Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ditopile Mzuzuri akamatwa kwa mauaji ya Dereva wa Daladala

sipendi kuendeleza malumbano na wewe quartz.

KAMA UNASEMA MADREVA WANAVUNJA SHERIA HATA MIMI NINAKUBALIANA NA WEWE KWA HILO TENA WANAUDHI SANA!!

SASA NI NANI WA KUWABANA HAWA MADREVA! UNANATAKA KUITETEA SERKALI KUWA INAWABANA????!!

BYE!
 
No question kuna mnaotaka kuuharibu huu mjadala, Mkuu wa polisi ambaye ndiye anahusika na yote mnayobishania at this stage Mzee Tibaigana, ameshatoa tamko rasmi, kuwa Blaza Dito, is in big trouble, ndio maana amejiuzulu mapema yeye mwenyewe,

Hizo yadi yadi na blah blah, sawa tumesikia, mana ndio lazima tuonyehse siku zote kuwa tumeeenda shule, kuna baadhi ya wananchi hapa inaonekana mnahitaji kujiunga na wanasheria wa Blaza Dito, maana tumepania kuona sheria inachukua mkondo wake kwenye hii simly put ni MURDER CASE,

......YA RC, MKUU WA MKOA WA TABORA KUMUUUA KWA BASTOLA, DEREVA WA BASI LA WALALAHOI AND A HARMLESS ONE, AN EXCUTION STYLE MBELE YA PUBLIC....

Kama kweli hizo argument zenu ni valid, basi hata kina Idd Amin, Hitler, Saddam, Rwanda Genocide, Milosevich, Taylor, na wengineo, walikuwa na sababu valid ambazo nyinyi kwa mtizamo wenu ndizo chanzo cha wao kufanya mauaji hayo waliyoyafanya, lakini wao hawana makosa kabisaaa!

You better be right, nyinyi kina Mwanahabari na wenzako, maana hiii kesi ndio the make au the break ya urais wa JK!
 
Inasemekana JK alivyorudi juzi alienda kumtembelea Dito usiku.Inasemekana kuwa aliingia kwenye chumba akiwa na watu wengine wawili,ili isianze minong'ono kuwa alikwenda kumsevu.Pia tetesi hizo zinasema kuwa hakuongea nae chochote kuhusu kesi yake,alimpa pole tu na kuongelea mambo mengine...maana nae ni mtoto wa town(mjanja),kisha akaondoka zake.
 
Zanaki, kama usemayo ni ya kweli, huu ni upindishaji mkuu wa sheria... Haijalishi kama walizungumzia kesi au la, kitendo cha JK kwenda kumtembelea kinaleta mgongano wa kimaslahi!!
 
quarz,

im sorry, (see my previous post here) my analysis/evaluation of your two posts shows you are supporting event B (i.e. Kumsupport Dito Kuua ndio ku-eliminate root of the problem?), ndio maana nikatumia neno "Contradiction", yaani you are contradicting yourself, sasa kama statement zako mwenyewe huwezi kuzielewa, usitulazimishe tuku-Ngw,
sisi ambao si wanasayansi tunajua kuwa wanasayansi kama nyinyi mkiwa na idea zinazo-contradict mka-practice matokeo huwa ni disastrous. No wonder Dito aliua kama alikuwa na washauri kama wewe!!.
 
mp5_Elian_Extraction_KIT.jpg


Tatizo ni kuwa kuna watu hawaamini kuwa mtu kama Dito anaweza kufanya kitendo cha kinyama namna hiyo!! Ni kwa sababu hiyo basi watu wanajaribu kutafuta kila jinsi ya kuelezea kitendo hicho kwa namna yoyote ile isipokuwa kukiita kwa jina lake halisi "mauaji ya kinyama"!!!

Hiyo picha hapo juu inamhusu mtoto wa Kicuba Elian Gonzalez ambaye alinyakuliwa kwa nguvu toka mikononi mwa ndugu zake huko Florida na kurudishwa kwa babake huko Cuba na maafisa wa uhamiaji. Ilipooneshwa kwenye vyombo vya habari watu wasiojua mambo ya silaha walianza kulalamika utamshikiliaje mtoto bunduki namna hiyo vipi ikifyatuka na kumlipua? Ndipo Mwanasheria Mkuu wa wakati ule Bi. Janet Reno alipotoa maelezo ambayo wale tunaojua silaha tuliyaona tulipoangalia kwa mara ya kwanza hiyo picha.

Maelezo ya Bi. Reno yalijenga hoja kuwa ukiangalia picha hiyo utaona kuwa mtoto huyo hakuwa katika hatari ya kupigwa risasi hata chembe! Kidole cha askari huyo mwenye silaha kiko nje ya kifyatushi (trigger) na hivyo kuondoe hata kuonekana kwa risasi kupigwa kwa bahati mbaya!! Hivyo basi huweki kidole kwenye kifyatushi isipokuwa umedhamiria kufyatua!!!

Kwanini Dito, kama kweli alikuwa anamtishia tu huyo kijana kidole aweke kwenye kifyatushi? Isipokuwa alikusudia kufyatua?? Hili tukio lingekuwa "ajali" kama bwana Dito angejipiga risasi yeye mwenyewe wakati akigonda dirisha la kidaladala kwa kitako cha bunduki. Ila inaonekana alikuwa anagonga kwa mtutu huku kidole kikiwa kifyatushi na bunduki imeelekezwa kwenye kichwa cha kijana Mbonde!!

Hili litamfunga mzee Dito miaka mingine, hakuna maelezo ya kuridhisha yatakayoondoa ukweli kuwa mauaji haya yalikuwa ni ya kukusudia na si bahati mbaya!!!
 
Kwanza kabisa ni furaha kubwa sana kuwaona vizito wa enzi za BCStimes yaani ile niliimiss sana, mpaka majuzi nikakutana na Mze MwanakiJiJi ndio akanishtua kuwa vizito woote wapo hapa.
Ditopile afungwe na zidumu fikira za usawa na uongozi wa kufuata sheria na kuheshimu haki za binadamu.
Na wale wanaosema yale ni mapenzi ya Mungu yaani mkishikwa nyie, Mungu hana mapenzi yale kabisa!
Wanasayansi tutatue matatizo ya maji safi, umeme nakadhalika,hapa sayansi haingii kabisa hapa ni commonsense na fikira za kawaida kabisa, Huwezi kumpasua mtu kichwa eti ulikuwa na hasira na kama tutahitaji wataalam hapa basi wanasayansi pembeni waje Malawyer waliosomea sheria kitivo pale mlimani!
Yaani Dito ndio ameenda huyo!sasa kwa style gani ataondoka ndio tuone!!
 
Salaaleh! Saint Pedro,
Umepotelea wapi? Good to see you man. And good points you are making. Wanasayansi watutatulie matatizo ya maji safi.
Hapa ni sheria tu kufuata mkondo wake.
 
Ogah said:
quarz,

im sorry, (see my previous post here) my analysis/evaluation of your two posts shows you are supporting event B (i.e. Kumsupport Dito Kuua ndio ku-eliminate root of the problem?), ndio maana nikatumia neno "Contradiction", yaani you are contradicting yourself, sasa kama statement zako mwenyewe huwezi kuzielewa, usitulazimishe tuku-Ngw,
sisi ambao si wanasayansi tunajua kuwa wanasayansi kama nyinyi mkiwa na idea zinazo-contradict mka-practice matokeo huwa ni disastrous. No wonder Dito aliua kama alikuwa na washauri kama wewe!!.

mr ogah,
i think you know that information is a fuction of interpretation,
kwa upande wangu sijaona hiyo "contradiction" katika hizo statement ulizo niquote,just the opposite ,i see you interpreting my syntax to fullfill your wishes.

For the first part of that quotation I was just trying to show that ,what happened was not a direct intention( neither of them planned anything)

In the second part then I was distancing myself with your interpretations and made may case clearly.what I mean.
To make it more clear to you, I am not diffending mr ditopile for what he did, but rather I am using this as a case study to explain my concerning on the safety of passengers in the dare s salaam city.
 
true fununu kuwa jk amemtembelea mtu wake ,zipo...alipofika pia alitaka kwenda kwa mbonde ,washauri wakamuambia kelele zitakua nyingi ...akaamu kuonyesha gesture kuwa ni all weather kwa jana kuhudhuria msiba wa mzee mmoja mfugaji wa kimasai[laibon ] ,ambapo aliwataka waache kuhamahama.
hata hivyo sina uhakika kama hakwenda usiku wa manane kimya kimya...
au pia anaweza kwenda baadaye mambo yakitulia...ila mshkaji lazima atatoka pale wadanganyika watakaposahau,,....na kina mbonde ambao wangeleta mdomo wameshatulizwa.
pia naomba wana board mueendelee kupiga kelele maana uzuri umu ndani watu wanapiga facts kwani jamaa kuona soo kwenda kwa mbonde inatokana na kelele zenu...maana upinzani wilki hii hoja yao ilikua karume,karume ..wakati kuna mambo yanayotuumiza umeme,na haki hii,,kelele hizi anaziona maana huku anapita..for sure.
 
Quarz,
mwanasayansi wewe mkali ndugu yangu. Na laukama dunia hii itatumia mifano yako kutatua KESI za mauaji sidhani kama kutakuwepo na MKOSA....Hakuna kitu chochote kinachotokea dunia hii bila root course na hakuna anayebisha isipokuwa KUUA ni kosa!..Kwa waumini wa dini ndio hao watakao kubaliana na wewe kuwa ni - Kazi ya Mungu.... That is root course kwani iliisha andikwa.
Mimi ndugu yangu naamini kabisa kuwa we are responsible for our own destiny. Mungu kesha panda mbegu za mti wa mchungwa (life) na ni jukumu letu kuutunza mti huo. Iwe kwa sayansi ama dini kinachotakiwa ni utunzaji wa mti huo, sayansi, dini na wasiokuwa na imani wote tunapishana tu jinsi ya utunzaji wa mti huo ikiwa ni pamoja na kinga zake.
Now, kama kuna mtu atavizia na kuiba mti wa mtu, ndugu yangu hakuna sayansi wala dini isipokuwa tunaangalia MOTIVE ya mkosa na sio root course inayotokana na victim...
Unachofanya wewe ni kumweka mahakamani victim badala ya the suspect.

Hiyo sheria ya kuacha umbali fulani ipo dunia nzima na bado magari hugongana. Madereva wabaya wanagonga magari wamejaa dunia nzima na ndio maana ikaitwa AJALI (accident) na zipo sheria za ku deal na watu hao. Nadhani vifo vya magari duniani vinakamata nambari za juu sana kuliko hata Ujambazi na sijawahi kusikia watu wakichukua hatua ya Dito - road rage na kuipamba kwa sayansi. Isipokuwa tunaambiwa na haohao wanasayansi kuwa road rage ni upungufu fulani ktk akili. Hivyo basi hapa root course ya janga hili ni kumtazama Dito alikuwa na matatizo gani akilini!...
 
Quarz the Scientist

It's all well and proper to defend most of the scientific methods kama zako hapo juu, but you know very well that much of what is currently accepted as fact can constantly being disproven and rewritten by new events and/or discoveries. Fikiria nje ya box kidogo tu utagundua unachoelezwa!!

Mkandara anakupa somo hapo, wakati mwingine inabidi tuwaangalie akina "Dito" ili kusolve most of our problems
 
normal_wassora-ruvu-juu4.jpg


Waziri wa Maji, Stephen Wassira (mwenye tai katikati) akipokea maelezo kutoka Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Boniface Kasiga (kulia) kuhusu kupungua kwa kina cha maji katika chanzo cha maji cha Ruvu Juu, wakati alipofanya ziara ya kutembelea chanzo hicho, Mkoani Pwani jana. Kupungua kwa kina cha majikumesababisha uhaba wa maji kwa Mkoa huo na Dare s Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO, Blandina Nyoni (wa tatu kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ditopile Mzuzuri.
Date: Jan 11, 2006




normal_wassora-ruvu-juu2.jpg


Waziri wa Maji, Stephen Wassira (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Ditopile Mzuzuri (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea chanzo cha maji cha Ruvu Juu Mkoani Pwani jana, kufutia kina cha maji kushuka na kusababisha uhaba wa maji kwa Mkoa huo na Dare s Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO, Blandina Nyoni (wa pili kulia) ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Boniface Kasiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Alex kaaya.
Date: Jan 11, 2006



normal_Edward_lowassa_291.jpg


Mke wa Waziri Mkuu, mama Regina Lowassa akizungumza na Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Asila Ditopile kwenye makazi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma juzi usiku wakati Waziri Mkuu alipowaalika wakuu wa mikoa na wenyeviti wa kati za Bunge

Date: Jun 30, 2006
 
Karibu sana Pedro, ila nadhani umechelewa kidooogo, ial si sana.

Jasusi,
Nilikuwa ninaangalia pande zote za shilingi.

FD
 
Ombi la mawakili katika kesi dhidi ya Ditopile:
Viongozi wazuiwe kuwafariji wafiwa
Wadai kuhani msiba ni kama kutoa hukumu
Na Ester Bulaya
JOPO la mawakili wanaomtetea mkuu wa zamani wa mkoa, Ditopile Mzuzuri (58), katika kesi ya mauaji, limeiomba mahakama kutoa amri ya kuwakataza viongozi kwenda kuifariji familia ya Hassan Mbonde, kwa sababu kitendo hicho kinaweza kuingilia uhuru wa mahakama na kufanya haki isitendeke.
Ditopile, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, anashitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mauaji ya Mbonde, aliyekuwa dereva wa daladala. Mauaji hayo yanadaiwa kufanyika Novemba 4, mwaka huu kwenye makutano ya barabara za Kawe na Bagamoyo.
Akiwasilisha ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Michael Lugulu, anayesikiliza shauri hilo, Wakili Nimrod Mkono, ambaye ameongezeka katika jopo la mawakili na kuifanya idadi yao kuwa watano, alidai kitendo cha viongozi kutembelea familia hiyo na kutoa fedha za rambirambi kinaleta hisia mbaya katika jamii dhidi ya mteja wao, wakati kesi bado haijaanza kusikilizwa wala kutolewa uamuzi.
Akiwawakilisha mawakili wenzake, Dk. Ringo Tenga na Cuthbert Tenga waliokuwapo mahakamani, Mkono alidai wanapata wasiwasi juu ya maamuzi yatakayotolewa dhidi ya kesi hiyo.
Mkono alidai jamii tayari inakuwa imeshatoa hukumu kutokana na viongozi wazito kwenda kuhani msiba huo kwa niaba ya Serikali, hivyo kuonyesha mshitakiwa ametenda kosa hilo moja kwa moja, kabla ya hukumu kutolewa.
“Tunaweza kusema vitendo vinavyofanywa na viongozi wetu vinakwenda kinyume cha Katiba ya nchi na misingi ya sheria… inatupa hofu kuona viongozi wazito wamekwenda kutembelea familia ya marehemu.
“Alikwenda Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo, akasema amekwenda kwa niaba ya Rais kutoa pole, amekwenda Makamu wa Rais…hii inaleta picha gani katika jamii si ina maana wao wanaamini kuwa huyu mtu amefanya kosa? Sisi tunaomba upige marufuku, mteja wetu hatendewi haki, ” alisema Mkono.
Mkono aliongeza: “Wakienda kutoa pole bila magari ya vingora na mapikipiki hatutakuwa na tatizo, lakini kama wanaenda kiserikali basi waende na gerezani kumtembelea mteja wetu, isiwe ubaguzi wa upande mmoja.
“Hii kesi hata upelelezi bado, mimi sitaona ajabu nikisikia Jaji Mkuu naye amekwenda sijui na Spika naye atakwenda au hata wewe mheshimiwa unaweza kwenda, kwa kweli inatupa hofu, hii kesi ipo mahakamani tunaomba waiachie mahakama.
“Kama wanataka basi waende kwa siri kuliko hali ilivyo sasa, yaani kila anayejisikia na msaada wake anataka kwenda kutoa rambirambi, mbona kuna watu wengi wanapigwa risasi hatuoni wakipewa pole na kutembelewa kama ilivyo kwa kesi hii? Waende basi na hizo zawadi gerezani kumpa mteja wetu,” alisema Mkono.
Akijibu hoja hizo Mwendesha Mashitaka Charles Kenyela, alidai mahakama imepewa mamlaka na serikali pamoja na uhuru wa kufanya kazi na kutoa maamuzi bila ya kuingiliwa na viongozi au mtu yeyote.
“Mahakama haifanyi kazi ama kutoa maamuzi kwa ajili ya maneno ya mtaani au kwa ajili ya shinikizo, hivyo kwa mawazo yangu sidhani kama matukio hayo yataingilia utoaji maamuzi ya kesi hii,” alidai Kenyela.
Akijibu maombi ya mawakili wa Ditopile, Hakimu Lugulu alisema mahakama hiyo, haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji, hivyo hata maamuzi mengine yoyote yanayohusu kesi hiyo yataamuriwa na Mahakama Kuu. Hata hivyo, alisema malalamiko hayo yatabaki katika kumbukumbu za mahakama .
“Kama nilivyosema awali, kesi hii inasikilizwa Mahakama Kuu, hivyo hamna namna ya kuagiza hilo litendeke, lakini ninaimani viongozi wa Serikali watakuwa wamesikia na waandishi wa habari watakuwa wamesikia, lakini pia malalamiko haya yote nimeyanoti kwenye kumbukumbu ya mahakama,” alisema Hakimu Lugulu.
Ditopile aliyepandishwa kizimbani mara ya kwanza Novemba 6, mwaka huu na kusomewa shitaka la mauaji ya Mbonde (33), jana akiwa kizimbani alionekana mwenye simanzi muda wote, akiwa amejishika tama na kuinamisha kichwa chini.
Kesi hiyo tofauti na zingine za mauaji, imevuta hisia za watu wengi ambao jana walijaa mahakamani. Itatajwa tena Desemba 4, mwaka huu.

Chanzo: Gazeti la Uhuru, Jumanne 21, Novemba 2006
 
Back
Top Bottom