Wananchi wakerwa na Mkandarasi anavyochelewesha Ujenzi wa Barabara

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Wananchi wanaotumia Barbara inayotoka Kibaoni kuelekea Sitalike mkoani Katavi yenye urefu wa kilomita 74 wamemlalamikia mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ambapo utekelezsji wake mpaka sasa unasuasua licha ya kukabidhiwa mradi huo mwezi juni 2022.


Florenc Johakimu, Silas Damashi na Debora Mwashi wamesema tangu mkandarasi amekabidhi kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo bado hata kipande kidogo cha lami hakijawekwa licha ya mkandarasi huyo kuonekana katika eneo la mradi tangu mwezi Juni 2022.

Martin Mwakabende ni meneja wa wakala wa barabara TANROADS mkoa wa Katavi amesema ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 74 utagharimu zaidi ya bilioni 88 huku mhandisi msaidizi mkazi katika mradi huo Jovin Ntiyetabula amesema kuchelewa kwa mkandarasi kutamlazimu afanye kazi zaidi huku akisisitiza mkandarasi kuzingatia mkataba wa kazi yake.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amefanya ziara mahsusi katika mradi huo na kubaini namna mkandarasi anavyosuasua kutekeleza mradi huo ipasavyo ambapi hadi sasa ni zaidi ya miezi 18 lakini kazi ya mkandarasi haionekani ikamlazimu kumuomba waziri wa wizara husika kumbadirisha mkandarasi ili ujenzi wa barabara hiyo uweze kutekelezwa na kukamilika haraka ili wananchi wa mkoa wa Katavi waanze kunufaika na barabara hiyo kwa kusafiri na kusafirisha mazao yao.
 
Wataalam hatuwezi kujudge kama mkandarasi anasua sua au laah...Bila kujua mkataba ni wa muda gani...kafanya kazi % ngapi.

Je amelipwa kiasi gani?

Je kuna changamoto za kimkataba au kimazingira zozote?

Ila wananchi ni haki yao
 
Back
Top Bottom