Kwa namna linavyojadiliwa,hapana shaka suala hili lina 'maslahi ya umma'.Ninajaribu kujibu kutoka 'viatu' vya wanafunzi wanaolalamikiwa.Haitakuwa haki kumtaka mwanafunzi aishiye Mabibo Hostel avue ID mara atokapo Chuoni awe anatembea kwa miguu ama kwa usafiri wa gari.Hii ni kutokana na ukweli kwamba akifika getini Mabibo atalazimika kuonyesha ID.
Wale wanaoenda nazo Posta ama Kimara ama kwingineko,wanakabiliwa na changamoto ile ile:wanaporejea Hosteli ama Mabwenini Mlimani watapaswa kuzionyesha na kwa hiyo kwenda nazo mtaani inaweza kuwa sahihi.Ipo hoja ya kuzivua na kuziweka mfukoni mara watokapo getini.Hii nayo haitekelezeki kirahisi kwa sababu upo uwezekano wa kuibiwa ama kupotea na kusababisha usumbufu mkubwa kwa muhusika.Bila ID hawapati huduma na kuzipata inagharimu nishati,nguvu,muda na pesa.
Kwa sehemu kubwa wanafunzi husika wanazo sababu za msingi za kuvaa ID zao.Tujifunze kuvumiliana na kuchukuliana.Kabla ya kutafuta makosa elewa mazingira.