Uhaba wa Mafuta na Dola, nashauri Rais atumie fursa ya Mkutano wa Afrika na Urusi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Nafikiri tumshauri Rais Samia afanye uamuzi mgumu kunusuru uchumi wa nchi kwa mgogoro huu wa mafuta nchini.

Tarehe 27/28 July 2023 nchi za Afrika 49 kati ya 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa zilishiriki Mkutano wa Afrika na Urusi mjini St. Petersburg nchini Urusi na mambo Makuu mawili ambayo Rais wa Urusi Vladmir Putin alitangazia dunia na kuahidi kwa Nchi za Afrika ni;

1. Biashara zote kati ya Mataifa ya Afrika na Urusi zitafanyika kwakutumia Sarafu za Mataifa husika na sarafu ya Urusi ya Ruble.

2. Putin alitangaza kuyapatia Mataifa ya Afrika Mafuta na Gesi kwa Bei rahisi (nusu bei na kusafirishiwa bure).

3. Kuyapatia Chakula na Nafaka BURE mataifa yote yenye Uhaba wa chakula hii ilijumuisha Kuanzia kusafirishiwa bure hadi katika nchi husika na kwakuanza, Urusi iliainisha Tani 50,000 za nafaka kutolewa bure kwa nchi 6 za awali wiki inayoanza jumatatu ya keshokutwa.

Tukio lingine kubwa ni kusamehewa madeni yote kwa nchi za Afrika. Hii inamaana madeni ya Tanzania kwa Urusi hasa yale ya Kipindi cha Vita na Uganda maarufu kama maneni ya EPA ambayo CCM iliwahi kuiba pesa zile na kufanyia uchaguzi kipindi cha 2005-2015. Pia madeni ya ununuzi wa Silaha za Kijeshi katika majeshi yetu na vyombo vingine vya Usalama.

Tanzia ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki kikamilifu mkutano huo, na hata baada ya mkutano kuisha, Tanzania ilipewa upendeleo wa kipekee kwa kualikwa na Rais Putin kushiriki sherehe za maadhimisho ya majeshi ya majini nchini Urusi, ambapo Waziri Mkuu aliongozana na Putin katika manowari ya Kijeshi wakizuru na kukagua vikosi vyabaharini kikamilifu.

HOJA: Rais Samia tumia fursa hii ya kuwa Tanzania ni nchi isoyofungamana na Upande Wowote, Wafanyabishara waagize mafuta moja kwa moja Urusi kwakutumia Sarafu ya Tanzania. Tuache kuogopa mashinikizo ya kimagharibi ambayo yanazidi kuumiza taifa letu. Sisi ni nchi isoyofungamana na Upande Wowote. Tuitumie haki hii kama tulivyothubutu kushiriki mkutano huu ili tuokoe watu wetu.

Matunda ya kushiriki Mkutano ule na kupata fursa ile, ni kuzitumia fursa hizi, biashara ya mafuta hatufungwi na sheria yoyote ya Kimataifa zaidi ya matumizi ya Dola tu ndio yanayotufunga, tunaweza kununua popote. Fursa ya kununua kwa kutumia Shilingi yetu imepatikana kutoka MOSCOW, tunataka nani atuamulie jambo hili?

Moscow inavikwazo vya Kimataifa, je, fursa ya Urusi waliyoitoa ya kutuletea wao wenyewe mafuta hadi bandaniri Dar es Salaam kwanini tusiitumie?

Kama sio hivyo kwanini tusipate kwa njia mbadala mfano, Nchi za OPEC zinauza mafuta, na Urusi ni mkuu wa OPEC, kwanini tusinunue mafuta ya Urusi kupitia Dubai, Oman, Saudia nk kwa mwamvuli wa OPEC transit?

Hivi nani anatakiwa kutusimamia kucheza game hizi ndogo kabisa kama sio sisi wenyewe?

IMG_20230805_215735_610.jpg
 
Yericko Nyerere unajiita mtaalam wa ujasusi unashindwa kutambua siasa za kimataifa hadi unauliza hili swala

"kwanini tusinunue mafuta ya Urusi kupitia Dubai, Oman, Saudia nk kwa mwamvuli wa OPEC transit",

Kununua mafuta ya Russia ni complicated kuliko hata upatikanaji wa Dola, Urusi iliwekewa ukomo wa bei ya mafuta, yanasafirishwa kwa njia ya bahari, kwa sasa meli zote kubwa za usafirishaji wa mafuta bima zao nyingi wakatia Uingereza na Marekani kwa sababu hiyo wasafirishaji wengi inabidi wafate vikwazo vilivyoko.

Kingine kiwango cha biashara kati ya Urusi na Tanzania ni kidogo san, tukibadilisha Tshs na Rubbles, bila shaka wao watapokea fedha zetu nyingi sana kuliko sisi tunavoweza kupokea zao, unadhani ni nchi gani duniani Urusi atenda kununua huduma/bidhaa na Pesa ya Tanzania.

Huwa nikiwasikiliza viongozi wa kiafrika wanavojiongopea kuwa watafanya biashara kwa currency zao, nacheka sana.. yaani sidhani kama hata ile batter trade wanaikumbuka

Mwisho upungufu wa dola nchini ni uzembe wa serikali ya Samia kwa 200%
 
Jirani zetu Kenya na DRC wanaagiza nafaka kutoka Urusi na zinafika bila hiyo complicated unayozungumza.... Uliwahi kujiuliza wanafanikiwaje?
 
Inasemekana,Nilisoma Humu thread fulani kuwa Sasa hivi Nchi yetu inanunua Mafuta kutoka Kampuni za India, ambapo India inanunua 1/2 bei kutoka Urusi na Kuleta hapa TZ kwa bei faida maradufu.
Mwisho hii ni Vita Kubwa mnoo na huwa inaweza ondoa mtu ktk maslahi ya Kibiashara.Kwa hili inawezekana watu wanapiga Hela sawa sawa?
 
Jirani zetu Kenya na DRC wanaagiza nafaka kutoka Urusi na zinafika bila hiyo complicated unayozungumza.... Uliwahi kujiuliza wanafanikiwaje?
Elezea hiyo njia unayoweza kuishauri Serikali kununua mafuta Russia.

Na hujajibu swali langu, tukinunua mafuta kwao kwa TSZ, wao watazitumia wapi hizo TZS wakati hakuna usawa kati ya biashara sisi na wao.

Marekani haina hata shaka na issue inaitwa De-dollarization, sababu some currency ni so useless nje ya mipaka yake.

Upungufu wa dola nchini ni uzembe wa serikali ya Samia na for some reason kunawatu wanafanya currency manipulation, na Samia anaogopa kuambiwa alifungia Bureau de change, wenzetu China wana deavaluate currency yao at state level kwa kununua dola hili ziwe chache, watu waende China kununua bidhaa kwa bei nafuu against dollar, sisi tunaacha wauza hela wajiamulie.
 
Labda kama tutafanya barter system. Hizo rubble tunazitoa wapi? Tunawauzia nini Urusi ili tupate rubbles??

Unafahamu biashara za kimataifa zinavyofanyika kweli? Sisi na Urusi biashara yetu ina ukubwa kiasi gani?

Alafu tukipigwa vikwazo na mataifa mengine unadhani faida ya kufanya biashara na Urusi itakuwa kubwa kuliko hasara tutakayoipata?
 
Kuomba nafaka ni uvivu wa wananchi kulima, ardhi yenye rutuba ipo tele.
 
CCM hawajuhi wafanye nini? Serikali imejaa wajinga na wezi, ni kikundi cha watu wameiteka nchi, wanaitafuna,
Hawafiki hata laki tano,lakini wananchi milioni55! Wamekaa tu, wanasubili hawa laki tano walete miujiza, dawa ni mapinduzi, ya kijeshi tu,
Uarabuni mabadiriko yaliletwa na vijana, kitaani, Huku Afrika nyeusi, vijana wa jeshini, wafanye Mambo, tatizo wa hapa bongo, wanachojua ni kugombsnia madem baa, kununua foresta,na kujenga vijumba kadhaa kigsmboni na bagamoyo, kufuga kuku, hawana ambitions kubwa!
 
Ushauri wa hovyo na mbaya we huzi rubles utazipeleka wapi??
Nchi gani itaikubali??
Mabeberu wanatupa lesa kiasi gani hadi tuwaruke tununue mafuta ya urusi(discount)
urusi yenyewe iko taabani kiuchumi hana nafaka ya kuuza kwa africa wala kutoa bure
 
Labda kama tutafanya barter system. Hizo rubble tunazitoa wapi? Tunawauzia nini Urusi ili tupate rubbles??

Unafahamu biashara za kimataifa zinavyofanyika kweli? Sisi na Urusi biashara yetu ina ukubwa kiasi gani?

Alafu tukipigwa vikwazo na mataifa mengine unadhani faida ya kufanya biashara na Urusi itakuwa kubwa kuliko hasara tutakayoipata?
Hahahahahaa kichekesho kaandika
 
Hebu ondoa matango pori Yako hapa sema hivi mmebanwa na USA kununua bidhaa ya Urusi Ili tuendelee kupokea misaada ikiwamo fedha za kukata watu magovi, vyandarua etc, hivi unaposema hakuna business balance kati ya Russia na Tanzania Kwan ni nani alikwambia kuwa Kuna business balance kati ya USA na Tz? Halafu ndo nyie mlisema bila dollar Dunia haitojizungusha kwenye mhimili wake lakini watu wameipiga chin na maisha yanaendelea kama Kawa, au unataka kusema Kuna business balance kati ya tz na china?
 
Yericko ni kanjanja kihiyo tu.
Ni hasara CHADEMA kuwa na mtu wa aina yake mstari wa mbele.
Yericko Nyerere unajiita mtaalam wa ujasusi unashindwa kutambua siasa za kimataifa hadi unauliza hili swala

"kwanini tusinunue mafuta ya Urusi kupitia Dubai, Oman, Saudia nk kwa mwamvuli wa OPEC transit",

Kununua mafuta ya Russia ni complicated kuliko hata upatikanaji wa Dola, Urusi iliwekewa ukomo wa bei ya mafuta, yanasafirishwa kwa njia ya bahari, kwa sasa meli zote kubwa za usafirishaji wa mafuta bima zao nyingi wakatia Uingereza na Marekani kwa sababu hiyo wasafirishaji wengi inabidi wafate vikwazo vilivyoko.

Kingine kiwango cha biashara kati ya Urusi na Tanzania ni kidogo san, tukibadilisha Tshs na Rubbles, bila shaka wao watapokea fedha zetu nyingi sana kuliko sisi tunavoweza kupokea zao, unadhani ni nchi gani duniani Urusi atenda kununua huduma/bidhaa na Pesa ya Tanzania.

Huwa nikiwasikiliza viongozi wa kiafrika wanavojiongopea kuwa watafanya biashara kwa currency zao, nacheka sana.. yaani sidhani kama hata ile batter trade wanaikumbuka

Mwisho upungufu wa dola nchini ni uzembe wa serikali ya Samia kwa 200%
 
Elezea hiyo njia unayoweza kuishauri Serikali kununua mafuta Russia.

Na hujajibu swali langu, tukinunua mafuta kwao kwa TSZ, wao watazitumia wapi hizo TZS wakati hakuna usawa kati ya biashara sisi na wao.

Marekani haina hata shaka na issue inaitwa De-dollarization, sababu some currency ni so useless nje ya mipaka yake.

Upungufu wa dola nchini ni uzembe wa serikali ya Samia na for some reason kunawatu wanafanya currency manipulation, na Samia anaogopa kuambiwa alifungia Bureau de change, wenzetu China wana deavaluate currency yao at state level kwa kununua dola hili ziwe chache, watu waende China kununua bidhaa kwa bei nafuu against dollar, sisi tunaacha wauza hela wajiamulie.
Mjadala huu unatija:
Ziko njia mbili au tatu hata nne za kuchukua Fursa ndani ya changamoto.

1.Mafuta:
Ni kweli Mafuta na gas pamoja na NAFAKA zinapatikana Russia kwa Nusu bei!

Nchi kama Nchi haiwezi kuingia kwenye biashara kama hii kwa Sababu globally inasomeka kama Black or grey business!

Lakini Serikali inaweza kufungua Dirisha dogo na la muda maalum kwa wafanyabiashara....wa kimkakati kwa ajili ya kuingiza Mafuta kwa au iyo Nusu bei au Robotatu bei..!

Wafanyabiashara wanajuana....

Wao watafanya isipokuwa tu kuwepo na jicho la tai...iwapo kutakuwa n hatari ya kupoteza mitaji....

Hii inafanyika na Mataifa tajiri...mfano ni China na Huwawei...

Sasa hivi ziko kampuni za China zinazotengeneza Microchips....ni Makampuni binafsi Lakini jicho la tai liko juu yao..

2.Njia ya Pili ni Kudevaluate Bei ya Gold kwa ajili ya ku attract iyo Nusu bei ya Mafuta...iyo ni Nchi kwa Nchi.

3.Dollar:
Hii inahitaji akili kubwa sana lakini moja na la haraka ni Bot kushusha thamani ya Shilingi kwa makusudi ya kuchochea influx ya Dollar...hapa Lazima avenue zote za kuingiza Dollar zitizamwe vizuri kabla ya kufikia uamuzi huo.

Miradi Mikubwa ya Nchi ifanywe ns Wenyeji ili kuokoa pesa kwenda nje..

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Kwa nini mfanyabiashara aache kununua mafuta nchi za karibu na Tanzania akazurure huko kote mbali Ruzzia??
Mjadala huu unatija:
Ziko njia mbili au tatu hata nne za kuchukua Fursa ndani ya changamoto.

1.Mafuta:
Ni kweli Mafuta na gas pamoja na NAFAKA zinapatikana Russia kwa Nusu bei!

Nchi kama Nchi haiwezi kuingia kwenye biashara kama hii kwa Sababu globally inasomeka kama Black or grey business!

Lakini Serikali inaweza kufungua Dirisha dogo na la muda maalum kwa wafanyabiashara....wa kimkakati kwa ajili ya kuingiza Mafuta kwa au iyo Nusu bei au Robotatu bei..!

Wafanyabiashara wanajuana....

Wao watafanya isipokuwa tu kuwepo na jicho la tai...iwapo kutakuwa n hatari ya kupoteza mitaji....

Hii inafanyika na Mataifa tajiri...mfano ni China na Huwawei...

Sasa hivi ziko kampuni za China zinazotengeneza Microchips....ni Makampuni binafsi Lakini jicho la tai liko juu yao..

2.Njia ya Pili ni Kudevaluate Bei ya Gold kwa ajili ya ku attract iyo Nusu bei ya Mafuta...iyo ni Nchi kwa Nchi.

3.Dollar:
Hii inahitaji akili kubwa sana lakini moja na la haraka ni Bot kushusha thamani ya Shilingi kwa makusudi ya kuchochea influx ya Dollar...hapa Lazima avenue zote za kuingiza Dollar zitizamwe vizuri kabla ya kufikia uamuzi huo.

Miradi Mikubwa ya Nchi ifanywe ns Wenyeji ili kuokoa pesa kwenda nje..

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Hebu ondoa matango pori Yako hapa sema hivi mmebanwa na USA kununua bidhaa ya Urusi Ili tuendelee kupokea misaada ikiwamo fedha za kukata watu magovi, vyandarua etc, hivi unaposema hakuna business balance kati ya Russia na Tanzania Kwan ni nani alikwambia kuwa Kuna business balance kati ya USA na Tz? Halafu ndo nyie mlisema bila dollar Dunia haitojizungusha kwenye mhimili wake lakini watu wameipiga chin na maisha yanaendelea kama Kawa, au unataka kusema Kuna business balance kati ya tz na china?
Hata kujaribu kukuelekeza kiazi kama wewe ni kupoteza muda, wazazi wako na heri wangefuga ng'ombe kuliko kuleo jitu mbumbumbu namna hii.
 
Ushauri wa hovyo na mbaya we huzi rubles utazipeleka wapi??
Nchi gani itaikubali??
Mabeberu wanatupa lesa kiasi gani hadi tuwaruke tununue mafuta ya urusi(discount)
urusi yenyewe iko taabani kiuchumi hana nafaka ya kuuza kwa africa wala kutoa bure
Itapendeza ukiwa unafuatilia facts before kujibeza. Asilimia zaidi ya 80% ya mafuta duniani yaliyokuwa yanatumika, ni mafuta ya urusi. Zaidi ya %95 ya gesi iliyokuwa inatumika kwa nchi za ulaya, (Asia n kwa weupe wotee isipokuwa waarabu tu) na inayoendelea kutumika hadi leo ulaya, ni gesi ya Russia. Kwa tathmini isiyo rasmi, urusi amefanya biashara na duniani kwa zaidi ya miaka 15. Kwa ufafanuzi zaidi, mruzi amekuwa akiiuzia dunia nzimaaaaa, yani kwa siku amekuwa akiingiza zadi ya $ 1 trilion, hili lijamaa ni tajiri aisee😂😂😂Pia tukumbuke, sijalizingatia bara la africa sababu tunachangia %2 tu ya magari, so matumizi yetu ya mafuta ni madogo saaaana, ila tunaweza kusema %80 ya mafuta ya africa before the special operation in Ukraine, yalikuwa ni ya mrusi. Mzee putin kwenye hii vita, bado hajaanza kuzitumia silaha mpya, Asilimia zaidi ya 90 ya vifaa vyake, ni vifaa vya karne iliyopita, bado hajaanza kutumia vifaa vipya. NATO nzima ni lazima ipigane kwa umoja ili iweze kupambana na mrusi. Yani hakuna nchi iliyokamilika kama urusi. Ile nchi ni tajiri hadi shidaaah. Uchumi wake utatetereka ila haitotokea kuja kuanguka. Yule ndio super power wa dunia. Yani, one man army. Akiamua kuimaliza marekani, ataimaliza na kukifyeka kizazi chote cha kimarekani kwenye uso wa dunia. Nilikuwa sitaki kuongelea nuclear warheads (mabomu ya nyuklia), anayamiliki zaidi ya 5000 (ambayo sio hewa, wamarekani wamepandisha idadi yao ili kujibeza) hadi sasa, ambayo dunia nzima tukijikusanya ndio labda tutafanikiwa kuifikia idadi ya Russia. Kwa ufupi yule ndiye mwanaume peke yake miongozi kwenye kikao cha wavulana wanaojiita super powers. Kwa sasa mchina na muindi wanamuunga mkono mrusi. Pia, tukirudi kwenye uhalisia, mrusi ndiye rafiki pekee wa ukweli wa afrika ila wengine wotee ni wakoloni wa kung'ata n kupuliza. Nia yake ni kutafuta marafiki wa kweli ambao watategemeana kwa kusaidiana kibiashara za kuzinufaisha pande zote bila masharti ya kibepari. Ametengwa na wadhungu wenzie. Huyu ndiye mwanaume pekee aliyeshikilia button ya vita ya 3 ya dunia. Aisee kujihusisha n mrusi ni faida kuliko hasara. Yule atanunua hata dagaa wetu wa kigoma maana anauhitaji, nyanya zetu, makaa ya mawe, dhahabu, parachichi, korosho yani kila bidhaa na bado kutupa kazi urusi na visa rahisi kuliko nchi yeyote ya ulaya. Shida yake hapo nyuma amekuwa na visa vya ubaguzi wa rangi hadi shidaaah. Haitaji malelemama yule mwanaume. Ila ni mwanaume n nusu. Itapendeza kujitenga na dunia, tujisogeze karibu zaidi n mrusi, mchina n muindi kuliko kujihusisha na muamerica na dunia yake ya ukoloni. Nitakuja n uzi kumfafanua mrusi kiundani zaidi, pia kumfafanua kwanini kufanya biashara na mrusi kutakuja na faida kuliko hasara tukizingatia kuwa tutatengwa n dunia
 
Back
Top Bottom