Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Paul Makonda, Mwenezi wa CCM akiwa anazunguka nchi nzima kwa misafara mirefu kuliko kiongozi yeyote na kusikiliza kero na kuwalalamikia CCM wenzake kwa kutofanya kazi. Mwanzo alianza na kulalamikia CHADEMA, AKAJA KWA MBOWE SASA wana CCM wenzie.
Makonda amewaambia wananchi na kuwaagiza wasipeleke kesi Mahakmani kwakuwa hawana hela kama yeye ili kununua haki na kwamba hata yeye alidhulumiwa nyumba lakini akaona asiende mahakamani maana hatapata haki.
Juzi hapa Makonda alielimishwa na Mh AG Eliezer Feleshi ambaye kama watu hawajui FELESHI ndiye Mshauri Mkuu wa Nchi ya Tanzania. Sasa Makonda kampanda kichwani, Mahakama na AG, wamekaa kimya.
Hii kauli ya Makonda tunaweza kuitazama kwa angle nyingi lakini inauvua nguo mfumo wa haki nchini.
Kwa bahati mbaya ni kauli ya kweli kabisa. Ndio, ni kauli ngumu lakini ina akisi tatizo la mfumo wetu wa utoaji haki.Mahakimu mishahara ya milioni na nusu lakini wanautajiri uliopindukia huku wakiwa na anasa mitaani. Fedha za wenyenazo dhidi ya wasio nazo.
Anachosema Makonda ni kuwa bila kuwa na pesa na connection, sahau HAKI hasa kwenye mahaama. Yeye anaamini anazidiwa fedha na GSM ndio maana nyumba ya masaki kasamehe.
Ninachopingana na Makonda ni kuwa haki ipo serikalini, hii sio kweli. Wala serikali sio chombo cha kutoa haki, chombo cha haki ni mahakama/judiciary. Ni muhimili unaojitegemea.
Tunahitaji kujenga mfumo wa mahakama ulio huru na unaosimamia kweli na usioegemea upande wowote.
Rostam Aziz alisema kuhusu Mfumo wa Mahakama kuwa umeoza akaambiwa akanushe chap sasa Mwenezi anaonesha panapovuja na ndio Uhalisia.
Mfumo ambao haki siyo upendeleo bali ni fursa inayoweza kupatikana na kila mtu. Ni muhimu sasa, zaidi ya wakati wowote, kutafuta suluhu na kufanya mahakama zetu kuwa huru. Mbona Kenya wanaweza? Hawa si ni wenzetu tu wa eneo hili la Afrika Mashariki?
Makonda anasema mfumo wetu wa utoaji haki umeoza, inawezekana ni kweli. Basi turekebishe huo mfumo, tusiukimbie na kutengeneza mfumo mwingine. Hiyo sio solution.
Pia Soma:
- Paul Makonda: Maskini Ukizulumiwa Haki Usikimbilie Mahakamani" Mahakama Wajitafakari