Nimesoma maelezo yenu ama kwa hakika yamenivutia nilikuwa na uvivu wa kuanza kufuga sasa mmenipa moyo wa kuanza.ningependa kuwa na mtiririko mzuri wa kuandika ili iwe rahisi kwa msomaji aweze kupata elimu kwa ufasaha!ila nimefaidika sana kwani kuna ucheshi ndani yake na pia elimu kubwa zaidi kwa moyo huu tutafika mbali sasa ni vitendo vinahitajika.naanza na matayarisho ya banda kwanza ahsanteni.

Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako :)

Asante sana for sharing, swali lang; Je kuku mmjoa anaweza kutaga mayai mangapi kwa mwezi?

Mkuu mimi nilipoona ihi thread niliamua kuendleza kuku waliokuwepo nyumbani walikuwa wanajitafutia chakula wenyewe lakin kwa sasa 50% namimi nawatafutia msosi matetea wapo 13 majogoo 2 niliyanunua mkoani singida.nashukuru kukuwanadondosha mayai kama mvua.tatizo nililokumbana nalo ni maradhi kwa vifaranga walipotimiza mwezi 1 walianza kupofuka macho,kutoa vidonda pembeni ya macho,kusinzia,kushusha mabawa na mafua makali sana vifaranga walikuwa 43 wamepukutka hadi wamebaki 13 nilionana na wataalam wa mifugo dawa walizonpa azikusaidia.chanjo ya kideri nilifanikiwa na kwa sasa nishapata vifaranga wengne zaidi 50 naombeni ushauri jinsi ya kuwapa kinga ya maradh mbalimbal ya kuku wa kienyej hasa vifaranga .

Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako :)
sikutegemea mtu mzoefu kama wewe Newmzalendo utoe post iliyo general kama hii... hebu tupe sababu za kisayansi kusema kuwa kama unataka kufuga kuku kwa ajili ya afya ufuge wa kienyeji tu na wa kisasa ni kwa ajili ya pesa... si vizuri kutoa general statement zinazopotosha kwa sababu watu wengi wanasoma JF.

ha haa haaa haaaa

sijui niwe upande upi hapa. .., labda tujiulize swali moja, kuku wa kisasa hufugwa kwa muda wa hadi kuanzia wiki saba na kuwa tayari kwa matumizi na kuku wa kienyeji hufugwa kwa hadi wiki 20 , je tofauti hii ya muda maana yake ni nini kisayansi?

wanajamvi, ni muhimu kufahamu kuwa katika ufugaji ni lazima uzingatie ufugaji bora kama unataka kulinda afya za walaji iwe umefuga kienyeji au kizungu au kisasa. unachotakiwa kuzingatia ni wakati gani unawapa kuku wako dawa, na upite muda gani kabla ya kutumia product za hao kuku (i.e. mayai na nyama). kila dawa inakuwa na maelezo ya muda unaotakiwa upite kabla ya kuchinja au kutumia mayai endapo utakuwa umewapa hiyo dawa.

Na katika ufugaji wowote wa kuku lazima utakinga na/au kutibu magonjwa iwe ni kuku wa kienyeji au wa kisasa. lazima utawakinga au kuwatibu dhidi ya kideri/mdondo, ndui, homa ya matumbo, gumboro, mafua n.k.

kwa ufupi, kinacho-matter si aina ya kuku ulionao (kienyeji/kisasa) bali ni utaratibu/mbinu gani unatumia katika ufugaji wa kuku wako (i.e. practices).

nawashauri wanajamvi msidhani kuwa kwa kuwa kuku ni wa kienyeji basi ni bora kwa afya- bila kujua kuwa kuku huyo anaweza kuwa na ugonjwa au amepewa dawa siku za karibuni. the same applies kwa kuku wa kisasa!

Vipi kuhusu suala la ladha? Kuku wapi ni watamu waidi?

• Thanks
Reactions: LAT
Naomba kujua uwezo wa kutaga wa kuku wa kienyeji uko vp? I mean ni mayai mangapi labda kwa muda gani? Nasikia kuku wa kienyeji akiwa anataga na unayatoa mayai haumpi kuyaatamia anaendelea tu kutaga bila kuacha ni kweli au maneno ya mtaani tu?
kwa mtago mmoja kuku anataga mayai 10-15 na wengine wanataga mpaka mayai 20. Kwa hiyo kwa mwaka anaweza kutaga mpaka mayai 45......Inawezekana kabisa kuku akaendelea kutaga pale unapompokonya mayai asiyaatamie, lakini pia kuna njia nyingine ya kienyeji niliwahi ikuta kijijini kumzuia kuku asiatamie mayai, ambapo alikuwa anawekwa kwenye maji, hasa sehemu ile ya kifua....

Asante kwa kutufungua macho, na ninashukuru kwa mchango wako.
Kuna tatizo la mahesabu kidogo. Jumla ya gharama ni 1,590,277 na siyo 1,490,277 na kufanya faida kuwa 1,702,523. Kwa kuwa unatumia Msexcel
nakushauri utumie formulas badala ya kutype figures zote:
Column ya mapato( e3)andika =b3*d3 press enter, jibu litakuja pale. Then click kwenye E3 then kwenye right hand lower corner itakuja alama ya msalaba (+), press your left side mouse usiachie na vuta kwenda chini. Fomula itakuwacopied hadi chini yaani E4 itakuwa =b4*d4 nk. Kuweka jumla mwishoni click kwenye cell unayotaka jibu liwe e34 halafu nenda juu kwenye tool bar click
∑ basi jibu la jumla ya namba hizo itakuja,kwanza itajionyesha kwa kuhighlight, au andika =sum(e3:e33) press enter. Fanya hivyo hivyo kwa upande wa gharama, utapata jibu sahihi. Na profit ni =e34-f34. Hii inapunguza makosa madogo madogo ya kimahesabu
Pili tungefurahi zaidi kama ungetueleza una kuku wangapi? na sikuelewa eggies!
Thanks again

kweli Jf ni shule

Wana JF

Msaada wenu unahitajika katika hivi vitu viwili

1. Kuku wangu wa kienyeji nafugia ndani (siyo huria), wameanza kutaga ila mayai yao yanafanana sana na ya kuku wa kisasa wa mayai. Inaniletea tatizo kupata wateja wanahisi ni ya kisasa. tatizo lipo wapi?

2. Nitapata wapi mashine ndogo ya kutotolesha ya kutosha mayai kati ya 30 hadi mia?

Asanteni sana

Tatizo wana Jamii wengi hawajawahi hata kufuga kuku hata mmoja enzi za utoto wao, sasa inakuwa taabu kweli kweli kuwasaidia mawazo how to go about it.

Mama Joe wala usihangaike kwenda Ruvu kutafuta vifaranga wa kienyeji - kama kweli umeamua kufuga kuku kwa nini usianze na majike 30 na majogoo 3 tu - bei ya hao ukiwapata toka mkoani itakugharimu sh 6,000 kila mmoja Jumla inakuwa 198,000/- Tshs.

Baada ya siku 60 hayo majike yatakuwa na vitoto average 10 kila mmoja = utakuwa na vifaranga 300. Utawanyan'ganya mama zao na kuviweka chumba chenye joto linalotakiwa na utawapa chakula na maji.

Utawaruhusu majongoo yaanze kazi yao immediately baada ya kuwanyanganya vifaranga, then after 2 months hao wanataga tena -- Simple circle!! - after 2 year's utakuwa na hao kuku zaidi ya 1000 unaowataka.

Elnino, nimeipenda sana hii coment yako, nashukuru kwa kutufumbua macho mana hata nami nina wazo hili la kufuga, ila sikujua nianzaje! Endelea kutuelemisha zaidi!

Karibu mkuu,
kuku wa kizungu athari zake kiafya ni nyingi kuliko wa kienyeji,unaweza kufuga wa kizungu kwa ajili ya pesa na wa kienyeji kwa ajili ya afya yako :)

Kimaadili ya kiubinadamu na kibiashara ni muhimu kuzingatia afya ya walaji/wateja na sio kupata pesa tu.......ni mtazamo tu!

Hii nzuri sana sijui kwanini haijawekwa kule juu tukafaidi maana nimechelewa
kuiona. Tunaomba muiweke juu kwa faida ya wengine pia.

Similar Discussions

Back
Top Bottom