Kigezo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kuwa na Sifa ya Ujaji Hakifanyi Maamuzi yake kuwa ni ya Haki

Konny Joseph

Member
Aug 28, 2016
98
173
Kumekuwa na dhana inayotengenezwa na serikali ya CCM kwamba kwa kuwa Mwenyekiti wa NEC ni mtu mwenye nyadhifa ya ujaji basi ni wazi kwamba maamuzi yote atakayoyapitisha yatakua ni haki,na hayapaswi kupingwa na mtu yeyote au chombo chochote.

Jamii inapaswa ielewe kwamba heshima ya maamuzi ya jaji inapatikana pale tu Jaji anapokalia kiti cha Mahakama au chombo mfano wa mahakama kama Tume ya Maadili ya Mawakili kupitisha maamuzi.

Maamuzi ya ujaji hayatopatikana ikiwa mtu anatekeleza majukumu mengine nje ya mahakama,kama kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Mwanassheria Mkuu au Mwendesha Mashitaka Mkuu.

Nadharia hii potofu ndio imekuwa inatumiwa na serikali ya CCM kupinga hoja ya maamuzi ya Tume ya Uchaguzi kupingwa Mahakamani kwa kisingizio kwamba maamuzi ya tume yametolewa na mtu mwenye nyadhifa ya ujaji.

Hiki ni kiini macho cha wazi amabacho serikali ya CCM wamekitengeneza ili kulaghai umma kuwa maamuzi yote ya tume yatakuwa halali kwa kutumia kigezo hicho bandia.

Ieleweke kwamba chombo chenye mamlaka ya kutoa haki ni Mahakama peke yakekwa mujibu wa katiba.Tunaposema mahakama ni pale jaji wanapokalia kiti cha mahakama katika kutoa haki.Hii haina maana kwamba mtu mwenye sifa ya jaji anaweza kutoa haki nje ya mipaka ya kimahakama.

Na ndio maana hata kinga ya majaji na mahakaimu inapatikana pale tu wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya kimahakama na sio vyenginevo.

Hivyo ni wazi kwamba maamuzi ya Tume ya Uchaguzi yanapaswa kupingwa katika mahakama za kisheria kama zilivo katika nchi nyingi duniani.

Tume kuongozwa na jaji hakuipi tune mamlaka ya kimahakama ya kutoa haki.Hivyo mamamuzi yake hayawezi kuhesabiwa kuwa ni maamuzi ya haki kamwe.
 
Hakika , Kwa mfano hakuna Jaji aliyekuwa mtenda haki Mahakamani kama Lewis Makame , lakini alipoletwa Tume ya Uchaguzi , heshima yake yote aliyojijengea ilipeperuka kirahisi sana baada ya kuanza kutumikishwa na ccm .

Makame hakupaswa kuzikwa namna ile baada ya kufa
 
Bora hata katiba iseme mkuu wa majeshi ndio mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Au vipi jamani siingekua vizuri
 
Majaji karibu wote ni Makada wa CCM, hawatendi haki mahakamani na nje ya mahakama
 
Bora hata katiba iseme mkuu wa majeshi ndio mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Au vipi jamani siingekua vizuri
Ingekuwa ni bora zaidi,ingawa na hawa viongozi wetu wa vyombo vya dola nao wamekuwa wanatumika vile vile kulinda maslahi ya kisiasa.

Ndio ukaona Col Lubinga (aliekuwa msemaji wa jeshi)aliteuliwa kuwa katibu muenezi na uhusiano wa mambo ya nje wa CCM, huku akiwa bado ni mtumishi wa JWTZ.

Kuna wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni wanajeshi nao wapo wanalinda maslahi na ilani za CCM katika maeneo yao jambo ambalo ni kosa kubwa.

Kwa hiyo ukichunguza utakuta mifumo yote ya nchi imeshafeli na ndio maana ukakuta nguvu ya kukabiliana na CCM imekua ndogo kwa kuwa wameshanunua mifumo mingi ya nchi.
 
Bora hata katiba iseme mkuu wa majeshi ndio mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Au vipi jamani siingekua vizuri
Ingekuwa ni bora zaidi,ingawa na hawa viongozi wetu wa vyombo vya dola nao wamekuwa wanatumika vile vile kulinda maslahi ya kisiasa.

Ndio ukaona Col Lubinga (aliekuwa msemaji wa jeshi)aliteuliwa kuwa katibu muenezi na uhusiano wa mambo ya nje wa CCM, huku akiwa bado ni mtumishi wa JWT

Back
Top Bottom