Uhuru wa Mahakama unadhihirika pale kila Jaji anapoweza kujitegemea katika kufanya Maamuzi ya kesi kwa Haki, bila upendeleo wala kushawishiwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Tafiti mbalimbali za Kimataifa zinaonesha Mahakama ni moja ya Taasisi zinazoongoza kwa vitendo vya Rushwa katika nchi za Afrika na Amerika ya Kusini.

Ingawa dhana hii inaweza kubadilika, haipaswi kupuuzwa kwani Rushwa Mahakamani hupelekea kukosekana kwa Haki na hivyo kuharibu Imani ya Umma katika Mfumo wa Mahakama kama chombo cha kutoa haki na usawa.

Nchi ya Denmark inatajwa mara nyingi kuwa kinara kwenye Nchi zenye kiwango kidogo cha Ufisadi kutokana na Uhuru mkubwa wa Vyombo vya Habari, Uwazi na Upatikanaji wa Taarifa kuhusu Matumizi ya Fedha za Umma, Viwango vikubwa vya Uadilifu kwa Maafisa wa Umma, na Mfumo huru wa Mahakama

Katika Nchi nyingi, kashfa kubwa zinazohusiana na Ufisadi, Matumizi mabaya ya Fedha za Umma au tabia zisizo za Maadili kutoka kwa Viongozi na Wanasiasa zimechangia kufanya Wananchi wapoteze imani kwa Serikali zao na hata kupelekea Mapinduzi kwa baadhi ya Nchi.

Uhuru wa Mahakama unadhihirika pale kila Jaji anapoweza kujitegemea katika kufanya Maamuzi ya kusuluhisha kesi iliyofikishwa mbele yake, kwa Haki, bila Upendeleo, au kushawishiwa na upande wowote (Majaji wengine, Serikali, Taasisi au Mtu binafsi).

Pia, Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwepo kwa Uhuru wa Kifedha na Kiutawala wa Chombo hiko cha Haki ambao unalindwa na kukuzwa, bila kuingiliwa na Mtu au Taasisi nyingine.

Uhuru wa Mahakama unaweza kulindwa kwa (i) Uteuzi wa Majaji kwa kuzingatia Sifa na Uadilifu; (ii) Majaji kulindwa dhidi ya maamuzi yasiyofaa kwao na (iii) Ulinzi dhidi ya kuondolewa kwa Unyanyasaji.
 
Bwana Rostam Azizi alisema ukweli mchungu kuhusu mahakama zetu.nikikumbuka kesi ya ugaidi ya Mbowe, huwa nabaki kushangaa,ujinga wa majaji wa Tanzakiza.
 
Tafiti mbalimbali za Kimataifa zinaonesha Mahakama ni moja ya Taasisi zinazoongoza kwa vitendo vya Rushwa katika nchi za Afrika na Amerika ya Kusini.

Ingawa dhana hii inaweza kubadilika, haipaswi kupuuzwa kwani Rushwa Mahakamani hupelekea kukosekana kwa Haki na hivyo kuharibu Imani ya Umma katika Mfumo wa Mahakama kama chombo cha kutoa haki na usawa.

Nchi ya Denmark inatajwa mara nyingi kuwa kinara kwenye Nchi zenye kiwango kidogo cha Ufisadi kutokana na Uhuru mkubwa wa Vyombo vya Habari, Uwazi na Upatikanaji wa Taarifa kuhusu Matumizi ya Fedha za Umma, Viwango vikubwa vya Uadilifu kwa Maafisa wa Umma, na Mfumo huru wa Mahakama

Katika Nchi nyingi, kashfa kubwa zinazohusiana na Ufisadi, Matumizi mabaya ya Fedha za Umma au tabia zisizo za Maadili kutoka kwa Viongozi na Wanasiasa zimechangia kufanya Wananchi wapoteze imani kwa Serikali zao na hata kupelekea Mapinduzi kwa baadhi ya Nchi.

Uhuru wa Mahakama unadhihirika pale kila Jaji anapoweza kujitegemea katika kufanya Maamuzi ya kusuluhisha kesi iliyofikishwa mbele yake, kwa Haki, bila Upendeleo, au kushawishiwa na upande wowote (Majaji wengine, Serikali, Taasisi au Mtu binafsi).

Pia, Uhuru wa Mahakama unamaanisha kuwepo kwa Uhuru wa Kifedha na Kiutawala wa Chombo hiko cha Haki ambao unalindwa na kukuzwa, bila kuingiliwa na Mtu au Taasisi nyingine.

Uhuru wa Mahakama unaweza kulindwa kwa (i) Uteuzi wa Majaji kwa kuzingatia Sifa na Uadilifu; (ii) Majaji kulindwa dhidi ya maamuzi yasiyofaa kwao na (iii) Ulinzi dhidi ya kuondolewa kwa Unyanyasaji.
Hatuna majaji, tuna shyster judges, majaji wa UPE, takataka tupu
 
Back
Top Bottom