Kuna dada alileta uzi akasema nyie mnaoenda marekan eti kule maisha ni magumu sana mwisho wa siku huwa mnarudi hamna kitu zaid ya kuleta stori za mayami na majina ya airport, wengine mnarudi mmevaa viatu aina mbili tofaut kila mguu na kiatu chake
Mkifika mnakuta mlio waacha wamepiga hatua fulan kimaisha mnaanza kudata na wengne wanaamua warud huko huko wakafe na aibu zao
Mi nilibisha sana lakin sijui Kama ni kweli
Nadhani huyo dada alikua biased, au hakutoa picha kamili. Niko Marekani kwa kama miaka 12 sasa, nimeona Watanzania walifiofika mbali sana, na wengime mambo yakiwaenda kinyume na matarajio yao, hali hiyo hata wangebaki Tanzania ingekua hivyo hivyo, safari ya maisha kwa kila mtu huleta matokeo tofauti.
Labda nikupe mtazamo wangu kuhusu maisha ya Marekani ambayo ni tofauti na ya kwetu Tanzania kwa karibu kila kitu.
1.Maisha ya Marekani hasa ya hii miaka ya karibuni bila kibali halali cha kuishi Marekani ni tabu tupu, na maaninisha ukiwa na Green Card, Green Card inakuwezesha kufanya kazi, na ukifanya yoyote ile itakuwezesha kuyakidhi maisha yako, kumbuka hata Marekani ina watu wa kawaida kama nchi yoyote ulimwenguni.Kazi ya chini Marekani isiyotaka ujuzi wowote ule itakupa maisha ambayo kazi ya chini Tanzania haiwezi kukupatia. Hutaishi maisha ya kujitanua sana lakini utaishi comfortably.
2. Green Card itakupa nafasi kutokana na uwezo wako au ndoto zako kwenda shule, ukweli ni kwamba mfumo wa Marekani hautambui kabisa vyeti kutoka nchi nyingine nyingi! Inabidi vyeti vyako uvifanyie certification au uanze upya! Hii ni njia rahisi kabisa kubadili maisha yako! Kupata mkopo wa masomo ni kitu rahisi sana, na schorlaships. Kitu kinacho washinda wengi ni kusoma na kufanya kazi, Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana ambayo wengi wa Watanzania hawana.
3. Mfumo wa Marekani hauna ujanja ujanja, bills kama za umeme, maji, simu bima za magari hulipwa kwa wakati unaotakiwa, kuchelewesha kulipa kwa wakati unaotakiwa unaingia kwenye records na unavuruga kabisa historia yako.Hivyo nidhamu yako ya matumizi ya pesa inatakiwa iwe ya hali ya juu mno, wengi wabongo huwa inawashinda.
4.Jambo kubwa nililojifunza kwa miaka yangu kumi na mbili Marekani ni kuwa hawa jamaa wanafanya kazi! Nafanya kazi kiwandani ( Mtaniita mbeba mabox) Lakini kwa kazi hii nimeninunua nyumba Marekani ( midle class area) na kufanya mambo ya msingi Tanzania. Hakuna uvivu au longololo, na yote utakayosema mabaya kuhusu wamarekani, lakini kama kuna kitu nimejifunza hawa jamaa wanafanya kazi, na wakipumzika wanakula maisha.
5. Maisha ya Marekani ni ya kila mtu kuangalia maisha yake, ni nzuri sana na mbaya sana, hasa kwa watu toka Bongo, mtu haangalii umevaa nini, unaendesha gari, unaiishije. Majirani zangu siwajui kabisa, huwa tunapungiana mikono tunapoingia ndani ya magari kwenda kwenye shughuli zako! Hii imenifanya nichukie Bima ya ya kunizika mimi na mke wangu, sitegemei bakuli/Mchango wa mtu yoyote. Hali hii inafanya ukomae na maisha ki kweli kweli.
6. Jambo jingine ambalo litakushangaza kuhusu Marekani ni kuwa nchi imevuta watu kutoka kila nchi, kwa kifupi na ubaya wote unaosikia kuhusu Marekani, bado imebakia ni kimbilio la wengi! Matajiri na maskini! Wenye pesa kutoka China, Ulaya, India, Korea Uarabuni wanakuja kuwekeza, na maskini kama sisi tunakuja kutafuta! Nimefanya kazi na watu toka Brazil, Afghanistan, Japan, UK nk Kila mtu ana sababu zake za kuja Marekani. Na mfumo wa elimu yao bado unavuta watu wa mataifa mengi.
Angalizo! Uje Marekani ukiwa na malengo maalumu, maisha ni popote pale, unaweza kupata unachotaka hata hapo Tanzania.