Ukitaka kwenda kuishi Marekani inabidi ujipange

Nilipata green card kwa kucheza DV lottery nikiwa Tanzania nafanya kazi. So sikupata challenge sana, nilifika nikapata SSN na sikuchelewa kupata kazi. Nilikuja na familia na watoto wote walipata kila karatasi na kuanza shule! Wanamaliza high school sasa niliokuja nao!
DV lottery Ni nin
 
Nadhani huyo dada alikua biased, au hakutoa picha kamili. Niko Marekani kwa kama miaka 12 sasa, nimeona Watanzania walifiofika mbali sana, na wengime mambo yakiwaenda kinyume na matarajio yao, hali hiyo hata wangebaki Tanzania ingekua hivyo hivyo, safari ya maisha kwa kila mtu huleta matokeo tofauti.
Labda nikupe mtazamo wangu kuhusu maisha ya Marekani ambayo ni tofauti na ya kwetu Tanzania kwa karibu kila kitu.
1.Maisha ya Marekani hasa ya hii miaka ya karibuni bila kibali halali cha kuishi Marekani ni tabu tupu, na maaninisha ukiwa na Green Card, Green Card inakuwezesha kufanya kazi, na ukifanya yoyote ile itakuwezesha kuyakidhi maisha yako, kumbuka hata Marekani ina watu wa kawaida kama nchi yoyote ulimwenguni.Kazi ya chini Marekani isiyotaka ujuzi wowote ule itakupa maisha ambayo kazi ya chini Tanzania haiwezi kukupatia. Hutaishi maisha ya kujitanua sana lakini utaishi comfortably.

2. Green Card itakupa nafasi kutokana na uwezo wako au ndoto zako kwenda shule, ukweli ni kwamba mfumo wa Marekani hautambui kabisa vyeti kutoka nchi nyingine nyingi! Inabidi vyeti vyako uvifanyie certification au uanze upya! Hii ni njia rahisi kabisa kubadili maisha yako! Kupata mkopo wa masomo ni kitu rahisi sana, na schorlaships. Kitu kinacho washinda wengi ni kusoma na kufanya kazi, Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana ambayo wengi wa Watanzania hawana.

3. Mfumo wa Marekani hauna ujanja ujanja, bills kama za umeme, maji, simu bima za magari hulipwa kwa wakati unaotakiwa, kuchelewesha kulipa kwa wakati unaotakiwa unaingia kwenye records na unavuruga kabisa historia yako.Hivyo nidhamu yako ya matumizi ya pesa inatakiwa iwe ya hali ya juu mno, wengi wabongo huwa inawashinda.

4.Jambo kubwa nililojifunza kwa miaka yangu kumi na mbili Marekani ni kuwa hawa jamaa wanafanya kazi! Nafanya kazi kiwandani ( Mtaniita mbeba mabox) Lakini kwa kazi hii nimeninunua nyumba Marekani ( midle class area) na kufanya mambo ya msingi Tanzania. Hakuna uvivu au longololo, na yote utakayosema mabaya kuhusu wamarekani, lakini kama kuna kitu nimejifunza hawa jamaa wanafanya kazi, na wakipumzika wanakula maisha.

5. Maisha ya Marekani ni ya kila mtu kuangalia maisha yake, ni nzuri sana na mbaya sana, hasa kwa watu toka Bongo, mtu haangalii umevaa nini, unaendesha gari, unaiishije. Majirani zangu siwajui kabisa, huwa tunapungiana mikono tunapoingia ndani ya magari kwenda kwenye shughuli zako! Hii imenifanya nichukie Bima ya ya kunizika mimi na mke wangu, sitegemei bakuli/Mchango wa mtu yoyote. Hali hii inafanya ukomae na maisha ki kweli kweli.

6. Jambo jingine ambalo litakushangaza kuhusu Marekani ni kuwa nchi imevuta watu kutoka kila nchi, kwa kifupi na ubaya wote unaosikia kuhusu Marekani, bado imebakia ni kimbilio la wengi! Matajiri na maskini! Wenye pesa kutoka China, Ulaya, India, Korea Uarabuni wanakuja kuwekeza, na maskini kama sisi tunakuja kutafuta! Nimefanya kazi na watu toka Brazil, Afghanistan, Japan, UK nk Kila mtu ana sababu zake za kuja Marekani. Na mfumo wa elimu yao bado unavuta watu wa mataifa mengi.

Angalizo! Uje Marekani ukiwa na malengo maalumu, maisha ni popote pale, unaweza kupata unachotaka hata hapo Tanzania.
Nina chalii yangu mwaka jana mwezi wa 9 kapiga chini kazi ya serekali Tz baada ya kufanya kazi miaka kama mi 5 kama utani utani tu jamaa aliacha kazi kaenda zake USA ila alikua na connection kuna ndugu yake alimuita huko mwana sahiv huwa namchungulia kwa Fb tu kwel hata picha anazopiga haina haja ya ku tag location unajua tu huyu yuko mbele

Akikaza naamini atatoboa na mimi namuombea atoboe maana alifanya maamuzi magum sana ambayo watu wengi walioko huko serekalini hawawez kufanya wamerizika na mshahara wa Tsh700k
 
Wafanyakazi wa McDonalds na Walmart wamepata fursa kujisifu wanaishi Marekani.

Wanaume wazima wameamua kusomea unesi maana kila kona wamebanwa hawapati kazi. Their feminine side ultimately takes control of their lives out of a sheer desperation to survive in a iredeemiably racist, capitalist society.

Hao wanaume wangekuwa TZ wasingefikiria hiyo kazi ya kike hata siku moko.

Dume zima anajisifia yeye registered nurse?!!

Boss, nilitaka kukupuuza lakini nimeona sintowatendea haki vijana walioanzisha huu uzi na kutaka kujua mambo! Ujuzi unapoupata uwe unakufaa au haukufai tayari ni wako kama utautumia is up to you!

Mzee kwanza unaonekana una makasiriko sana, nikushauri kitu, ukiona uzi haupo kwenye interest zako achana nao, dunia hii mzee ina mambo mengi sana kama ilivyo JamiiForums, ina nyuzi za kutosha nenda kasome na na kuchangia za kiume. Mzee kazi za kiume ni zipi? Unaonekana umepitwa sana na wakati, ni uhasibu, uhandisi, ujenzi, uchimbaji wa madini, uanajeshi, mgambo au ni nini unamaanisha? Najua kazi pekee inayoweza kufanywa na mwanaume tu ni kutom... Zingine zote duniani hazina jinsia kila mtu anafanya, ndio maana Rais ni mwanamke au hiyo nayo ya kike?. Una haki ya kuchagua chochote ufanye ila uwe na adabu kwa mambo yasiyokuhusu. Kama hayakupendezi unapita tu kushoto.

Hiyo unayosema kazi ya kike mwaka jana imenipa $195,000 na tax refund $45,000 wewe yako ya kiume imekupa ngapi? Yani nipo sawa na vyeti vyangu vingine vimekaa vinachakaa. Wanangu hapa baada ya graduation wakiamua kurudi Tz watashindana na watoto wa Lowasa na wa ngazi hizo. Sio hao 60,000 plus wanaokwenda kudhalilishwa Mkapa stadium kugombea nafasi 1000 za TRA. Akija anakuja kuchukua senior position popote ndani na mfumobongo bila shaka. Yani mwanao na mwanangu wa kike hawatakaa waonane popote au na wewe. Usidharau usivyovijua wakati huna cha kuonyesha na hata hivyo kama umefanikiwa sana na kazi za kiume why kuhangaika na wengine? Fanya yako dunia kubwa hii, kila mtu angekuwa wewe si ingekuwa inaboa sana? Mmoja akilima nyanya, we lima bamia mkivuna wote mnapata mchuzi!!!

Hamna kati yetu aliyeanzisha huu uzi hapa kujisifia kama unavosema, tumejibu maswali ya vijana wanaohangaika kujua kupata hali halisi na ni hiyari yao kuchukua au kuacha, uwanja mpana huu. Wabongo bana mkiuliza mkajibiwa shida, wakikaa kimya wana roho mbaya, tukoje sisi? Sorry kwa watakaokwazika.
 
Nadhani huyo dada alikua biased, au hakutoa picha kamili. Niko Marekani kwa kama miaka 12 sasa, nimeona Watanzania walifiofika mbali sana, na wengime mambo yakiwaenda kinyume na matarajio yao, hali hiyo hata wangebaki Tanzania ingekua hivyo hivyo, safari ya maisha kwa kila mtu huleta matokeo tofauti.
Labda nikupe mtazamo wangu kuhusu maisha ya Marekani ambayo ni tofauti na ya kwetu Tanzania kwa karibu kila kitu.
1.Maisha ya Marekani hasa ya hii miaka ya karibuni bila kibali halali cha kuishi Marekani ni tabu tupu, na maaninisha ukiwa na Green Card, Green Card inakuwezesha kufanya kazi, na ukifanya yoyote ile itakuwezesha kuyakidhi maisha yako, kumbuka hata Marekani ina watu wa kawaida kama nchi yoyote ulimwenguni.Kazi ya chini Marekani isiyotaka ujuzi wowote ule itakupa maisha ambayo kazi ya chini Tanzania haiwezi kukupatia. Hutaishi maisha ya kujitanua sana lakini utaishi comfortably.

2. Green Card itakupa nafasi kutokana na uwezo wako au ndoto zako kwenda shule, ukweli ni kwamba mfumo wa Marekani hautambui kabisa vyeti kutoka nchi nyingine nyingi! Inabidi vyeti vyako uvifanyie certification au uanze upya! Hii ni njia rahisi kabisa kubadili maisha yako! Kupata mkopo wa masomo ni kitu rahisi sana, na schorlaships. Kitu kinacho washinda wengi ni kusoma na kufanya kazi, Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana ambayo wengi wa Watanzania hawana.

3. Mfumo wa Marekani hauna ujanja ujanja, bills kama za umeme, maji, simu bima za magari hulipwa kwa wakati unaotakiwa, kuchelewesha kulipa kwa wakati unaotakiwa unaingia kwenye records na unavuruga kabisa historia yako.Hivyo nidhamu yako ya matumizi ya pesa inatakiwa iwe ya hali ya juu mno, wengi wabongo huwa inawashinda.

4.Jambo kubwa nililojifunza kwa miaka yangu kumi na mbili Marekani ni kuwa hawa jamaa wanafanya kazi! Nafanya kazi kiwandani ( Mtaniita mbeba mabox) Lakini kwa kazi hii nimeninunua nyumba Marekani ( midle class area) na kufanya mambo ya msingi Tanzania. Hakuna uvivu au longololo, na yote utakayosema mabaya kuhusu wamarekani, lakini kama kuna kitu nimejifunza hawa jamaa wanafanya kazi, na wakipumzika wanakula maisha.

5. Maisha ya Marekani ni ya kila mtu kuangalia maisha yake, ni nzuri sana na mbaya sana, hasa kwa watu toka Bongo, mtu haangalii umevaa nini, unaendesha gari, unaiishije. Majirani zangu siwajui kabisa, huwa tunapungiana mikono tunapoingia ndani ya magari kwenda kwenye shughuli zako! Hii imenifanya nichukie Bima ya ya kunizika mimi na mke wangu, sitegemei bakuli/Mchango wa mtu yoyote. Hali hii inafanya ukomae na maisha ki kweli kweli.

6. Jambo jingine ambalo litakushangaza kuhusu Marekani ni kuwa nchi imevuta watu kutoka kila nchi, kwa kifupi na ubaya wote unaosikia kuhusu Marekani, bado imebakia ni kimbilio la wengi! Matajiri na maskini! Wenye pesa kutoka China, Ulaya, India, Korea Uarabuni wanakuja kuwekeza, na maskini kama sisi tunakuja kutafuta! Nimefanya kazi na watu toka Brazil, Afghanistan, Japan, UK nk Kila mtu ana sababu zake za kuja Marekani. Na mfumo wa elimu yao bado unavuta watu wa mataifa mengi.

Angalizo! Uje Marekani ukiwa na malengo maalumu, maisha ni popote pale, unaweza kupata unachotaka hata hapo Tanzania.
Ndo maana nikasema kama mtu una bachelor degree kutoka Tanzania ukiweza kusomea masters kule inakua ni vizuri zaid
 
Boss, nilitaka kukupuuza lakini nimeona sintowatendea haki vijana walioanzisha huu uzi na kutaka kujua mambo! Ujuzi unapoupata uwe unakufaa au haukufai tayari ni wako kama utautumia is up to you!

Mzee kwanza unaonekana una makasiriko sana, nikushauri kitu, ukiona uzi haupo kwenye interest zako achana nao, dunia hii mzee ina mambo mengi sana kama ilivyo JamiiForums, ina nyuzi za kutosha nenda kasome na na kuchangia za kiume. Mzee kazi za kiume ni zipi? Unaonekana umepitwa sana na wakati, ni uhasibu, uhandisi, ujenzi, uchimbaji wa madini, uanajeshi, mgambo au ni nini unamaanisha? Najua kazi pekee inayoweza kufanywa na mwanaume tu ni kutom... Zingine zote duniani hazina jinsia kila mtu anafanya, ndio maana Rais ni mwanamke au hiyo nayo ya kike?. Una haki ya kuchagua chochote ufanye ila uwe na adabu kwa mambo yasiyokuhusu. Kama hayakupendezi unapita tu kushoto.

Hiyo unayosema kazi ya kike mwaka jana imenipa $195,000 na tax refund $45,000 wewe yako ya kiume imekupa ngapi? Yani nipo sawa na vyeti vyangu vingine vimekaa vinachakaa. Wanangu hapa baada ya graduation wakiamua kurudi Tz watashindana na watoto wa Lowasa na wa ngazi hizo. Sio hao 60,000 plus wanaokwenda kudhalilishwa Mkapa stadium kugombea nafasi 1000 za TRA. Akija anakuja kuchukua senior position popote ndani na mfumobongo bila shaka. Yani mwanao na mwanangu wa kike hawatakaa waonane popote au na wewe. Usidharau usivyovijua wakati huna cha kuonyesha na hata hivyo kama umefanikiwa sana na kazi za kiume why kuhangaika na wengine? Fanya yako dunia kubwa hii, kila mtu angekuwa wewe si ingekuwa inaboa sana? Mmoja akilima nyanya, we lima bamia mkivuna wote mnapata mchuzi!!!

Hamna kati yetu aliyeanzisha uzi hapa, tumejibu maswali ya vijana wanaohangaika kujua kupata hali halisi na ni hiyari yao kuchukua au kuacha, uwanja mpana huu. Sorry kwa watakaokwazika.
Jamaa ana hasira aliomba viza wakampiga chini kwenda mbele we achana nae ni ng'ombe tu huyo
 
Ni ngumu kupata kazi ya taaluma uliyosomea kama hauna experience ya kazi katka kampuni za US,

Lakini unaweza kuji3ndeleza na masters kwa hiyo Bsc yako .. kisha ukapata internship then ukapata kazi,

So kipindi chote hicho una hustle kupata kazi za taaluma yako ..hauwezi kukosa kazi za kawaida za kufanya...

Wengine wanatoka na Bachelor degree, ukifika kule unawe,a kusoma zile courses ukapata certification ikakusaidia..
Asante kwa ufafanuzi mzuri.
 
Waambie Rais na wizara yake,waweke Pay rates za mamilioni kwa manesi,kama hujaona madume yakiingia kwenye unesi hapo Tanzania
Mambo mengine ni kukariri tu, huyu jamaa anaweza kufikiri hata kazi ya upishi ni kazi ya wanawake na wanaume wanapika / chef's wanafanya kwasababu ya shida??

Miaka ya zamani duniani kote, Kabla wanawake hawajaingizwa kwenye mfumo rasmi wakuajiriwa , anafikiri hizo kazi zilikuwa zikifanywa na nani??
 
3. HAKUNA UONGO MKUBWA WATU WANAAMBIWA TZ KAMA ETI UTAUZA VINYAGO HUKU. Hakuna kitu kama hicho. Hakuna kuuza vitu barabarani au nyumba kwa nyumba. Utaenda kupiga hodi kwa mtu.. UTAFYATULIWA RISASI.
Kuna Mtanzania anauza nguo za kimasai na bangili hereni,cheni vitu vya kiasili ya Afrika huko huko Marekani alihojiwa na Maulid kitenge kwao ni Tabora alisema yeye ni machinga lakini amesajiliwa anatumia Gari anapaki sehemu pembezoni mwa barabara anauza bidhaa zake.
 
Mpishi.. unaweza.. lakini USA Hawali ugali.. na hata vyakula vyao ni tofauti sana na Africa.. kwa hip itabidi usomee upya. Na pia hawalipi vizuri sana.
Kuna mdada wa kichaga alihojiwa na Kitenge huko huko marekani anauza chakula cha kiafrika Mashariki anapika ugali,samaki,chapati Maharage ,viazi,n.k tuliona hadi wazungu wanakula ugali kaka
 
Story tu hizi kisa uliskia kuna waliofanikiwa kupata wamama wa kizungu...uhalisia ni tofauti sana na machalii wa chuga hadi walishaamua wafanye ishu zingine...sasa sembuse wa kutoka mkoani eti uende arusha utegemee utapata bibi/mama wa kizungu? Nimefanya sana kazi chuga hadi kule karatu ambapo ndio gateway ya utalii nafahamu. Na ninawashkaji ambao baba zao wanahotel za kitalii au kampuni za tours na miaka yote wanasaka wazungu wanaishia kuwagonga tu for fun napo uwe unazali na inaishia hapo tu.
Wapo waliofanikiwa wachache sana. Sema hiyo mipango ya kutafuta bibi wa kizungu ni mmojawapo ya mission za kipumbavu sana inayochangiwa na uvivu.
 
Nadhani huyo dada alikua biased, au hakutoa picha kamili. Niko Marekani kwa kama miaka 12 sasa, nimeona Watanzania walifiofika mbali sana, na wengime mambo yakiwaenda kinyume na matarajio yao, hali hiyo hata wangebaki Tanzania ingekua hivyo hivyo, safari ya maisha kwa kila mtu huleta matokeo tofauti.
Labda nikupe mtazamo wangu kuhusu maisha ya Marekani ambayo ni tofauti na ya kwetu Tanzania kwa karibu kila kitu.
1.Maisha ya Marekani hasa ya hii miaka ya karibuni bila kibali halali cha kuishi Marekani ni tabu tupu, na maaninisha ukiwa na Green Card, Green Card inakuwezesha kufanya kazi, na ukifanya yoyote ile itakuwezesha kuyakidhi maisha yako, kumbuka hata Marekani ina watu wa kawaida kama nchi yoyote ulimwenguni.Kazi ya chini Marekani isiyotaka ujuzi wowote ule itakupa maisha ambayo kazi ya chini Tanzania haiwezi kukupatia. Hutaishi maisha ya kujitanua sana lakini utaishi comfortably.

2. Green Card itakupa nafasi kutokana na uwezo wako au ndoto zako kwenda shule, ukweli ni kwamba mfumo wa Marekani hautambui kabisa vyeti kutoka nchi nyingine nyingi! Inabidi vyeti vyako uvifanyie certification au uanze upya! Hii ni njia rahisi kabisa kubadili maisha yako! Kupata mkopo wa masomo ni kitu rahisi sana, na schorlaships. Kitu kinacho washinda wengi ni kusoma na kufanya kazi, Inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana ambayo wengi wa Watanzania hawana.

3. Mfumo wa Marekani hauna ujanja ujanja, bills kama za umeme, maji, simu bima za magari hulipwa kwa wakati unaotakiwa, kuchelewesha kulipa kwa wakati unaotakiwa unaingia kwenye records na unavuruga kabisa historia yako.Hivyo nidhamu yako ya matumizi ya pesa inatakiwa iwe ya hali ya juu mno, wengi wabongo huwa inawashinda.

4.Jambo kubwa nililojifunza kwa miaka yangu kumi na mbili Marekani ni kuwa hawa jamaa wanafanya kazi! Nafanya kazi kiwandani ( Mtaniita mbeba mabox) Lakini kwa kazi hii nimeninunua nyumba Marekani ( midle class area) na kufanya mambo ya msingi Tanzania. Hakuna uvivu au longololo, na yote utakayosema mabaya kuhusu wamarekani, lakini kama kuna kitu nimejifunza hawa jamaa wanafanya kazi, na wakipumzika wanakula maisha.

5. Maisha ya Marekani ni ya kila mtu kuangalia maisha yake, ni nzuri sana na mbaya sana, hasa kwa watu toka Bongo, mtu haangalii umevaa nini, unaendesha gari, unaiishije. Majirani zangu siwajui kabisa, huwa tunapungiana mikono tunapoingia ndani ya magari kwenda kwenye shughuli zako! Hii imenifanya nichukie Bima ya ya kunizika mimi na mke wangu, sitegemei bakuli/Mchango wa mtu yoyote. Hali hii inafanya ukomae na maisha ki kweli kweli.

6. Jambo jingine ambalo litakushangaza kuhusu Marekani ni kuwa nchi imevuta watu kutoka kila nchi, kwa kifupi na ubaya wote unaosikia kuhusu Marekani, bado imebakia ni kimbilio la wengi! Matajiri na maskini! Wenye pesa kutoka China, Ulaya, India, Korea Uarabuni wanakuja kuwekeza, na maskini kama sisi tunakuja kutafuta! Nimefanya kazi na watu toka Brazil, Afghanistan, Japan, UK nk Kila mtu ana sababu zake za kuja Marekani. Na mfumo wa elimu yao bado unavuta watu wa mataifa mengi.

Angalizo! Uje Marekani ukiwa na malengo maalumu, maisha ni popote pale, unaweza kupata unachotaka hata hapo Tanzania.
Umeandika kwa weledi wa hali ya juu sana. Hongera. Hapa Tanzania kuingiza laki kwa siku inawezekana lakini inahitaji utulivu pia kama huko Marekani. Ila watu wengi TZ bado vipato vyetu viko chini kwahiyo kufikiria kuja Marekani bado ni wazo lenye uhai.
 
Nina chalii yangu mwaka jana mwezi wa 9 kapiga chini kazi ya serekali Tz baada ya kufanya kazi miaka kama mi 5 kama utani utani tu jamaa aliacha kazi kaenda zake USA ila alikua na connection kuna ndugu yake alimuita huko mwana sahiv huwa namchungulia kwa Fb tu kwel hata picha anazopiga haina haja ya ku tag location unajua tu huyu yuko mbele

Akikaza naamini atatoboa na mimi namuombea atoboe maana alifanya maamuzi magum sana ambayo watu wengi walioko huko serekalini hawawez kufanya wamerizika na mshahara wa Tsh700k
Mwanangu Rangi za picha za mbele huulizi mara mbili kitu HD,yaani kuna picha ukiziona unajua hapa sio kweusi,hata ngozi huwa na muonekano tofauti na ngozi zetu huku...mtu mweusi kwa mbele anakuwa na mg'ao flani mzuri sijui tulikosea wapi aisee!
 
Nina ndugu Marekani anaishi Ohio cleaveland -ankol
Nina dada yangu wa damu moja yuko Canada -nisaidieni mganga wa kuwapiga kizizi waniite kwa Gharama yeyote niende kupiga box,halafu aliyenisaidia nitampeleka ndugu yake mmoja au wawili....maana wanadai ni ngumu sana kupeleka mtu,ila huyu anko alimpeleka jamaa wazimbabwe akamuoe shemeji yake maana naskia kule wamarekani ni pasua kichwa kwenye ndoa bora waafrika kwa waafrika.
 
Ukitaka kujua life la state sikiliza hiphop.

Lighters up - Lil kim
Brooklyn Anthem - Foxy Brown.
Chicago - L.E.P Bogus
Welcome to ATL - J.Dupri
Welcome to Detroit - Trick ft Eminem
We built this city - Diplomat
Ghetto- Akon
 
Nina ndugu Marekani anaishi Ohio cleaveland -ankol
Nina dada yangu wa damu moja yuko Canada -nisaidieni mganga wa kuwapiga kizizi waniite kwa Gharama yeyote niende kupiga box,halafu aliyenisaidia nitampeleka ndugu yake mmoja au wawili....maana wanadai ni ngumu sana kupeleka mtu,ila huyu anko alimpeleka jamaa wazimbabwe akamuoe shemeji yake maana naskia kule wamarekani ni pasua kichwa kwenye ndoa bora waafrika kwa waafrika.
Mkuu, wala usipate taabu ya kumtafuta mganga wa kuwaroga ndugu zako ili wakuite huko majuu. Kama umesoma huu uzi wote nadhani utakuwa umejifunza kuwa mtu kuwa Ulaya, Marekani ama Canada siyo ticket ya kutoboa kimaisha. Ili uweze kutoboa kuna mambo mengi sana. Na kuna wanaotoboa na kuna ambao wanaishia kuishi maisha ya kawaida tu na kuna wengine wanaona bora warudi home.

Ni kama tu ilivyo bongo, unakuta mtu ana fursa kabisa ya mtaji mzuri hata 50M ama 100M anaanza biashara ila bado anarudi nyuma tena. Kwahiyo kuanza biashara haimanishi kuwa ndio ticket ya kutoboa. Pamoja na mipango mizuri, jitihada kwenye maisha na nidhamu ya kuishi, bado nadhani kuna kitu kinachoitwa bahati ya mtu kwenye maisha na ina play part kubwa.

Labda nikuulize, hao ndugu zako wana mda gani tangia wameenda huko majuu? Isije kuwa na wao bado wanapigana, maana huko unakuta anaishi chumba kimoja kwa kujibana sana. Sasa akisema akuite wakati mambo yake hayajakaa sawa si itakuwa shughuli nyingine?
 
Back
Top Bottom