Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,754
Kupitia upashanaji habari wa sisi wananchi, tumegundua kuna ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu uliofanywa na JWTZ Kambi ya Lugalo dhidi ya raia.
Siyo siri, tukio la kuuawa kwa Luteni Kanali limeacha pigo kubwa kwa familia yake, wanajeshi wenzake na serikali kupoteza asset yake muhimu.
Ukweli huo haufichi hatua ambazo jeshi la polisi wamefanya la kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji hayo.
Lakini, wananchi wanaoishi jirani na kambi ya Lugalo eneo la Kawe wamelipa gharama kubwa kupitia vipigo vikali vilivyotembezwa na wanaodaiwa ni MP kutoka Lugalo. Watu wameumizwa na inahofiwa wengine wamepoteza maisha kupitia tukio hilo
Haiwezekani, jambo kama hili linatokea nchini kwetu na mamlaka zinafumbia macho bila.kuchukua hatua hata ya kukemea vitendo vya wanajeshi kujitwalia sheria mkononi dhidi ya raia. Yapo matukio.kadhaa yanayoshabihiana na unyama wa wanajeshi dhidi ya raia. Tumeshuhudia video zikisambazwa za wanajeshi wetu wanavyowashuhhulikia raia wanaokutwa na mavao yafananayo.na jeshi ambayo mamlaka zetu za customs wametoza kodi na kuruhusu yauzwe madukani. Matukio ni mengi
Waziri wa Ulinzi amekaa kimya
Mkuu wa Majeshi amekaa kimya
Mkuu wa Mkoa amepiga kimya
Kikubwa zaidi Amiri Jeshi ambaye kwa mujibu wa wasaidizi wake yeye ndo kila.kitu ktk kuruhusu na kukataza naye amekaa kimya.
Tunajua kwamba, jambo hili ni chafu na dosari mbaya sana dhidi ya utawala bora. Lakini maslahi na usalama wa wananchi ni kipaumbele kikuu kikatiba na kisheria. Jeshi letu linasemwa ni la Wananchi. Je wahanga wa Kawe siyo raia wa nchi hii? Je wamevamia mipaka ya nchi hadi washughulikiwe na wanajeshi kiasi kile? Jeshi lisiige tabia ya vibaka wa panyaroad ambao wakipoteza memba wao kwenye tukio hupanga kisasi dhudi ya raia wema na hilo huanzia makabutini....
Tunayo Tume ya Haki za Binadamu ambayo inayo mamlaka ya kufuatilia ama kuchunguza matukio ya uvunjivu wa Haki za Binadamu nchini. Tunalo Bunge la Tanzania ambalo lina mamlaka ya kuunda tume kuchunguza matukio yenye athari kwa jamii. Tukio la wananchu wa Kawe kupigwa na wengine kudhurika maisha, ni baya sana.
PENDEKEZO.

- Tume ya Haki za Binadamu ichunguze ba kutoa ripoti kwa umma juu ya tukio la wanajeshi kuvamia raia majumbani na kuwapiga limejiri au hoax
- Tume ya Haki za Binadamu ituambie kiwango cha athari zilizojiri kwa raia na jeshi
- Mbunge wa Kawe apeleke Hoja Binafsi Bungeni ili Kamati ya Bunge iundwe kuchunguza tukio hili. Hoja ya Mbunge ihoji mamlaka ya Waziri wa Ulinzi ktk kusimamia nidhamu ya vikosi vyetu
- Ofisi ya Rais ya Maadili ya Viongozi ichunguze mwenendo wa viongozi wa kambi ya Lugalo kuhusu tukio hili na namna walivyoshiriki ama kudhibiti tukio la kupigwa kwa wananchi.