Ujenzi wa barabara Bugene - Burigi Chato urefu kilometa 60

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
Mlima Nyaishozi changamoto yake kubwa kuwa historia

Ujenzi Barabara ya kiwango cha lami ya kutoka Bugene hadi Bugiri Chato mkoa wa Kagera urefu wa kilometa 60 kuifikia CHATO NATIONAL PARK unaendelea


View: https://m.youtube.com/watch?v=GkkKS4c16Rg

SERIKALI imetoa Sh bilioni 92.84 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Bugene kwenda Burigi Chato Hifadhi ya Taifa yenye urefu wa kilomita 60 na kipande cha Bugene kwenda Kasulo hadi Kumunanzi yenye urefu wa kilomita 128.5 katika Mkoa wa Kagera.

Kaimu Meneja wa Wakala ya Barabara nchini (TANROADS) mkoa huo ametoa taarifa hiyo Novemba 11, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo inayotekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya China CCECC.

1702300395897.png
Photo : Mlima wa Nyaishozi

Mhandisi Mwaikokesya alisema ujenzi wa barabara hizo umeanza utekelezaji na kufikia asilimia 27.7 ikiwa kipande cha kilomita moja kilichopo kwenye Mlima wa Nyaishozi kimeanza kupasuliwa miamba na kuchimba kina kwa kwenda chini ya ardhi na kufikia mita 26.

Mhandisi Mwaikokesya alisema ujenzi unatarajia kukamilika Novemba 2024 ikiwa usanifu ulifanyika mwezi Februari 2022 na kampuni hiyo kusaini.

Lengo la kuiboresha zaidi eneo la mlima ilikuwa changamoto kubwa magari yalikuwa yanaanguka kila siku wakati mwingine kukwama hadi siku mbili Serikali ikaona kutatua changamoto hii.”alisema Mwaikokesya.

Aidha mhandisi Mwaikokesya alisema kuanza kwa ujenzi huo umeweza kutoa fursa kwa vijana ikiwa tayari ajira za muda 279 zimetolewa na Wananchi wa Wilaya ya Karagwe wananufaika kwa ajira.

Mhandisi Mwaikokesya alisema barabara hiyo ni kiwango cha udongo ambapo inawekewa kiwango cha lami ili wakulima waweze kusafirisha ndizi kwenda sokoni bila kukwama njiani.

Kaimu mhandisi Mshauri mkazi Onesmo Mgoha alisema maendeleo ya mradi huo yako vizuri hivyo wanao uhakika wakumaliza kwa wakati mvua sio kikwazo kwao watajitahidi kutumia njia mbadala ikiwemo kuongeza masaa ya kazi.
 
Mlima Nyaishozi changamoto yake kubwa kuwa historia

Ujenzi Barabara ya kiwango cha lami ya kutoka Bugene hadi Bugiri Chato mkoa wa Kagera urefu wa kilometa 60 kuifikia CHATO NATIONAL PARK unaendele...
Maendeleo hayana chama!
 
Maendeleo hayana chama!

Hatari ya maporomoko ya ardhi baada ya mlima Nyaishozi kuchimbwa kwa kina hiki kikubwa

Mifano ya ajali za ktk barabara zilizochongwa upande mmoja tofauti na hii barabara ya Bugene Bugiri Chato mkoani Kagera


View: https://m.youtube.com/watch?v=eePxKaQbWRQ

c.c
Wand
Content Manager / maxence melo Mubyazi JamiiForums editor : rejesha uzi huu jukwaa la siasa, ili wenye mamlaka ya maamuzi wanasiasa kama wabunge na mawaziri wafanye maamuzi sahihi kuepusha vifo, maafa na pia hasara mradi kutelekezwa kuwa White-elephant
 
Back
Top Bottom