Mahakama Kujikita Kwenye Kasoro za Kiufundi Katika Kutoa Maamuzi Yenye Tija kwa Taifa ni Ishara ya Udhaifu na Uoga Dhidi ya Serikali

Konny Joseph

Member
Aug 28, 2016
98
174
Pamoja na ukweli kwamba Ibara ya 107A(2)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitaka Mahakama kutoa haki bila kujifunga na mambo ya kiufundi kiasi cha kushindwa kutoa haki,mambo kwa upande wa mahakama zetu ni tofauti kabisa hususan kwenye mashauri ambayo yanahusu kushitakiwa kwa serikali au vigogo wa serikali.

Kumekuwa na muendelezo wa kesi nyingi kushindwa kutolewa maauzi yenye tija kwa umma kwa kigezo tu cha kasoro za kiufundi ambazo ukizichunguza huwa hazina uzito ukilinganisha na uzito wa ile haki inayodaiwa.

Nimejaribu kufuatilia kwenye Kesi ya Ado Shaibu v.Honorable John Magufuli,Misc Civil Cause No.29 of 2018,kesi ambayo ilipinga uteuzi wa Adelarus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu kwa kuwa hakuwa na sifa.Badala Mahakama kujikita katika kutoa uamuzi wa hoja iliyopo mezani,iliamua kujikita katika kijadili mambo na mapungufu ya kiufundi katika kesi husika na kushindwa kutoa uamuzi wenye tija kwa taifa.

Nikiangalia hata katika kesi inayoendelea ya Pauline Gekul na Ndugu Hashim Ally,naona Mahakama imejikita kushughulikia mambo ya kiufundi katika kesi hiyo badala ya kujadili haki ya msingi ambayo ndugu Hashim Ally anaiomba Mahakama impatie.

Ni wazi kwamba mambo yote haya,yanasbabishwa na udhaifu wa mfumo wettu wa utoaji haki.Na ubovu huu unasababishwa na Mahakama yetu kutokuwa huru,kiasi cha kuingiliwa uhuru wake na mihimili mengine.

Ni wazi kwamba mahakama kujikita katika mambo ya kiufundi badala kusimamia utoaji wa haki katika malalamiko yanayowasilishwa hususan yanayohusu serikali ni ishara ya namna mahakama ilivyo na uoga kuiwajibisha serikali katika mashauri ya msingi.Hivyo njia pekee huwa ni kuchambua kasoro za kiufundi kama njia pekee ya kukwepa kuiwajibisha serikali

Kukosekana kwa uhuru huku ndio husababisha kupatikana kwa majaji na mahakimu wasiokuwa na sifa,ambao wameendelea kuwa mzigo kwa mahakama na taifa kwa ujumla.

Ni wazi kwamba kuna haja ya kufanya mageuzi ya haraka ili kuboresha mifumo yetu ya utoaji haki ili kulinda maslahi ya Taifa.Na njia pekee ya kuboresha mifumo hii ni kupata katiba mpya ambayo itasimamia mifumo na kuhakikisha mahakama zinakuwa huru​
 
Nchi nyengine duniani jaji mkuu,mkuu wa mapolisi na mkuu wa mkoa hupigiwa kura na wananchi sio kuteuliwa.

Sababu ukiteuliwa lazima ulipe fadhila kwa alie kuteuwa.
 
Tanzania hakuna mahakama bali Majengo yenye jina la mahakama.Ni mpumbavu pekee ndio atapoteza muda kuamini kwamba Kuna haki ndani ya taifa hili.

Majaji wenyewe ndo hawa wanao chaniwa hukumu na viongozi wa serikali.
 
...kuna haja ya kufanya mageuzi ya haraka ili kuboresha mifumo yetu ya utoaji haki ili kulinda maslahi ya Taifa.Na njia pekee ya kuboresha mifumo hii ni kupata katiba mpya ambayo itasimamia mifumo na kuhakikisha mahakama zinakuwa huru
Nakazia ✍️ ✍️ ✍️
Katiba mpya ndo muarobaini wa kuweka huru mahakama na Bunge kutoka kwenye kongwa la mhimili wa serikali.

Kama alivyowahi kusema JPM (RiP), kwa mfumo wa sasa mhimili wa serikali umejichimbia kwenda chini zaidi na hivyo umejitwalia mamlaka juu ya mihimili mingine, jambo ambalo ni kinyume na utawala bora
 
Mahakama haina hadhi ya kusikiliza kesi, unataka ifosi.

Ikishahukumu muhukumiwa akikata Rufaa kuwa Mahakama haikustahili kusikiliza hiyo kesi, itakuwaje????

Acha kuleta hisia kwenye mambo ya kisheria
 
Kama Mahakama inasikiliza kesi ambayo haina hadhi yake hadi inatoa hukumu, basi huo ni udanganyifu wa hali ya juu sana,wote walioshiriki kufungua hiyo kesi kuanzia karani wa Mahakama hadi hakimu aliyesikiliza hiyo kesi na kutoa hukumu wote wanatakiwa washitakiwe kwa kuchezea haki za watu kwa makusudi kabisa,maana hao ndiyo wataalamu wetu wa sheria!!
 
Mahakama haina hadhi ya kusikiliza kesi, unataka ifosi.

Ikishahukumu muhukumiwa akikata Rufaa kuwa Mahakama haikustahili kusikiliza hiyo kesi, itakuwaje????

Acha kuleta hisia kwenye mambo ya kisheria
Sijaelewa hata unachokiongoa hebu fafanua vizuri hoja yako uelekezwe mana naona unahemkwa tu!!
 
Pamoja na ukweli kwamba Ibara ya 107A(2)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaitaka Mahakama kutoa haki bila kujifunga na mambo ya kiufundi kiasi cha kushindwa kutoa haki,mambo kwa upande wa mahakama zetu ni tofauti kabisa hususan kwenye mashauri ambayo yanahusu kushitakiwa kwa serikali au vigogo wa serikali.

Kumekuwa na muendelezo wa kesi nyingi kushindwa kutolewa maauzi yenye tija kwa umma kwa kigezo tu cha kasoro za kiufundi ambazo ukizichunguza huwa hazina uzito ukilinganisha na uzito wa ile haki inayodaiwa.

Nimejaribu kufuatilia kwenye Kesi ya Ado Shaibu dhidi ya Rais John Magufuli na Mwanasheria Mkuu,kesi ambayo ilipinga uteuzi wa Adelarus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu kwa kuwa hakuwa na sifa.Badala Mahakama kujikita katika kutoa uamuzi wa hoja iliyopo mezani,iliamua kujikita katika kijadili mambo na mapungufu ya kiufundi katika kesi husika na kushindwa kutoa uamuzi wenye tija kwa taifa.

Nikiangalia hata katika kesi inayoendelea ya Pauline Gekul na Ndugu Hashim Ally,naona Mahakama imejikita kushughulikia mambo ya kiufundi katika kesi hiyo badala ya kujadili haki ya msingi ambayo ndugu Hashim Ally anaiomba Mahakama impatie.

Ni wazi kwamba mambo yote haya,yanasbabishwa na udhaifu wa mfumo wettu wa utoaji haki.Na ubovu huu unasababishwa na Mahakama yetu kutokuwa huru,kiasi cha kuingiliwa uhuru wake na mihimili mengine.

Ni wazi kwamba mahakama kujikita katika mambo ya kiufundi badala kusimamia utoaji wa haki katika malalamiko yanayowasilishwa hususan yanayohusu serikali ni ishara ya namna mahakama ilivyo na uoga kuiwajibisha serikali katika mashauri ya msingi.Hivyo njia pekee huwa ni kuchambua kasoro za kiufundi kama njia pekee ya kukwepa kuiwajibisha serikali

Kukosekana kwa uhuru huku ndio husababisha kupatikana kwa majaji na mahakimu wasiokuwa na sifa,ambao wameendelea kuwa mzigo kwa mahakama na taifa kwa ujumla.

Ni wazi kwamba kuna haja ya kufanya mageuzi ya haraka ili kuboresha mifumo yetu ya utoaji haki ili kulinda maslahi ya Taifa.Na njia pekee ya kuboresha mifumo hii ni kupata katiba mpya ambayo itasimamia mifumo na kuhakikisha mahakama zinakuwa huru​
MAHAKAMA ZIPO KENYA HAPA NI VIKAO VYA CCM NDANI YA MAJENGO YA MAHAKAMA
 
Kama kichwa cha habari cha uzi huu kilivyo, ndivyo Antipasu alivyobobea kwenye eneo hili....!!! Anaweza kutumia kukosekana kwa nukta juu ya herufi "I" kupora haki ya mwenye haki!!!
 
Back
Top Bottom