Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Wakuu poleni na majukumu ya kila siku naomba kupata msaada kwa hili tatizo la uvimbe kwenye njia ya haja kubwa kama nilivyoeleza hapo juu, hili tatizo lilianza mwezi uliopita mwanzoni na ulianza uvimbe tu bila maumivu na ukiushika ni kama ni mshipa nikapata ushauri wa mtaalam flani na akaniambia nitumie dawa inayoitwa annusol pamoja na kufanya sitz bath tatizo limekuwa likipungua na kurudi tena na kwa sasa limekuwa na maumivu makali sana msaada tafadhari wakuu.
Habari!

Pole Sana, Jitahidi kufanya yafuatayo.

1. Pendelea kutumia Matunda, Hasa Tunda la PAPAI.. Na mengine yenye kamba kamba.

2.Kunywa Maji Mengi Safi na Ya Kutosha kiasi cha Lita 3.5-5 kulingana na aina ya shughuli zako za kila siku.

3.Tumia Dawa (Zipo ambazo inabd uandikiwe kwenye cheti/daftari la matibabu na zile ambazo unanunua dukani bila cheti)

4.Tumia maji ya uvuguvugu kwa kujiloweka/kukalia sehemu za haja kubwa.

5.Punguza Mazoezi hasa hayo ya kubeba vitu vizito.. Unaweza ukabadili pia aina hiyo ya mazoezi.

6.FIKA HOSPITALI/KITUO CHOCHOTE Cha Huduma za afya kwa Matibabu Zaidi.

Asante na Karibu.
 
Shukrani sana mkuu

Pole kwa tatizo linalokusibu,
Naomba nikushauri jambo juu ya hilo. Inabidi ubadili mfumo wako wa maisha kiasi ili kujitibu. Dawa za hospitali hukupa nafuu ila huenda ikarudi kama ratiba zikaendelea vile vile.
1. Kwa sasa pendelea kula vyakula laini pamoja na matunda kwa wingi, ambavyo vitasaidia kulainisha choo ili usiumie ukiwa unajisaidia.
2. Tafuta mafuta ya nazi/nyonyo na upake eneo la kutolea haja kubwa, husaidia kupunguza maumivu.
3. Ukijisaidia tumia majibya uvuguvugu kujisafisha (inapunguza maumivu, sio lazima)
4. Usikae zaidi ya dakika 3 au 5 chooni, jitahidi ukidhi haja na kutoka, kama haitoki usiilazimishe.
5. Hali ikiisha tulia jitahidi kuzingatia kula vyakula mchanganyiko vyenye kukupa choo.
 
Mkuu walioshauri matunda na kubadili mfumo wa maisha hasa ulaji naungana nao.

Pia mkuu mazoezi sitisha kidogo hasa kama unapiga skwashi na yafananayo na hayo

Pia pombe ipe likizo mkuu

Kingine usitumie nguvu sana kwenye kujisaidia, pia chuchumaa mkuu usikae.

Pressure kubwa wakati wa kujisaidia hupelekea ilo.

Kama upo Dar nakushauri nenda Kairuki hospital pale yupo mzee specialist iyo pande yupo vyema
 
Nashukuru sana kiongozi

Back
Top Bottom