Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Marekani kwa mind set hizi zetu za kibongo inabidi mtu ujipange sana, Kuna watanzania wanaishi kule maisha ya kuunga unga magumu hayatamaniki
Bora mliojitolea kuwa wakweli

Wengi waliopo huko anapotokea mtu wa kutusanua kama wewe wanawaka sana sijui wanahisi wanadhalilishwa sababu tulioko huku tunaamini wako poa au walipogundua walichofuata sicho walichokikuta wanataka wengi tujitose motoni
 
Usije USA na visitor visa.. Visitor visa mbaya sana. Utateseka hadi utajuta kwa nini uliondoka Tz.
Njoo na student visa.. itakusaidia utapata kazi. Utaomba tu TIN (SSN) na ID Card ya state. Then unapiga kazi wakati unafanya process za green card kupitia mke mmarekani au kampuni iliokupa kazi.
Mke au mme lakini uwe makini sababu akinusa foul.. haupati milele...
Ukiingia kwa ndoa.. unatakiwa ukae miaka miwili ndio unapewa green card isiyo na limitations. Mara nyingi kabla ya 2 years. Mmarekani anaona hapana.. anakuvurugia na haupati green card kabisa. Ndio hilo tu la kuwa makini.
Utumwa huo, mpaka uoe mmarekani ndio upewe green card? Wamarekani hao watata? Na ukitaka kurudi bongo unaacha watoto wako huko? Hapan
 
Wanalipa kuanzia $100 kwa saa na kuendelea.. unaweza piga masaa hata 80 kwa wiki ukitaka.. manake ukiamua unaweza pata $8000 kwa wiki. Wakitoa taxes.. unabakiwa na $6000 mfukoni sawa na karibia 14 million tshs. Binafsi nina investment programs nyingine, kwa hio sifanyi kazi hivyo. Lakini $12000 to $15000 per month unaipata kirahisi sana tu pia as a travel RN.
Muongo muongo sana wewe
 
Habari zenu wana jamvi. Mimi naomba nichepuke kidogo nje ya mada. Natamani kwenda vacay U.S/ U.K / Canada. Ni familia yenye 4 kids. Swali langu ni njia gani rahisi naweza kuitumia kufika mojawapo kati ya nchi hizo nikimaanisha unafuu wa gharama. Je naweza kwenda tu na nikajitembeza mwenyewe au ni lazima niwe na mwenyeji au nitumie makampuni? Naombeni gharama makadirio ya gharama za maisha kwa mwezi mmoja kwa kila nchi tajwa hapo juu kuanzia cheap return tickets, malazi, chakula na mizunguko.
NB: Lengo sio kuzamia, kipato changu ni cha uhakika na kinaniruhusu kwenda kuosha macho mbele na kurudi home. Natanguliza shukrani!
Inawezekana kabisa, nawafahamu Watanzania waliofanya hivyo, ila lazima uwe na pesa na uwe umepanga ni sehemu gani unataka kwenda. Njia rahisi ya pia ni kualikwa na mtu huku. Tuna shughuli fulani ya kifamilia hapa Marekani, baadhi ya jamaa zangu Tanzania walitaka kuja US kufungua macho, wanne wamepata visa, mmoja kanyimwa.Wenine wako kwenye process.

Gharama na makadirio ni ngumu kukupa, inategemea hasa utalii wako unataka kufanya wapi, lakini naamini ukiingia mitandaoni utapata. US ni mojawapo ya nchi inapokea watalii wengi duniani.
 
Inawezekana kabisa, nawafahamu Watanzania waliofanya hivyo, ila lazima uwe na pesa na uwe umepanga ni sehemu gani unataka kwenda. Njia rahisi ya pia ni kualikwa na mtu huku. Tuna shughuli fulani ya kifamilia hapa Marekani, baadhi ya jamaa zangu Tanzania walitaka kuja US kufungua macho, wanne wamepata visa, mmoja kanyimwa.Wenine wako kwenye process.

Gharama na makadirio ni ngumu kukupa, inategemea hasa utalii wako unataka kufanya wapi, lakini naamini ukiingia mitandaoni utapata. US ni mojawapo ya nchi inapokea watalii wengi duniani.
Asante sana 🙏
 
Inawezekana kabisa, nawafahamu Watanzania waliofanya hivyo, ila lazima uwe na pesa na uwe umepanga ni sehemu gani unataka kwenda. Njia rahisi ya pia ni kualikwa na mtu huku. Tuna shughuli fulani ya kifamilia hapa Marekani, baadhi ya jamaa zangu Tanzania walitaka kuja US kufungua macho, wanne wamepata visa, mmoja kanyimwa.Wenine wako kwenye process.

Gharama na makadirio ni ngumu kukupa, inategemea hasa utalii wako unataka kufanya wapi, lakini naamini ukiingia mitandaoni utapata. US ni mojawapo ya nchi inapokea watalii wengi duniani.

Upo jimbo gani mkuu?
 
Miaka flani Niko bongo sielewi mambo hayaeleweki, nina sista angu yuko U.S nkaongea nae kuhusu mi kwenda Marekani kujaribu maisha anakubali, mipango inakamilika kijana nkatua Jackson heartsfield Atlanta lengo kubwa la kwenda Marekani ni kupata exposure na kutafuta maisha.

Harakati zinazofuata ni mim kutafuta kazi, Marekani kazi zipo Ila sasa kule ukisikia kazin kazini kweli full supervision unafanya kazi masaa 10 mpaka 12 hiyo ni uongeze kipato ukizingatia kazi zenyenyewe unalipwa kwa masaa, kwa hiyo lazima ukomaee Ila kazi tu zipo, baada ya mda kudunduliza ela nahama kwenye basement nikahamia kwenye chumba kimoja sehemu moja hivi inaitwa sandy springs.

Tatizo la Marekani maisha expensive kipato cha kawaida ukizingatia nilienda kama mtu wa Kawaida, kila kitu ni ela yaan ukisikia capitalism kule ndo inakua practice 💯 swala la kuwa na depression, loneliness ni moja ya vitu lazima ukumbane navyo usipokua makini lazima uingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya.

Ukikaa Marekani kitu unachoombea kila siku ni usiumwe sababu ni balaa, kuhusu starehe nayo pia ni mtihan kwa mtu mwenye kipato cha kawaida, wanawake wengi wa Atlanta ni materials things inabidi kuwapata ni gharama wako after money.

Kwa sasa hivi nilisharudi tz sababu za kifamili, na maisha ya marekani ili yakuendee vizuri uwe na professional means at least umesomea master kule kama hujasoma bachelor kwenye fani za science, au unakipaji kitu ambacho kwa watanzania wengi mpaka wanakua hawajui vipaji vyao, kwenda marekani hivi hivi ni kugumu sana kwa sababu kwa maisha utajikuta unapata ela ya kawaida alafu unaishi kwa mawazo sana in short unataka kwenda marekani kutafuta maisha jipange na uwe mtu wa kujiongeza sana, na uwe competent hivi hivi sikushauri hata kidogo.

California, new York, Illinois, Massachusetts, na Washington state hayo ni majimbo ya kuyaepuka Kodi na gharama za maisha ziko juu. Ila Texas, Florida, Georgia, na north Carolina haya majimbo maisha yako cheap.

Vitu nilivuomiss marekani ni exposure Ila mwaka huu ntarudi nikiwa nimejipanga zaidi, kunakikampuni ntaenda kukifungua deleware kama domestic company, alafu baadae Virginia na Texas kama foreign company.
Vipi fursa za kusoma hapo Marekani??
 
Shida sio njaa ya mafanikio. Shida siwezi kuishi kwenye utamaduni wa design hiyo ya Marekani. Maisha sio kutafuta pesa tu.

Kuna mdau huko juu kasema, ukiwa unasaka maisha huko hata ukipata mtoto ni tabu nyingine umejiletea. Kwa mimi hiyo naona ni mateso tupu

Nchi huwezi kupiga story hata na jirani kila mtu bussy na mambo yake, hapohapo hata mtoto kuzaa ni kwa mahesabu makali aisee! Mimi loniless ingeniua. Nendeni mnaoweza sie hapahapa kwa Nyerere panatutosha, tena ukiwa na hela hapa bongo mbona tambarare tu.
Kweli mkuu, maisha sio pesa tu ukweli ni kwamba raia wengi wa mbele hasa wamarekani wanaishi kwa msongo

Ndio maana ukikutana nao huku njiani wanatembea wameinamisha kichwa
 
Sio kweli kwenye maendeleo marekani iko mbali sana hasa kwenye technologies ndo wanaongoza, alafu usalama ni mdogo kama utaishi yale maeneo ambayo ni ghetto mfano bankhead, au east point Ila kwa sandy springs, Buckhead, Alpharetta hakuna ghetto ni sehemu moja amaizing za kinyamwezi vibaya mno moja ya vitu navyomiss ni Ile apartment yangu niliyokua naishi sandy springs

Kazi ndo zipo kama zote ndo maana ni ngumu kusikia watu wakilalamika swala la ajira kama huku kwetu Africa kinacholalamiliwa ni maslai madogo lakin sio kazi hamna
Wale homeless people wanatokeaje ikiwa kazi ni bwerere?
 
Mada ya mawazo ya Ujamaa wa zamani na leo mada ni nyingine! Sitaenda huko, Hebu nijibu aya yako ya mwisho.

1. Nimesaidia baadhi ya Vijana waliokwama na Tanzania ambao wameingia US nilioweza kufahamiana nao , si wengi, na wanafanya vizuri US through my guidance + juhudi zao wenyewe naona wanatoka kimaisha! Kule kukata tamaa ambao ndio wimbo waliokuwa nao bongo haupo tena.

2. Nimesadia baadhi wanafunzi walikokwama na ada kusoma US, Kijana mmoja nilimsadia Tution fee ya semester nzima, asije toka nje ya status

3.Kwa kijana aliyemaliza chuo Tanzania Akakwama kabisa hakuna mlango ulio wazi mbele yake, namshauri kama anaweza ajaribu US, nawafahamu vijana waliofanya hivyo! Si njia nyepesi but is worth trying, kuliko kulia kulia huna connections au huna mtaji!

4.Nimeshauri watu wacheze Greencard kujaribu bahati zao! Miaka miwili iliyopita jaam yangu mmoja alifanikiwa, nilimsadia process zote hapa anaendelea na maisha yake vizuri.

5. Nimewasadia baadhi ya vijana kama watatu hivi, waliokuja kusoma US na kutaka kuzamia pasipo plan yoyote warudi Bongo! Kuna binti mmoja niliwatafuta hata wazazi wake bongo wamshauri binti yao arudi nyumbani! Hiyo degree yake aliyosoma ina soko nyumbani, sio US alifanya hivyo, na mpaka kesho ananinishukuru.

Huo ndio mchango wangu ndugu Masdinero! Hebu na wewe toa ushauri kwa kijana ambaye kashindwa kabisa Tanzania, yaani mlango umefungwa! Kakosa ajira, hana mtaji, wala connection.Umeeleza baadhi ya nchi kama 30 ambazo ni bora kuishi na kuingia kuliko US, zitaje nchi hizo basi angalau ziwasaidie vijana waliokwama bongo wanaotaka kujaribu nje.
Hapigwi kweli mtu hapa?[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom