Orodha ya Wahanga Wakuu Ukosoaji wa Awamu ya Sita

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Kwa kumbukumbu zangu tangu Rais Samia Ameingia Madarakani. Kuna watanzania ambao wamekutana na Rungu lake uso kwa uso. Baada tu ya kutumia haki zao za kikatiba kwa kusema yale waliyoamini kwamba hayakuwa sahihi kutendeka ndani ya JMT.

Chini ya utawala wa Mama, Mimi ninaweka oridha ya wale ninaowakumbuka.

1. Msanii kutoka chato almaarufu Dawa Juma mkazi wa Kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.
Huyu anatumikia kifungo cha miaka sita jela kutokana na kile ambacho serikali ilidai ni yeye kutoa wimbo ambao ulionekana kuwa na matusi kwa Rais.

2. Mkazi mmoja wa mjini Bariadi mkoani Simiyu. Levinus Katanabi,anaetumikia kifungo cha miaka saba jela, pamoja na faini ya shilingi milioni 15.kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kumkashifu Rais wa JMT.

3. Job Ndugai
Huyu ni mbunge wa Kongwa na spika mstaafu ambaye alilazimishwa kustaafu baada ya kutoa maoni kinzani kwa utawala wa Samia kuhusu kasi ya ukuaji wa deni la Taifa.Na kusema kwamba kama kasi ile ingeendelea vile na deni likaendelea kukua basi itafikia mahali tutauzwa kama taifa.
Kilichomtokea ni historia kwa sasa.

4. Humphey Polepole
Kitendo chake cha kufungua kile alichokiita Darasa la Siasa.Ba kuitumia platform ile kuwaelimisha wananchi katika masuala mbalimbali ya haki zao kikatiba. Alijikuta aliondolewa nchini kwa mgongo wa Kiteuliwa Ubalozi na mpaka sasa amesukumiwa mbali huko kisiwani Cuba. Hii ni baada ya kuondolewa Pale Malawi ambapo ilionekana bado anawafikia kwa karibu watanzania.

5. Dk, Bashiru Ally Kakurwa (Anonymous Decision)

6. Prof. Palamagamba Aidan Kabudi (Anonymous Decision)

7. Mh. William Lukuvi (Anonymous Decision).

8. Dk Wilbroad Slaa,Huyu ameondolewa hadhi ya kibalozi kwa kile kinachoonekana kama ni kutokana na harakati zake kupinga Mkataba mbovu wa DP-WORLD.

Hao ni wachache ambao mimi niwaona ki hivyo ila na nyinyi members JamiiForums mnayo nafasi ya kuongezea orodha au kutoa maoni yenu ili tu kuweka kumbukumbu sawa.

Kuna Member !
Fernando Jr amenikumbusha na imebidi kurudi na kuongezea hii muhimu kabisa.

9- Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe ambaye alifunguliwa kesi banfia ya ugaidi na kusota jela kwa takriban miezi tisa,na hatimae serikali kulazimika kumuachia kutokana na shinikizo la Watetezi wa haki ndani na nje ya nchi.

10- Advocate Boniface Mwabukusi.
Huyu pia ameponzwa na upingaji wa mkataba mbovu wa DP-WORLD.

11- Mdude Nyagali .Sambamba na Mwabukusi.Mdude pia ameponzwa na msimamo wake mkali juu ya mkataba huu mbovu wa DP-WORLD.
Pamoja na harakati zake za kuipinga serikali katika masuala mbalimbali.

Sabato Njema!
 
Kwani hapo #5-7 una maanisha nini kusema “anonymous decision”?

Kwamba hatua zilizochukuliwa dhidi yao hazifahamiki?
 
Ndio mkuu!
Yaani sio hatua bali sababu ya maamuzi dhidi yao.
 
Kwa kumbukumbu zangu tangu Rais Samia Ameingia Madarakani. Kuna watanzania ambao wamekutana na Rungu lake uso kwa uso. Baada tu ya kutumia haki zao za kikatiba kwa kusema yale waliyoamini kwamba hayakuwa sahihi kutendeka ndani ya JMT.

Chini ya utawala wa Mama, Mimi ninaweka oridha ya wale ninaowakumbuka.

1. Msanii kutoka chato almaarufu Dawa Juma mkazi wa Kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita.
Huyu anatumikia kifungo cha miaka sita jela kutokana na kile ambacho serikali ilidai ni yeye kutoa wimbo ambao ulionekana kuwa na matusi kwa Rais.

2. Mkazi mmoja wa mjini Bariadi mkoani Simiyu. Levinus Katanabi,anaetumikia kifungo cha miaka saba jela, pamoja na faini ya shilingi milioni 15.kwa kupatikana na hatia ya makosa ya kumkashifu Rais wa JMT.

3. Job Ndugai
Huyu ni mbunge wa Kongwa na spika mstaafu ambaye alilazimishwa kustaafu baada ya kutoa maoni kinzani kwa utawala wa Samia kuhusu kasi ya ukuaji wa deni la Taifa.Na kusema kwamba kama kasi ile ingeendelea vile na deni likaendelea kukua basi itafikia mahali tutauzwa kama taifa.
Kilichomtokea ni historia kwa sasa.

4. Humphey Polepole
Kitendo chake cha kufungua kile alichokiita Darasa la Siasa.Ba kuitumia platform ile kuwaelimisha wananchi katika masuala mbalimbali ya haki zao kikatiba. Alijikuta aliondolewa nchini kwa mgongo wa Kiteuliwa Ubalozi na mpaka sasa amesukumiwa mbali huko kisiwani Cuba. Hii ni baada ya kuondolewa Pale Malawi ambapo ilionekana bado anawafikia kwa karibu watanzania.

5. Dk, Bashiru Ally Kakurwa (Anonymous Decision)

6. Prof. Palamagamba Aidan Kabudi (Anonymous Decision)

7. Mh. William Lukuvi (Anonymous Decision).

8. Dk Wilbroad Slaa,Huyu ameondolewa hadhi ya kibalozi kwa kile kinachoonekana kama ni kutokana na harakati zake kupinga Mkataba mbovu wa DP-WORLD.

Hao ni wachache ambao mimi niwaona ki hivyo ila na nyinyi members JamiiForums mnayo nafasi ya kuongezea orodha au kutoa maoni yenu ili tu kuweka kumbukumbu sawa.

Kuna Member !
Fernando Jr amenikumbusha na imebidi kurudi na kuongezea hii muhimu kabisa.

9- Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe ambaye alifunguliwa kesi banfia ya ugaidi na kusota jela kwa takriban miezi tisa,na hatimae serikali kulazimika kumuachia kutokana na shinikizo la Watetezi wa haki ndani na nje ya nchi.

Sabato Njema!
Mdude Nyagali na Boniface Mwabukusi
 
Back
Top Bottom