Ukimya wa vyombo vya habari juu ya unyama wa wanajeshi dhidi ya raia huko Kawe

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Kufuatia tukio lq mauqji ya Luteni Kanali aambaye inasadikiwa alizozana na mwendesha bajaji na kupelekea ugomvi uliogharimu maisha. Imesemwa kuwa mruhumiwa ameshatiwa nguvuni akisubiri sheris kuchukua mkondo wake

kuna vurugu zinaendelea Kawe ambapo baada ya shughuli za kuaga marehemu pale Lugalo, imesemwa vurugu hizo zinafanywa na wanajeshi hususan MP ambapo wwnatembeza kichapo kwa kila raia wanayemkuta. Hawwjali jinsia wala hali.

Je, jeshi ni DPP na Mahakama wakati huo huo? Wananchi wanaopigwa wana mchango upi kwenye tukio ambalo inasemwa marehemu alilianzisha dhidi ya dereva wa bajaji?

Ni lini wananchi watqthibitishiwa amani ndani ya nchi yao?

F9d1QjtXsAEOPNV.jpeg.jpg

F9d1Q35XMAAuuyL.jpeg.jpg


picha hizi zinapatikana mtandao wa X kwa mtumiaji aitwaye Fortunatus Buyobe

Vyombo vyetu vya habari kama havipo ila wanaendekeza sana habari za udaku na ujinga wa kila namna. Hata kama imetokea hayo wengine hawahusiki na hayo wanayotendewa,hii nchi inaendeshwa kwa mjibu wa Katiba na sheria,watu waishi kwaku heshimiana ili Amani idumu.

Media House za Tanzania kwa kiwango kikubwa imekuwa ikifumbia macho matukio hasi yanayofanywa na serikali na vyombo vyake dhidi ya raia. Tumeona waandishi wengi wakipata teuzi ambazo ni kama rushwa za kisiasa.


RAI
Naliomba Jeshi (JWTZ) kutoa tamko la kurekebisha huu mtanziko unaoendelea. Jeshi linalopendwa na raia haliwezi hata mara moja likawadhuru raia.


inawezekaba likaona kuomba radhi ni kujishusha, basi likemee ama lizuie askari wake kushiriki matendo yanayoumiza ama kuwaletea raia tafran

Tunashukuru JamiiForums kutupatia jukwaa la kuzungumza kwa uwazi

Tuamke
Tuzinduke
Tuiponye Tanzania
 
Kizazi kijacho,kitakuja kutushangaa sana miaka ijayo,yaani unapigwa na mtu anayetakiwa kulinda mipaka halafu hata vyombo vya habari,sijui vinaogopa nini kuripoti hali hii?
Huu sasa ni kama utawala wa kikoloni,ni ushenzi sana unaofanyika.Inamaana Kawe nzima,wamekubali waishi kwa kuonewa,isipokua Kato tu?
Aisee,uoga mwingine ni wa kipumbavu,ni bora vurugu itokee,kuliko kuwa kondoo.Watokee wananchi ambao wanatakiwa kuonyesha kuwa hawakubaliani na hali ya unyanyasaji huo.Siyo fair kabisa.Kato kafanya kwa nafasi yake,na wengine waonyeshe protest hadi suluhu ipatikane.
 
Na mbunge, Askofu PhD yuko kama hayupo. Askofu asipokemea haya, tena kwa wapiga kura wake, uaskofu wa nii sasa!
Na huko pia ni kwake mtume Mwamposa. Naye yuko kimya anasubiri kukusanya shekeli kwa wagonjwa na may be, majeruhi wa hiyo kadhia
Askofu amehamia kwa kaisari.

Ya Mungu (haki) yamebaki kwa Mungu
 
Back
Top Bottom