaje kumuwakilisha watu ambao hata hawajui wanataka nini? Anawawakilisha au anajiwakilisha?

Haya mambo anayoibua Paul Makonda ndio namna ambayo wabunge wetu walipaswa kuyajua na kuyawasilisha ngazi husika na kama yasipopatiwa majibu basi yangesonga bungeni kuiwajibisha serikali. Huu ni ushahidi mwingine.

My Take
Kusubiri nchi ya maziwa na asali kwa wabunge na serikali hii ni kupoteza muda. Endelea na mambo mengine
 
Back
Top Bottom