ok sasa hata sisi tulio nje ya nchi tuataka bibi zetu udeliver kuku so publish your number
nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji,bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje,
kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri ,pros and cons etc.
bye the way nimeanza na Jogoo mmoja,ila natarajia kuongeza kuku within a week,
projections ni kuwa na kuku 1000,hapo ndio nianze kuuza,matarajio yangu ni kuuza via interent-hapa nalenga watu wa DAR,ambao wako bize,i can do delivery maofisini within city center,na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni,e.g mwenge junction,morroco petrol station,etc,malipo via M-pesa,sms banking pia na mahoteli.
sitarajii faida ya haraka ,naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii,au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.
 
nimefurahi sana kukutana na wafugaji hapa.Mimi pia ni mfugaji na kama kweli ndugu huyu ana nia ya kufuga kuku wa kienyeji nampa shauri aendelee.Mimi ni mjasiriamali ambaye pia ni mwalimu wa ujasiriamali.
angalia hapa Home - ICT4TD Learning Centre
hapa tunawafundisha watu kujifunza kiingereza,computer na kifaransa pia tunafundisha ujasiriamali wa kufunga kuku wa kienyeji na samaki. angalia pia Africa Upendo Group .
ukitaka kuniona ama ukitaka kujifunza hatua moja hadi nyingine na kukuonyesha shamba darasa letu na kukufundisha jinsi ya kutayarisha chakula na pia kukusimamia hadi uanze na jinsi ya kutengeneza banda lako hata kama una nafasi ndogo kiasi ngani basi usisite kunipigia simu 0712-308941/0784-869809/0768816262 njoo tutakusaidia na pia ninaimani kuwa kama tuna nia ya dhati hebu tusaidiane hata ikiwezekana tuwe na kama group fulani hivi ya wafugaji na tuweze kupiga hatua.Nina maana ya wale ambao tayari wana mawazo ya kufuga kwani hapa tunaelimishana tu.twende mbele kidogo tuanze sasa kwa vitendo.
sio lazima kuanza na mamilioni hapana.ukiwa tu na banda ndogo na hata unaweza kuanza na kuku mitetea sita na jongoo moja.Tunaweza kujenga vizuri kwenye kichanja na wakaingia kuku wengi tu.
 
Nimeanza na kuku wachache wa kienyeji 12, nataka nifuge kiasili ya huko kwetu, kuku wangu nataka wapate nafasi ya kufanya mazoezi kwa kutembea, kuparura chini kwenye mboji ya miti, kula majani/mboga au nyasi,walale juu chanjani. Nitawapa suppliments nitakazoshauriwa na bwana mifugo.

Eneo sio tatizo, nimeshafanya utafiti kidogo, wadudu wabaya hawapo. Nataka kufuga kwa kufuata kanuni za kilimo hai kwa ajili ya wateja wachache ninao weza kuwamudu.
 
Nami nipo katika mchakato wa kufuga kuku wa kienyeji lakini mtaji wangu ni mdogo kiaina kwani nina kuku wakubwa makoo 6 na Vifaranga 10, ila kuna wadudu (Utitiri) wananisumbua katika banda la kulazia kuku, Naomba kwa anayejua dawa mzuri ya kutumia anisaidie kunifahamishe niweze kukabili hilo suala.
 
Mdau aneyejua ni mahoteli gani makubwa nitaweza kupata oda ya kuku wa kienyeji,tafadhali anijuze coz nataka nimfunike mkenya nelson muguku
 
Utitiri wa kuku...,mdau kashdz- Tumia dawa kwa kunyunyuzia inayoitwa sevin dust, poultry dust,malathion 2% na nicotine sulphate kwa kuku wote, nyunyiza na safisha banda kwa kutumia dawa zilizotajwa hapo juu. Zingatia usafi wa banda, usiache kuonana na mtaalam kwa elimu zaidi. Huo ndo ushauri wangu
 
mimi nafuga kuku wa kienyeji.
wanalipa vizuri mayai yananunulika vizuri tu na kuku wenyewe...siku za sikukuu ndio faida inakua mara dufu..bado sijawa mfugaji mkubwa..nina kuku 70(wazalishaji; majogoo 10 na mitetea 60) na kuku wanaokua wako 100.
 
Asante,
Naomba nikuchape swali, chakula gani unawalisha?
 
mimi nafuga kuku wa kienyeji.
wanalipa vizuri mayai yananunulika vizuri tu na kuku wenyewe...siku za sikukuu ndio faida inakua mara dufu..bado sijawa mfugaji mkubwa..nina kuku 70(wazalishaji; majogoo 10 na mitetea 60) na kuku wanaokua wako 100.

eneo lako ni kubwa kiasi gani la kuweza kufugia kuku mia at once
 
mimi nafuga kuku wa kienyeji.
wanalipa vizuri mayai yananunulika vizuri tu na kuku wenyewe...siku za sikukuu ndio faida inakua mara dufu..bado sijawa mfugaji mkubwa..nina kuku 70(wazalishaji; majogoo 10 na mitetea 60) na kuku wanaokua wako 100.

Average unapata mayai mangapi kwa siku?
 
Mzazi Bobo. Nashukuru sana kwa Ushauri wako umenisaidia kwa kiasi kikubwa sana. sasa tatizo la utitiri nimelikomesha.

Utitiri wa kuku...,mdau kashdz- Tumia dawa kwa kunyunyuzia inayoitwa sevin dust, poultry dust,malathion 2% na nicotine sulphate kwa kuku wote, nyunyiza na safisha banda kwa kutumia dawa zilizotajwa hapo juu. Zingatia usafi wa banda, usiache kuonana na mtaalam kwa elimu zaidi. Huo ndo ushauri wangu
 
Ni wazo zuri tena sana ila biashara matangazo, kuitangaza muhimu kwakua watu wa dar wako busy na ndio stakeholder wako wakuu na wengi wanashinda ma ofisini muda mwingi kwahiyo wanategemea kupata matangazo kwenye internet zaidi, kuna system ambayo iko kwenye mitandao ambayo unaweza kuwapata hao wadau wako kiurahisi zaidi na rahisi kuitumia ni vizuri ungeitembelea ambayo ni Jigambeads.com
 
Kuku wa kienyeji wakifugwa ndani kwenye banda na kupewa vyakula vya kisasa wanaendelea kuwa wa Kienyeji tena?
 
chakula wanachokula kuku wa kisasa ni hicho hicho cha kienyeji
kwani kuna pumba, mahindi, mashudu ya alizeti, dagaa nk,
kwahiyo hatakuwa wakisasa ila watakua vizuri kwa wakati tofauti na wale wanaijitafutia chakula kwani saa ingine wanaweza wasipate virutubisho vyote hasa kwa maeneo ya mjini.

Labda nikufafanulie kidogo.

Kuna ufugaji kuku wa kienyeji wa aina 3

  1. ufugaji huru
Ufugaji huu ni ule wakuacha kuku ajitafutie chakula mwenyewe. Yaani unamfungulia asbh anarudi jioni. Pia huu unaweza kuufanya uwe kisasa kidogo kwa kujaribu kuwaongezea chakula cha ziada (kwa dizaini ya kuwatupia).
Sio wa gharama sana kwani kuku anajitafutia chakula, ila unahitaji kuwa naeneo kubwa.
Ni hatari kwani wezi, wanyama wakali wanaweza kuwashambulia kuku.
Mayai yanaweza kutagiwa porini na usijue yalipo.
Kuku anaweza kuambukizwa magonjwa na ndege wengine au kuku kutoka kwa majirani.

2. ufugaji nusu huru
Ufugaji huu. ni banda ndani ya uzio yaani unawapa chakula na maji kama kawaida lakini hawatoki nje ya uzio. Unakuwa umewatengenezea eneo la kuchezea na kukumbizana.
nao unahitaji eneo kubwa kidogo, kuku wanakua salama dhidi ya wezi na wanyama wakali kwa kiasi fulani.
Utahitji kuwatafutia chakula kwa zaidi ya 50%.

3.ufugaji wa ndani

huu ni wagharama zaidi. kwani kuku huitaji kutafutiwa chakula kwa 100%.
ila kuku huwa salama dhidi ya magonjwa wezi na wanyama wakali.
Tatizo kubwa nivigumu kudhibiti ugonjwa uingiapo banda kwa hiyo inakupasa uhakikishe magonjwa hayafiki.
jingi ne tabia mbaya kama ya kula mayai na kudonyoana inaweza kusambaa kwa haraka.

Kwa hiyo ni methods tu za ufugaji hazibadilishi kuku wa kienyeji kuwa wakisasa.
 
Nami nipo katika mchakato wa kufuga kuku wa kienyeji lakini mtaji wangu ni mdogo kiaina kwani nina kuku wakubwa makoo 6 na Vifaranga 10, ila kuna wadudu (Utitiri) wananisumbua katika banda la kulazia kuku, Naomba kwa anayejua dawa mzuri ya kutumia anisaidie kunifahamishe niweze kukabili hilo suala.

kuna dawa moja initwa akheri powder ni nzuri but kama banda kalo huwa hufanyi usafi utalia na hao wadudu kila siku. Dawa nyingine nia mafuta ya taa unachukua unyoya wa kuku na kuchovya kwenye mafuta ya taa halafu una mpk kuku.
 
chakula wanachokula kuku wa kisasa ni hicho hicho cha kienyeji
kwani kuna pumba, mahindi, mashudu ya alizeti, dagaa nk,
kwahiyo hatakuwa wakisasa ila watakua vizuri kwa wakati tofauti na wale wanaijitafutia chakula kwani saa ingine wanaweza wasipate virutubisho vyote hasa kwa maeneo ya mjini.

Labda nikufafanulie kidogo.

Kuna ufugaji kuku wa kienyeji wa aina 3
  1. ufugaji huru
Ufugaji huu ni ule wakuacha kuku ajitafutie chakula mwenyewe. Yaani unamfungulia asbh anarudi jioni. Pia huu unaweza kuufanya uwe kisasa kidogo kwa kujaribu kuwaongezea chakula cha ziada (kwa dizaini ya kuwatupia).
Sio wa gharama sana kwani kuku anajitafutia chakula, ila unahitaji kuwa naeneo kubwa.
Ni hatari kwani wezi, wanyama wakali wanaweza kuwashambulia kuku.
Mayai yanaweza kutagiwa porini na usijue yalipo.
Kuku anaweza kuambukizwa magonjwa na ndege wengine au kuku kutoka kwa majirani.

2. ufugaji nusu huru
Ufugaji huu. ni banda ndani ya uzio yaani unawapa chakula na maji kama kawaida lakini hawatoki nje ya uzio. Unakuwa umewatengenezea eneo la kuchezea na kukumbizana.
nao unahitaji eneo kubwa kidogo, kuku wanakua salama dhidi ya wezi na wanyama wakali kwa kiasi fulani.
Utahitji kuwatafutia chakula kwa zaidi ya 50%.

3.ufugaji wa ndani
huu ni wagharama zaidi. kwani kuku huitaji kutafutiwa chakula kwa 100%.
ila kuku huwa salama dhidi ya magonjwa wezi na wanyama wakali.
Tatizo kubwa nivigumu kudhibiti ugonjwa uingiapo banda kwa hiyo inakupasa uhakikishe magonjwa hayafiki.
jingi ne tabia mbaya kama ya kula mayai na kudonyoana inaweza kusambaa kwa haraka.

Kwa hiyo ni methods tu za ufugaji hazibadilishi kuku wa kienyeji kuwa wakisasa.

Thanks for the info mi nilikuwa nafikiri kuku wa kienyeji ukiwalisha chakula cha kuku wa kisasa unawaharibu na hawawi wa asili tena
 
Naomba kujua uwezo wa kutaga wa kuku wa kienyeji uko vp? I mean ni mayai mangapi labda kwa muda gani? Nasikia kuku wa kienyeji akiwa anataga na unayatoa mayai haumpi kuyaatamia anaendelea tu kutaga bila kuacha ni kweli au maneno ya mtaani tu?
 
Mkuu mimi nilipoona ihi thread niliamua kuendleza kuku waliokuwepo nyumbani walikuwa wanajitafutia chakula wenyewe lakin kwa sasa 50% namimi nawatafutia msosi matetea wapo 13 majogoo 2 niliyanunua mkoani singida.nashukuru kukuwanadondosha mayai kama mvua.tatizo nililokumbana nalo ni maradhi kwa vifaranga walipotimiza mwezi 1 walianza kupofuka macho,kutoa vidonda pembeni ya macho,kusinzia,kushusha mabawa na mafua makali sana vifaranga walikuwa 43 wamepukutka hadi wamebaki 13 nilionana na wataalam wa mifugo dawa walizonpa azikusaidia.chanjo ya kideri nilifanikiwa na kwa sasa nishapata vifaranga wengne zaidi 50 naombeni ushauri jinsi ya kuwapa kinga ya maradh mbalimbal ya kuku wa kienyej hasa vifaranga .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom